Kwa Mujibu wa Gazeti la Majira, Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe amemtimua katika nafasi yake Bibi Apolonia Mosha ambaye aliteuliwa na Mwakyembe mwenyewe katika wadhifa wa Meneja wa Bandari. Apolonia alichukua nafasi ya Cassian Ngamilo ambaye naye alitimuliwa na Mwakyembe mwaka jana pamoja na vigogo wenzake wa Bandari akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Ephraim Mgawe.
Taarifa za Majira zinaeleza kuwa Mwakyembe amemuondoa mteule wake Apolonia baada ya mteule huyo kushindwa kazi ya kuleta ufanisi alioutarajia Bandarini baada ya kumtimua Ngamilo. Apolonia alikuwa mhasibu kabla ya Waziri Mwakyembe kumteua mama huyo kuwa meneja wa TPA wadhifa ambao ameshindwa kuutumikia kwa ufanisi.
Mwakyembe anatakiwa kujua kuwa tatizo la nchi hii ni kubwa sana katika serikali na mashirika yake. Wengi wa walioshika nyadhifa kubwakubwa hawana sifa hasa za kushika madaraka hayo. Aidha, uteuzi na/au uajiriwa wao umepitia mfumo usioangalia utendaji wa ufanisi. Wengi wao kwa sasa wamekwenda vyuo na kupata Masters ya kuandikiwa na wewe unafikiri huyu ni msomi wa fani husika. Kwa kuteua waliomo ndani na kuwapa vyeo ni kama unatingisha chungu na kuokota mwingine lakini viazi vyote vilivyomo ndani vinafanana.
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka vigezo vya ufanisi ambavyo anayeteuliwa atapimwa kwa vigezo hivyo. Nafasi zote kubwa zitangazwe upya na usaili wa wanaoomba uwe wazi. Kwa Tanzania ya sasa, sifa kubwa ya mwombaji isiwe degree yake ya Masters au PhD kwani hizi ni nyingi sana feki bali uwezo wa muombaji kutegemeana na atakavyoainisha mipango yake na mikakati ya kufikia malengo ya shirika. Upimaji wa utekelezaji wa maengo hayo ufanywe na mashirika ya kimataifa kama PriceWaterHouseCoopers au Enrst and Young, kila mwaka. Akishindwa kufikia vigezo hivyo mkataba unafutwa na kuajiriwa mwingine.
Wapo WaTZ wengi tu ambao wana uwezo wa kufanya kazi hizo kwa ufanisi ila hawapewi nafasi kwa ajili ya ufisadi.
Anza na Bandari halafu utaona matunda yake.
upendeleo
Hivi TPA haina bodi ya wakurugenzi? Inakuwaje waziri anashughulika na meneja wa bandari wakati mkurugenzi mkuu na bodi ya wakurugenzi wapo? Kwa nini asiwajibishe bodi ya wakurugenzi na mkurugenzi mkuu ikiwa wameshindwa kazi yao ya kusimamia utendaji wa kila siku wa watendaji wa ngazi ya chini kama meneja wa bandari? NKwa mtazamo wangu huyu waziri anaingilia kazi zisizomhusu na sidhani kama kufanya hivyo kunalenga kuisaidia bandari.
Tatizo mtu akiteuliwa tu anajisahau kabisa. Mwakyembe aweke 'perfomance' agreement na management wote, ili kila mtu ajue anatakiwa ku-deliver nini kwa wakati gani. Huu mtindo wa watu kuzunguka kwenye corridor kutwa nzima na blackberry vyao unachosha.
Safi sana Mwakyembe kama mtu kashindwa kazi piga chini.
Mkuu hapo umepatia kweli kweli, kama Dk.Mwakyembe ana kawaida ya kupitia maoni ya wana JF basi maoni yako anapaswa kuyazingatia na kuyafanyia kazi fasta; mashirika yetu mengi ya umma yamefikia hatua ya kutia simanzi kutokana na utamaduni wa kuwapatia/kuzawadia vyeo Wakurugenzi wasio na sifa zozote zaidi ya kujuana na jamaa wizarani au Serikalini, vile vile Board hasa hasa board Chairmen na baadhi ya wajumbe wa board wanakuwa karibu mno na wakurugenzi wakuu - hii inaodoa kabisa dhana ya check and balance na wakikuta Mkurugenzi Mkuu ambaye ni mjanja, basi anaweza kugeuza Board nzima kuwa rubber stamp tu ya ku-approve chochote apendacho na kufanikiwa kufanya ufisadi bila woga.
Naku-support 100% ushauri wako kuhusu usahili wa watendaji muhimu kwenye mashirika yetu ya umma, usahili huo wapewe mashirika ya kimataifa ambayo hayana vested interest na wahusika, jamaa hawa wako makini sana na kazi zao hawatilii maanani sana vyeti vya ma PhDs and what have you; wana ku-grill kuona kama una uwezo wa kufanya kazi kiufanisi na weledi na infact uwezi kukuta wameweka lundo la watu wa kukuhoji, mtu mmoja aliye jipanga vizuri ndie anakuhoji kiundani lakini yuko friendly - jamaa hawa ni Pro kweli kweli!! Sasa nenda interview hizi zetu za kienyeji/zilizo pitwa na wakati unakuta Panel ina zaidi ya watu kumi na ushee kila mmoja kapewa karatasi ya swali na jibu, mtu unaweza kufikili unahojiwa kijiunga na chuo fulani vile, na kwa bahati mbaya interview zenyewe ni kiini macho tu.
Hakuna haja ya kuanza kumtafuta mchawi wa udolololaji wa mashirika yetu zaidi ya kijisahihisha sisi wenyewe, bila ku-address tatizo hilo kikamilifu tutaendelea kubaki nyuma daima duni.