Mwakyembe aanza kuwatimua aliowateua Bandarini

Mwakyembe aanza kuwatimua aliowateua Bandarini

Sasa wadhungu husema, "like father like son" nami nasema like boss like appointee. Mwakembe nae ataweka historia ya kuteua makapi na kufukuza kama bosi wake. vigezo viko kichwani mwake na siyo qualifications. Awamu ya nne.
 
Mwakyembe anatakiwa kujua kuwa tatizo la nchi hii ni kubwa sana katika serikali na mashirika yake. Wengi wa walioshika nyadhifa kubwakubwa hawana sifa hasa za kushika madaraka hayo. Aidha, uteuzi na/au uajiriwa wao umepitia mfumo usioangalia utendaji wa ufanisi. Wengi wao kwa sasa wamekwenda vyuo na kupata Masters ya kuandikiwa na wewe unafikiri huyu ni msomi wa fani husika. Kwa kuteua waliomo ndani na kuwapa vyeo ni kama unatingisha chungu na kuokota mwingine lakini viazi vyote vilivyomo ndani vinafanana.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka vigezo vya ufanisi ambavyo anayeteuliwa atapimwa kwa vigezo hivyo. Nafasi zote kubwa zitangazwe upya na usaili wa wanaoomba uwe wazi. Kwa Tanzania ya sasa, sifa kubwa ya mwombaji isiwe degree yake ya Masters au PhD kwani hizi ni nyingi sana feki bali uwezo wa muombaji kutegemeana na atakavyoainisha mipango yake na mikakati ya kufikia malengo ya shirika. Upimaji wa utekelezaji wa maengo hayo ufanywe na mashirika ya kimataifa kama PriceWaterHouseCoopers au Enrst and Young, kila mwaka. Akishindwa kufikia vigezo hivyo mkataba unafutwa na kuajiriwa mwingine.

Wapo WaTZ wengi tu ambao wana uwezo wa kufanya kazi hizo kwa ufanisi ila hawapewi nafasi kwa ajili ya ufisadi.

Anza na Bandari halafu utaona matunda yake.

Mkuu

Viongozi wetu wengi hufanya makosa makubwa sana katika uteuzi na hapo ndipo hata Mwakyembe alipofanya kosa katika kumteua huyu mama. Lakini ni afadhali Mwakyembe ameona amekosea na ameamua kukubali kula matapishi yake kwa kumuondoa kuliko angekomaa na kumuacha mambo yaendelee kuharibika. lakini achukue kosa hilo kama funzo kwake na asirejee makosa hayo in future.

JK alikosea sana kumteua Mkurugenzi wa sasa wa TBC Clement Mshana na mambo yanazidi kuwa mabaya kila siku na Television hiyo inazidi kudumaa kila uchao. Angekuwa makini basi alipaswa kumuondoa Mshana haraka na kuteua mwingine maana kwa hali ilivyo TBC iko ICU now kinachosubiriwa ni tangazo la kifo tu.

Uteuzi una matatizo makubwa sana na viongozi wetu hawako makini wanapofanya uteuzi.
 
Mkuu point zako mbili zina mshiko sana, nianze na point yako ya pili - mimi naona huyu mama hakupewa muda wa kutosha, alafu tusisahau kwamba wakina mama ni binadamu makini sana, nina wasi wasi kwamba remnant ya mafisadi walio baki TPA wanaweza kuwa walimfanyia hujuma ili aonekane kazi haiwezi - wanaume wakati mwingine tuna wivu wa kijinga sana, hawapendi wanawake wapande ngazi.


Point yako ya kwanza mimi na mwezangu tumeizungumzia sana humu, bila ya kutangaza nafasi hizo na watu kufanyiwa usahili na Kampuni za nje ambazo hazina vested interest na mchakato mzima basi Dk.Mwakyembe anaweza kuishia kwenye ku-hire na ku-fire kila siku au tuseme kubadilisha viongozi like bolts in a machine! Akumbuke ni viongozi wachache wa ngazi za juu kwenye mashirika ya UMMA wenye nia thabiti ya kuhachana kufanya kazi kwa mazoea na kulindana, kama kuna umuhimu wa kutaka ku-retain Kiongozi kwenye Shirika fulani basi ashindanishwe na watu wa kutoka nje ya Shirika na sio kusikiliza mapendekezo kutoka Wizarani, kuna baadhi ya Viongozi wanao julikana kuwa ni ma-good orators tu, lakini wanakabidhiwa mashirika nyeti kutokana na urafiki tu - sasa nchi itategemea kuvuna nini at the end of the DAY - got it! dismal performance, alafu tunaishia kutafuta mchawi.

By Janjaweedkuna matatizo mawili,

  1. la kwanza ni uteuzi wenyewe, inaonekana Mwakyembe alikurupuka, na hawakufanya proper vetting, ndio maana hizi kazi zinatakiwa ziwe zinatolewa kwa kufuata utaratibu, Mwakyembe ni mwanasheria, kwahiyo kusimamia bandari bado ni kazi ngumu... shey should advertize for these positions
  2. La pili ni muda, yawezekana kabisa huyo mama hakupewa muda na sapoti ya kutosha


Maybe la tatu ni kuingiza siasa kila kona, sasa Mwakyembe anafanya kazi kishabiki zaidi... who knows, labda dawa zimeanza kumpa side effects mbaya zaidi

Points zenu zinanifanya niamini kwa kiwango kikubwa kuwa viongozi wetu wanakurupuka sana kabla ya kufanya uteuzi na kwa mtaji huo tunaweza kufukuza na kuteua kila siku bila changes.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom