Mwakyembe aanza kuwatimua aliowateua Bandarini

Mwakyembe aanza kuwatimua aliowateua Bandarini

bibikuku

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2011
Posts
832
Reaction score
496
Kwa Mujibu wa Gazeti la Majira, Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe amemtimua katika nafasi yake Bibi Apolonia Mosha ambaye aliteuliwa na Mwakyembe mwenyewe katika wadhifa wa Meneja wa Bandari. Apolonia alichukua nafasi ya Cassian Ngamilo ambaye naye alitimuliwa na Mwakyembe mwaka jana pamoja na vigogo wenzake wa Bandari akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Ephraim Mgawe.

Taarifa za Majira zinaeleza kuwa Mwakyembe amemuondoa mteule wake Apolonia baada ya mteule huyo kushindwa kazi ya kuleta ufanisi alioutarajia Bandarini baada ya kumtimua Ngamilo. Apolonia alikuwa mhasibu kabla ya Waziri Mwakyembe kumteua mama huyo kuwa meneja wa TPA wadhifa ambao ameshindwa kuutumikia kwa ufanisi.
 
Huwa magamba wanaangalia sifa zipi kuchagua au kuteua watu?
 
Tatizo mtu akiteuliwa tu anajisahau kabisa. Mwakyembe aweke 'perfomance' agreement na management wote, ili kila mtu ajue anatakiwa ku-deliver nini kwa wakati gani. Huu mtindo wa watu kuzunguka kwenye corridor kutwa nzima na blackberry vyao unachosha.
 
If you dont deliver then you dont deserve to serve where you are you better resign
 
Safi sana Dr Mwakyembe, maana hauishiikuwateua tu bali unafuatilia na uchapakazi wao!!Fukuza wazembe wote wasije wakaturudisha nyuma.
 
Natamani kama Mwakyembe angekuwa Rais amtimue Kawambwa na wenzake
 
Ni utaratibu mzuri..kama mtu hakidhi viwango kwa nini asitimuliwe...hata kama ni mara 80 timua tu...
 
Hongera Mwakyembe, Hata kama umemteua kama ana under perform unamtemesha sio kiti cha utemi au uchief
 
Safi sana na hata ikibidi timua mara mia sio huu mtindo wa kufanya kazi kwa mazoea!

Sent from my BlackBerry 9980 using JamiiForums
 
ushabiki wa kivyama sio mzur mtu anapofanya mazuri msifie tu! mkuu
Ni kweli kabisa Mkuu anayestahili kupongezwa lazima apongezwe

Tatizo sisi Watanzania mtu asipochukua hatua tunalalamika akichukua tunaanza kuleta vimaneno vya kejeli

Songambele Mwakyembe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom