Mwakinyo Asaini Mkataba wa Tsh. 232m Marekani, mwenyewe afungua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
collage-2.png
Taarifa ni kuwa bondia namba moja Tanzania, Hassan Mwakinyo amefanikiwa kusaini mkataba wa kucheza ngumi nchini Marekani wenye thamani ya Sh milioni 232 chini ya bondia wa zamani na promota Dmitriy Salita wa Kampuni ya Salita Promotion.

Mtanzania huyo ambaye kwa sasa anaishi na kufanya mazoezi nchini Marekani amevuliwa ubingwa wa Afrika ABU ikiwa imepita miezi kaadha tangu Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Duniani ‘WBF’ kumvua mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa watu wake wa karibu, wamekiri kuwa moja ya jambo linampa kiburi kwa sasa bondia huyo ni baada ya kufanikiwa kusaini mkataba na Kampuni hiyo ya Salita Promotion chini ya Mmarekani Salita mwenye asili ya Ukraine.

“Tatizo watu wengi wanashindwa kumuelewa Mwakinyo nini ambacho kwa sasa anakilenga katika ngumi maana ndiyo kazi yake hivyo kitendo cha yeye kupoteza mikanda ya ubingwa wa WBF na ABU kwake imekuwa ni jambo la kawaida kwa sababu amesaini mkataba na promota mkubwa nchini Marekani anaitwa Dmitriy Salita ambaye zamani alikuwa bondia.

“Mkataba aliosaini unafika milioni 232 japo kuwa bado wenyewe wamekuwa wakifanya ni jambo la siri kwa kuwa baadhi ya mambo bado hayajakamilika lakini ni kwa sasa watu wasahau kuona Mwakinyo akicheza tena hapa nchini kwa kuwa anataka kupigania mkanda mikubwa ya ubingwa,” alisema mtoa taarifa.

Alipotafutwa Mwakinyo alisema: “Ni kweli nimesaini mkataba ila muda wa kuweka wazi ukifika basi nitakwambia kila kitu ila kwa sasa nimekuwa nikiendelea kujifua hapa Marekani maana malengo yangu ni kupigana katika kuwania mikanda mikubwa na mabondia wa kubwa.”

Source: Global Publishers
 
Kila mtu na ndoto zake na malengo yake, jamaa yupo kwenye harakati za kutimkza malengo yake. Sio unakubali kupigwa pigwa migumi ya kichwa tu unastaafu meno huna, hela huna, akili kichwani zisharuka, apige hela ndio wakati wake, akiteleza tu, wakati ukuta.
 
Kila mtu na ndoto zake na malengo yake, jamaa yupo kwenye harakati za kutimkza malengo yake. Sio unakubali kupigwa pigwa migumi ya kichwa tu unastaafu meno huna, hela huna, akili kichwani zisharuka, apige hela ndio wakati wake, akiteleza tu, wakati ukuta.
Sio unakubali kupigwa pigwa migumi ya kichwa tu unastaafu meno huna, hela huna, akili kichwani zisharuka
 
Mwakinyo inawezekana akawa ndio Diamond au Samatta wa ngumi wa Tanzania anapigania sana pesa huyu ndugu yetu naomba maombi na dua zote zimuombee ili atuwakilishe vyema
Ni bongo pekee ndio wanaweza kusifia kitu au mtu kwa tetesi tu pasipo kuthibitisha kwanza ukweli wa taarifa. Yaani mtu anaandika kuwa source ni mtu wake wa karibu halafu mtu anafikia kuamini taarifa moja kwa moja.

Inawezekana ni kweli hii taarifa au inaweza kuwa sio kweli ameitengeneza Mwakinyo ili aonekane maadili yake ni makubwa ndio maana amekataa kupigana kwa mil 46.
 
Mwakinyo inawezekana akawa ndio Diamond au Samatta wa ngumi wa Tanzania anapigania sana pesa huyu ndugu yetu naomba maombi na dua zote zimuombee ili atuwakilishe vyema
Kabisa mkuu watu wanapenda kwenda extra mile kwenye industry zao ndio wanaopandisha thamani kazi zao pamoja na industry kwa ujumla ndio maana bongo movie tangu afariki kanumba imeangukia sio kwamba hakuna vipaji zaidi ya kanumba la hasha bali jamaa alikuwa anajitihada na maono ya mbali zaidi ni kama anachokifanya sasa hivi Diamond Platnumz kwenye industry ya Muziki kafanya kila jambo kubwa na still ana kiu zaidi ya hapo.Binafsi nakuunga mkono Mwakinyo huyo Twaha wanaompamba ngumi zikianza kumtumpa mkono hawa hawa wabongo wanaomsifia wataanza kumkataa na hawatamkumbuka kwa chochote
 
Hiyo 232 million ni kwa mwaka? Siyo hela nyingi. Ni approximately $90000 ambayo ni $7500 kwa mwezi. Bado kodi na living expenses. He needs to be advised.
Ni kweli ila kwa kuanzia siyo mbaya, vinginevyo atajikuta anaingizwa kwenye kile chama bila kujua, kuna watu wanafikiri malipo makubwa yanatokana na kupigana tu au kuimba tu nk, ukiona mtu analipwa malipo ya ajabu yaani makubwa sana basi jua ni member wao tayari, zaidi ya hapo utalipwa kawaida tu, na hii ni kote iwe kwenye ngumi, mziki au basketball ndio mfumo wenyewe ulivyo nk.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom