Mwakapugi atajwa Kesi ya Richmond | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakapugi atajwa Kesi ya Richmond

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 10, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tuesday, May 10, 2011


  MRATIBU wa Maboresho katika Ofisi ya Rais, Ikulu, Singi Madaka, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond, Naeem Gire, alihudhuria kama mjumbe kikao cha majadiliano ya rasimu ya mkataba na timu ya wataalam iliyoundwa na Serikali. Madaka aliiambia mahakama hiyo kuwa, katika kikao hicho, Gire alitambulishwa na Mohamed Gire ambaye naye alijitambulisha kama Mwakilishi na Msemaji Mkuu wa kampuni hiyo kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

  Madaka ni shahidi wa nne katika kesi ya kughushi na kutoa taarifa na hati za uongo inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Richmond Tanzania, Naeem Gire. Katika ushahidi wake, Madaka alidai kuwa, Aprili mwaka 2006 akiwa Kamishina Msaidizi, Sera za Madeni katika Wizara ya Fedha kabla hajahamia Ikulu mwaka 2007, aliitwa na Katibu Mkuu wa wakati huo, Gray Mgonja na kumuagiza kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa wakati huo, Arthur Mwakapugi ili akamuelekeze kazi ya kufanya.

  Alidai kuwa, alipokwenda aliwakuta maofisa wengine kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wengine kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. "Tukiwa hapo, Mwakapugi alitueleza kuwa nchi iko kwenye dharura kuu ya umeme na kwamba tunaweza kuingia gizani wakati wowote hivyo zinafanyika juhudi za kutatua tatizo hilo kupitia zabuni ya kupata wakodishaji wa kufua umeme wa dharura iliyokuwa imeitishwa na Tanesco.

  "Kwa mujibu wa zabuni ile, Tanesco walikuwa wametoa taarifa kwamba, wazabuni wote walikuwa hawafai, hivyo Serikali ilikuwa inatafuta njia nyingine ya dharura kupata ufumbuzi wa tatizo hilo ambapo Wizara ya Nishati na Madini iliamua kuitisha makampuni yale yale nane yaliyoomba zabuni awali ili yatoe ufafanuzi wa kitaalam kuhusu uwezo wao wa kutatua tatizo hilo," alidai Madanka.

  Aliendelea kudai kuwa, baada ya hapo iliundwa timu ya wataalam yeye akiwa Mwenyekiti na kazi ya timu hiyo ilikuwa ni kupokea majina ya makampuni manane na kuwasilisha majumuisho Wizara ya Nishati na Madini. Alidai kuwa kwa msingi wa maelekezo hayo Aprili 22-24, mwaka 2006 timu hiyo iliagizwa kukutana na kampuni hizo nane katika hoteli ya Protea kwenye chumba cha kufanyia kazi ambapo kampuni saba tu ndizo ziliwasilisha maelezo yao isipokuwa Kampuni ya Gapco.

  Wakati akiendelea kutoa ushahidi wake Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro, aliiomba Mahakama ipokee nakala ya ripoti hiyo kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo lakini Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alipinga kupokelewa kwa nakala hiyo kwa madai kuwa haikua nakala halisi hivyo haifai kupokelewa kwa mujibu wa sheria. Akiendelea na ushahidi wake Singi alidai kuwa baada ya ripoti hiyo ya wataalam kukabidhiwa Wizara ya Nishati na Madini, Juni mwaka, 2006 aliitwa tena na Mgonja na kutakiwa aende kwa Mwakapugi ili akaendelee na kazi waliyokuwa wameianza. Akiwa kwa Mwakapugi alikutana na maofisa wengine na kuwaeleza wajadili kwa kina juu ya mapendekezo ya Kampuni ya Richmond kuhusu kutatua tatizo la umeme.

  Baada ya hapo, shahidi huyo alidai, kuwa Juni 5, mwaka 2006 walikutana na wawakilishi wa Richmond katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Dar es Salaam (DICC) kwa ajili ya majadiliano ya rasimu ya mkataba, ambapo waliohudhuria walikuwa Julius Sarote kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mohamed Gire na Mwanasheria wao, Curtbet Tenga na Naeem Gire. Alidai kuwa rasimu ya mkataba iliainisha vipengele vyote kuhusu masuala ya fedha, kiufundi, jinsi ya kuendesha mradi na muda wa kukamilisha mradi wenyewe na kwamba katika kusaini mkataba, Kampuni ya Richmond iliwakilishwa na Mohamed Gire na Serikali alisaini yeye (Madaka).

  Shauri hilo litaendelea leo.

  Mwakapugi atajwa Kesi ya Richmond
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini wote waliotajwa wasijiuzulu kazi zao mpaka wa prove innocent? Wajaribu kama Kenya washitakiwa wote wa Kenya wanajiuzulu
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamna m-bongo asiyependa madaraka!! Akijiuzuli ale wapi? Hata kama ungekuwa wewe, ungejiuzulu?? Think!!
   
 4. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mwakapugi alishaondoka kiitambo lakini segerea yamngoja
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  Pengine kila mtu alitarajia baada ya jairo anaefwata ni aliekuwa katibu mkuu arther mwakapugi
  mh rais najiuliza hivi either umelogwa ama lah maana karatasi nyingi zilionyesha khusika na utapeli
  wa mamilion kwa njia ya huyu bwana sasa na hii ya leo hii mwananchi huyu bwana amekuwa akichangisha tpdc,tanesco miaka yake na kampuni nyingine kadhaa ..ssasa swali langu najiuliza huyu kikwete kawekewa nini na bado najiuliza
  kuna uhusiano mkubwa kati ya hizi hela na huyu mh sio hivi hivi tunalalamikia lakini ukweli utakuja kufichuliwa
  kila la kheri cag
   
 6. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kama ktk kesi ya richmond ametajwa basi lazima sheria ni msumeno lazima awe prosecuted and face justice to save the public image and good governance!
   
 7. t

  testa JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2014
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Nafikiri kama alitenda dhambi leo adhabu ya Mungu inamsubiri
   
 8. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2014
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Jamani kesi hii ni kiini macho. Mwenye kesi aliyesemwa kwenye mkutano mkuu yupo pembeni a kula bata , wanaangaika na vidagaa
   
 9. c

  chegreyson JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2014
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 60
  Uhuru Kenyatta rais wa Kenya ameshitakiwa ICC,alijiuzulu lini.Wachakuandika uongo wa mchana kweupe.
   
Loading...