Mwaka ule ikuwaje Mwakyembe akatamka haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka ule ikuwaje Mwakyembe akatamka haya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jul 18, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Najua naweza kuwa naudhi wengi lakini pia nadhani JF is where we dare , baada ya uchaguzi mkuu mwaka ule nakumbuka KAFU waliporwa ushindi na watu walikufa chini ya uongozi wa Mkapa .KAFU waliendelea kupiga kelele sana na walikuwa na point wakati ule , lakini kwa mshangao dakitari wa sheria bwana Mwakyembe ambaye leo anasema ni mzalendo alisimama na kuishauri serikali kumkamata Seif Sharrif na kumweka rumande na afunguliwe mashitaka ya uhaini .Baada ya siku chache Mwakyembe nadhani aliukwaa Ubunge wa EA .Wakati na sasa tofauti yake nini ? Upi uzalendo zaidi ? watu kufa na tena kwa kudai haki yao ya kuporwa kura zao ama leo kulia na mafisadi ndani Chama chake ambacho kilifisadi kura za watanzania wa kule visiwani na yeye hakuona huruma alishiriki ufisadi ule in a way na hakujali hatma ya Tanzania yangu ? Leo etu anaitwa hero ? Mnisaidie kuelewa hili jamani mie bado siamini na sijajua kwa nini Mwakyembe alitoa kauli ile na kumtaka Mkapa amkamate Seif kama mhaini .
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hakuna mtu hata huko CCM anayaweza kujua Mwakyembe aliingiwa na dudu gani jamani akanisaidia kuondoa hisia hizi moyoni mwangu na nijenge imani kwa Mwakyembe ?
   
 3. F

  FM JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa dalili za kuonyesha uzalendo zimeonekana baada ya kuwa alishafanya kosa kama unavyosema, basi wazi kuwa kuna dalili ya ungamo. Alifanya kosa, amejirekebisha. Hukumu yake iko mikononi mwako
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 0
  na hakuna muandishi wa habari aliyemuuliza kuhusu "aliyeyafanya nyuma na kuungama"?
   
 5. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,099
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  waandishi wetu jamaniii si kama ujuavyoo ile kwa sasa ni career of chance sio choice!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  yaani uliwataka wakumbuke hilo wakati wao kuwahoji viongozi ni bonge la ujikooo???
   
 6. B

  Bwassa Member

  #6
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 15
  Pamoja na kuwa naweza kutofautiana na Dk.wakyembe, lakini wakati ule alikuwa sahihi kutamka kuwa "Seif Shariff Hamad, alikuwa mhaini na akamatwe". Kura zinaibwa kote, isipokuwa Pemba tu, ambako CUF siku zote inashinda kihalali! Seif anawashawishi watu waingie mitaani kuandamana, si yeye wala kiongozi yeyote wa CUF anayeshiriki. Inalalamikiwa kuwa waandamanaji wamepiwa risasi na kuuawa, lakini hakuna anayezungumzia polisi aliyechinjwa na kukatwa kabisa kichwa kwa jmbia, alipokuwa kazini! Seif, na viongozi wenzake walijua nini kitatokea na walitaka kutumia hiyo kuwa ni "Political Mileage", lakini imeshindwa vibaya! Amegombea mara tatu sasa na ameshindwa na anataka tena! Angekuwa hana lake jambo, angemwachia mwana-CUF mwingine agombee! Kura kuibwa ni "danganya toto tu". Haiwezi kukubalika! Wapemba, hasa baadhi ya viongozi wa CUF, wanadai wananyanyaswa, lakini wana vitega uchumi kibao, Majumba, Mashamba, Maduka, Teksi n.k. Unguja na Tanzania Bara! Makamu wa Rais Mpemba, na tusiombee mabaya, JK akiitwa na Mwenyezi Mungu kesho subuhi, Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano atakuwa kutoka Pemba! Acheni siasa za ulalamishi!

  Bwassa
   
 7. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyo Mwakyembe wakati huo hakuwa mwanasiasa alizungumza kama nani na katika occasion gani? Mie sina kumbukumbu ya tukio hilo, hebu liweke sawa.
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,812
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Tunaomba quoted source ya maneno aliyosema mwakyembe siku hiyo.
   
 9. M

  Mitomingi Senior Member

  #9
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe anapatikana na anaweza kuulizwa juu ya hii kauli yake , alimshauri Mkapa na baadaye ndipo akawa Mbunge wa EA hata mimi nakumbuka .Hivi kusema watu waingie mtaani kupinga matokeo ya Uchaguzi ni uhaini kumbe kwa Tanzania ?Je adhabu ya watu kupinga matokeo yab kura zao kuibiwa ni kuwapiga risasi za moto ?
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Jul 20, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,096
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Hii habari tumeingizwa mjini kuijadili bila kuelezwa kuwa ushauri huu ulitolewa lini na wapi-source ya data! Au tuseme Mwakyembe alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Mkapa?
   
 11. M

  Mitomingi Senior Member

  #11
  Jul 20, 2009
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu rejea wakati wa uchaguzi mkuu na mauaji ya Zanzibar .Kama ulikuwa mdogo ingia Library pata habari uje .Mwakyembe hajaanza kuwa Mbunge jana ni baada ta matamshi haya ndipo akaukwaa Ubunge wa Mashariki .
   
 12. E

  Engineer JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lunyungu,

  Hiyo habari ya Dr. Mwakyembe ipo na hapa Kyela inajulikana kwamba alitetea kuuawa kwa raia na kuisafisha CCM ili apewe ubunge wa East Africa.

  Kuna madudu mengi ya Dr. ataulizwa hapo mwakani. Sababu iliyoudhi watu hapa ni kumsingizia huyo kijana wa UK kwamba ni fisadi au anapewa pesa na mafisadi wakati hakuna hata tone la ukweli. Jamaa anajulikana hapa Kyela kama mtu safi na asiyependa makuu kabisa.

  Dr. atofautiane na huyo jamaa na wachambuane kwa sera, lakini kwa ujinga na propaganda aliozoanza kuna watu wamejiandaa kumuumbua kweli hasa kuhusu hayo mauaji na pia kuiba wajumbe wa CCM na kwenda kuwaficha Rungwe wakati wa uchaguzi ndani ya CCM.

  Mimi nimewaambieni Kyela kutakuwa na kazi kubwa 2010.

  Mpaka sasa huyo jamaa hajaanza kumjibu Dr. Kuna waandishi nasikia walimfuata kumwambia ajibu akawaambia ukijibizana na kichaa nani anakuwa kichaa zaidi?
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Engineer mimi nilishikwa na mshangao sana kwamba hakuna Mtanzania anakumbuka mkasa huu ambayo baadaye alipewa Ubunge wa EA .Nataka mjue kwamba Mwakyembe might be a good guy na rafiki wa Watanzania kwa namna moja lakini he is aleading opprtunist.Inatakiwa aombe msamaha juu ya matamshi na ushauri wake kwa Rais kwamba Seif akamatwe kwa uhaini huku akiwa mganga wa sheria na anajua kwamba Zanzibar is not a state bali mkoa tu ule .
   
 14. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Alaah kumbe! Hoja hii imeletwa ikiwa ni harakati za kum-discredit Mwakyembe kwenye uchaguzi ujao!

  Kama walivyosema wengine hapa inabidi tupewe full story ya mazingira yaliyosababisha Dr. Mwakyembe kutamka maneno hayo. Kama Seif Sharrif alitamka ama alidhihirisha vitendo vilivyoashiria uhaini, Mwakyembe alikuwa na haki ya kutamka hivyo, kama alivyofanya. Yes, kama Dr. wa Sheria asingeliweza kukurupuka tu na kutoa matamshi mazito kama hayo bila sababu. Lazima sababu tena ya msingi ilikuwepo. Tutakuwa hatumtendei haki iwapo tumhukumu kwa kuwa tu kuna mtu anamezea mate na anataka kuchukua kiti chake cha Ubunge mwakani!
   
 15. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #15
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Njia ya mwongo siku zote ni fupi hata huyo aliyekutuma kuandika hiyo thread atajulikana siku c nyingi kuwa yye si mwana Igunga
   
 16. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,837
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145


  Boramaisha
  Mie sitoki Kyela na wala sijui huko wanaishi vipi .Mimi nime hoji hili si mara moja wala mara mbili .Swali langu halina mahusiano na siasa zao za majitaka huko CCM.Mimi nauliza kwamba leo aweje hero wa Taifa wakati alishindwa kuona mauaji ya Watanzania wale kwa dhuluma ya Chama chake kuiba kuiba kura .Alitamka maneno yale akijua Zanzibat si Nchi na bado alitaka CUF wakamatwe na Seif Sharrif kwa msimamo wa Chama chake kupinga wizi wa kura.Je katika kumbukumbu zako kuna jambo lolote lilifanywa na wana CUF la kuhatarisha usalama wa Nchi ? Alichinjwa Askari ilikuwa ni baada ya wao kutumia risasi za moto kuwaua raia kisa wanaipinga CCM.

  Rejea tena maneno ya Munishi kuna Youtube yake hapa JF .Ushabiki hakuna bado naomba majibu kama wasemaje wake mpo hapa nipeni majibu .
   
 17. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lunyungu, hata kama hutoki Kyela it amounts to the same thing. Swali lako ni la kishabiki kuliko kimantiki. Why ask it now? Huoni kwamba hoja yako imepitwa na wakati? Sasa hivi tuko kwenye operation Zinduka!
   
 18. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,069
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kwani Seif alitakiwa agombee mara ngapi ndo ionekane mwisho wake wa kugombea urais wa zanzibar??

  I dont get the connectionor the point you want to make on the wapemba kuwa na vitega uchumi Vs kunyanyaswa
   
 19. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,069
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Ushauri wake wa kutaka Seif akamatwe na ashtakiwe kwa uhaini ulikuwa wa kipumbavu ndo maana haukuzingatiwa.Hatuwezi kuongoza nchi kwa jazba za viongozi wa aina ya Mwakyembe..By the way i dont look at him as among the wazalendo to this country.Iam sorry
   
 20. M

  Masatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,286
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Lunyungu yupo sahihi katika hili, imefika wakati hawa wanasiasa tunao waita "wazalendo" tuwe tunawafanyia background check na kwa kufanya hivyo mara moja utawajua wakweli na wanafiki.

  Dr Mwakyembe alitamka maneno hayo dhahihri na shahiri! na ni kweli muda mfupi tu baada ya hapo "akazawadiwa" ubunge wa afrika masharika and the rest is history...

  Historia ita mhukumu Dr Mwakyembe kwa unafiki wake na ndio maana mwandishi huyu alikuwa na haya ya kusema kuhusu Dr Mwakyembe;

   
Loading...