Mwaka Mmoja baada ya Magufuli, Uvuvi Haramu unadaiwa kushamiri kwa Kasi Ziwa Victoria

Kabla ya ujio wa serikali ya Magufuli 2015.
Samaki waliadimika ndani ya Ziwa Victoria,kutokana na uvuvi haramu uliokuwa umeshamiri.

Hadi ikapelekea Viwanda vingi vya vya kuchakata na kusafirisha minofu ya Samaki,katika kanda ya ziwa victoria kupeleka nchi za nje kufungwa.

Hali iliyopelekea kudumaa kwa uchumi wa taifa na kukua kwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa waliokuwa watumishi wa sekta ya viwanda vya samaki katika kanda ya ziwa.

Ulipokuja utawala wa John Pombe Magufuli,ulisimama kidete kupambana na tatizo la uvuvi haramu pamoja na kuzuia uingizaji wa nyavu haramu na zenye matundu yasiyokidhi viwango stahiki nchini.

Ikiwa pia pamoja na kuwachukulia hatua kali wale waliobainika kuwa na hatia ya vitendo hivyo.Ikiwemo kuziteketeza zana zote haramu zilizokamatwa katika zoezi hilo kitaifa.

Pia serikali ikachukua hatua ya kusimamisha kwa muda,shughuli za uvuvi katika ziwa victoria nchini Tanzania.
Ili kuwapa samaki nafasi na muda wa kuzaliana ili kufidia ombwe kubwa lililokuwepo.

Muda mfupi haadae tukashuhudia matunda ya zoezi lile.

Kwa ongezeko la samaki katika ziwa victoria na kupelekea hadi kutosheleza uzalishaji katika viwanda vya kuchakata minofu ya samaki kurudisha shughuli zao mahali pake tena.

Hali ikawa hivyo katika kanda ya ziwa na kuleta ahueni ya kipato na afya kwa wakazi wa eneo husika pamoja na mikoa mingine ya nchi hii.
Ikiwemo na nchi kadhaa za jirani kama Rwanda na Congo DRC.

Mwaka mmoja baada ya kifo cha John Pombe Magufuli na kuondoka kwa serikali yake.

Tunashuhudia kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Tatizo la kuongezeka kwa kasi tatizo la uvuvi haramu kwa kutumia nyavu haramu na matumizi ya Baruti.

Hali ambayo inatishia upungufu au kutoweka kwa samaki katika ziwa Victoria na kupelekea matatizo ya kiuchumi kwa wananchi kama ilivyokuwa awali kabla ya Magufuli kuingia madarakani.

Je, Hali hii inatokana na serikali iliyopo kutojali kudhibiti tatizo la uvuvi haramu?

Au kelele nyingi tulizokuwa tukizisikia hadi kutoka ndani ya bunge la JMT.

Ni kiashiria kuwa moja ya waliokuwa wanufaika,ni pamoja na baadhi ya vigogo wa serikali wakiwemo pia baadhi ya wanasiasa na wabunge wetu na ndio sababu ya ukimya huu?

Pamoja na tatizo hilo kuwa tishio kwa uchumi wetu kitaifa na kutokana na kodi inayopatikana kutokana na usafirishaji minofu ya samaki nchi za nje?
jana wamethibitisha
 
Back
Top Bottom