Mwaka huu nimeamua kurudi shule, ushauri wenu ni muhimu

Malimi Jr

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,243
2,666
Heri ya mwaka mpya wakuu. Naenda moja kwa moja kwenye mada.

Hii ni baada ya harakati za hapa pale za kusoma kwa kuungaunga hatimaye nimepata vigezo vya kujiunga na digrii.

Na digrii yangu nitasoma facult ya elimu hilo sina namna nalo, nalazimika kusoma kitivo hicho kwa sababu mbalimbali ambazo sitazitaja hapa.

Ushauri naohitaji kutoka kwenu ni course gani nisomee ambayo kwa sasa ina manufaa maana sina uzoefu wa mambo haya.

Ikumbukwe sisomi kutafuta ajira ila nasoma kupanua maarifa na pia nijiongezee kipato kupitia elimu.

Nitaheshimu sana ushauri wenu wakuu.

Ahsanteni.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Hutaki kutuambia sababu zilizokufanya uamue kurudi shule halafu unataka tukuchagulie course ya kusoma. Una akili kweli?

Hiyo hela ya kulipia ada na gharama nyingine. Nunua hata toyo uzungushe vichwa.
 
acha uoga wa maisha, wekeza muda wako kutafuta pesa.

kutafuta elimu ya darasani ukubwani ni kupoteza mda na resources.

it's your wish to work on my advice or to ignore it.
 
Soma

1.. Bachelor of Education in Adult Education and Community Development (Bed Adult).(Udsm)

2... Bachelor of Education in Policy Planing and Management (Bed PPM). (Udom)

2.. Bachelor of Education in Psychology (Udsm)
 
acha uoga wa maisha, wekeza mda wako kutafuta pesa.

kutafuta elimu ya darasani ukubwani ni kupoteza mda na resources.

it's your wish to work on my advice or to ignore it.
Mkuu mbinu za kutafuta hela zipo nyingi sana.

Kusoma pia ni mojawapo ya mbinu za kutafuta hela.

Ile sauti ya upole ya ndani kabisa ya moyo wangu inaniambia nirudi shule.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu haya mambo ya kusoma soma yameathiri uchumi wangu kwa sehemu kubwa, mbaya zaidi hata vijana tuliokuwa lika moja ambao hata wengine waliamua kutokusoma na kupambana na maisha yao siku hizi wanafamilia zao na watoto wao harafu mtaani huwezi amini ndo naanza kutafta mke na maisha bado ni yakutafta ajira, inshort kusoma ni kulemaza akili
 
Mkuu kama ulisoma kuanzia la kwanza hadi kiwango ulichonacho bila kukwama njiani na haujapata ajira, hapo lazima uchukie kusoma.

Ila mimi nilisimama njiani kucheki mishe zingine mtaani. Sasa narudi shule huku mishe zangu zikiwa angalau zinakaunafuu.

Sasa hivi nahitaji ni kozi gani ipo makini idara ya elimu.

Kwenye familia yetu hatuna hela za kutamba mtaani, jamani hata mwenye digrii angalau apambishe historia ya marehemu na yeye akose kweli?

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Kama umepata nafasi ya kusoma wewe nenda kapige kitabu usisikilize wanaokuambia eti kusoma ni uoga wa maisha utakuja kuona umuhimu wake mbeleni Mimi mwenyewe ninatamani Sana kurudi shule Mungu akipenda mwakani nitaenda.Kila la heri
 
Asante sana mkuu kwa kunitia nguvu, hakika ushauri wako nitaufanyia kazi.

Hata nawe pia Mungu akutilie wepesi ili mwakani uweze kuanza rasmi.

Safari ya kusoma ni ngumu sana ila naamini Mungu atakuwa upande wetu.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Soma

1.. Bachelor of Education in Adult Education and Community Development (Bed Adult).(Udsm)

2... Bachelor of Education in Policy Planing and Management (Bed PPM). (Udom)

2.. Bachelor of Education in Psychology (Udsm)
Samahani mkuu naona namba 3 umetaja na psychology ,nauliza ikoje soko lake kwenye mkutadha wa elimu kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom