Mwaka 2020 tutaukumbuka kwa vituko vya CHADEMA kuanzia Lockdown hadi wabunge 19 wa viti maalumu!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,747
2,000
Kwaheri 2020 Karibu 2021.

Tutaikumbuka 2020 kwa ushindi wa kihistoria wa CCM ambao haujawahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa kufeli kihistoria kwa Chadema kwa kupata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa tukio la Chadema kujiweka lock down na baadae wale waliotoka lockdown wakaitwa Covid 19 baada ya kukubali kurejea bungeni na kuapishwa na Spika Ndugai katika viwanja vya bunge.

2020 Chadema ilifanya vituko vingi kuliko siasa.

Nawatakia nyote Heri ya Mwaka Mpya 2021!

Maendeleo hayana vyama!
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
27,076
2,000
Tutaukumbuka kwa CCM kutumia mabilioni na mabavu ya vyombo vya dola kuwaondoa wapinzani bungeni halafu kupitia vyombo hivyo hivyo na mabilioni mengine kuwaingiza wapinzani uchwara (covid 19) bungeni kwa mlango wa nyuma.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,104
2,000
Nakumbuka kituko cha mponya corona na kiki za vitambulisho vya wamachinga. Alilazimika kuvikana wakati wa kampeni kwamba "haikuwa lazima". Alipobanwa na mwanasheria nguli kwamba arudishe hela, akapinduka tena.

Mponya corona anayependwa na watanzania akapiga magoti kubembeleza kura kule Njombe.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,288
2,000
Kituko cha karne ni Tanzania kuimaliza Corona kwa maombi ya siku 3, huku tukishindwa kuomba kuumaliza ukimwi na Marelia.

Tunaomba 2021 Hollywood wafunguwe branch Tanzania kuna talent za hali ya juu, mtu anaigiza mkavu kabisa wala hacheki.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,421
2,000
Chadema haijafeli mmelazimisha kuifelisha kwenye ule uchaguzi feki wa maigizo mliofanya mwaka huu, watu wazima mlifanya mambo ya kitoto ambayo hata watoto wenyewe wakiona watashangaa.
 
Mayonene

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
1,598
2,000
Tutakumbuka 2020 kwelikulikuwana vituko sana huu mwaka tulisahau kuwa sisi ni Tanzania ya viwanda wakati wa uchaguzi, tukasahau ndege za keshi, tukasahau fryover, tukasahau Stglazgoji na esijiara. Tukakumbuka kuwa bima ya afya ni muhimu, madeni ya korosho na ya pamba, tukakumbuka barabara na umeme wa Kigoma na miradi yake ya umeme. Ha hahaaaaa
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,747
2,000
Chadema haijafeli mmelazimisha kuifelisha kwenye ule uchaguzi feki wa maigizo mliofanya mwaka huu, watu wazima mlifanya mambo ya kitoto ambayo hata watoto wenyewe wakiona watashangaa.
Kwahiyo CCM haikupata ushindi wa kishindo?!
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,530
2,000
Kwaheri 2020 Karibu 2021.

Tutaikumbuka 2020 kwa ushindi wa kihistoria wa CCM ambao haujawahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa kufeli kihistoria kwa Chadema kwa kupata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa tukio la Chadema kujiweka lock down na baadae wale waliotoka lockdown wakaitwa Covid 19 baada ya kukubali kurejea bungeni na kuapishwa na Spika Ndugai katika viwanja vya bunge.

2020 Chadema ilifanya vituko vingi kuliko siasa.

Nawatakia nyote Heri ya Mwaka Mpya 2021!

Maendeleo hayana vyama!
Hakika ile COVID 19 waliyokuwa wanaikimbia bungeni sasa yenyewe ndio imerudi bungeni

Malipo ni hapahapa duniani
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,093
2,000
Tutaukumbuka pia kwa uchafuzi badala ya uchaguzi!Tutakumbuka pia mauaji ya wazanzibar wakati wa uchafuzi!

Mpaka dakika za mwisho za uhai wa Mkapa alikuwa anakumbuka tukio la mauaji Zanzibar!Ilimtesa mpaka kuandika kitabu kutubu ndio akafa kwa amani!

Damu ya mtu haisahauliki,huu upuuzi mwingine unasahaulika!
 
Iboya2021

Member
Dec 1, 2020
97
150
Kituko cha karne ni Tanzania kuimaliza Corona kwa maombi ya siku 3, huku tukishindwa kuomba kuumaliza ukimwi na Marelia.

Tunaomba 2021 Hollywood wafunguwe branch Tanzania kuna talent za hali ya juu, mtu anaigiza mkavu kabisa wala hacheki.
Muogope mungu wako na umuheshimu na utubu kabla mwaka haujaisha mana huoni wala husikii yanayotokea nchi za wenzetu kuwa na imani hata kidogo tu mrudie muumba wako maana umekengeuka na hau appreciate utukufu na miujiza aliyolifanyia taifa
 
Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
1,627
2,000
Pia tutakumbuka kwa Mmililiki wa Timu fulani kutafuta waamuzi na uwanja wa kuchezesha mechi ambayo timu yake na ikajipatia ushindi haramu wa magoli mengi yasiyokua na mvuto mwishowe hata timu yake ikashindwa kufurahia kutokana na ushindi haramu na usio na mvuto
 
nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,913
2,000
Kwaheri 2020 Karibu 2021.

Tutaikumbuka 2020 kwa ushindi wa kihistoria wa CCM ambao haujawahi kutokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa kufeli kihistoria kwa Chadema kwa kupata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uasisiwe.

Tutaikumbuka 2020 kwa tukio la Chadema kujiweka lock down na baadae wale waliotoka lockdown wakaitwa Covid 19 baada ya kukubali kurejea bungeni na kuapishwa na Spika Ndugai katika viwanja vya bunge.

2020 Chadema ilifanya vituko vingi kuliko siasa.

Nawatakia nyote Heri ya Mwaka Mpya 2021!

Maendeleo hayana vyama!
NI MWAKA WA KIHISTORIA KWA:
Wale waliokuwa wanaonekana si lolote si chochote kugeuka "lulu" kwa ndugai na wenzake(alikuwa akiwatimua Bungeni kwa chuki za wazi wazi).

Taasisi mbali mbali kuungana kuhujumu uchaguzi kwa masilahi ya "watawala".

Serikali kufanya ufisadi wa kimataifa (kutangaza hakuna corona) lakini wakavuta "mpunga" wa wahanga wake!
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
14,172
2,000
Nakumbuka kituko cha mponya corona na kiki za vitambuoosho vya wamachinga. Alilazimika kuvikana wakati wa kampeni kwamba "haikuwa lazima". Alipobanwa na mwanasheria nguli kwamba arudishe hela, akapinduka tena.

Mponya corona anayependwa na watanzania akapiga mahoti kubekbeleza kura
Nakumbuka kituko cha yule jamaa alieamua kurusha chopa toka KIA to dar bila kibali akisema haogopi chochote na anaetaka kufanya lolote afanye,
Lakini baada ya uchaguzi alipopigwa chini akakimbilia kwa Amsterdam eti anaogopa kitisho cha kwenye simu. Just imagine kitisho cha kwenye simu.
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,677
2,000
Aisee kwangu Mimi Drama ya mwaka ni ile move ya Lisu kukimbilia Ubalozi wa Ujerumani,

Jamaa wakati wa kampeni alikuwa anapiga mkwara wa hatari mpaka ikafikia hatua akafunga barabara,

Ila ghafla tu baada ya matokeo kutangazwa akatangaza kuwa ametishiwa, akakimbilia ubalozini,

Aisee nilichoka,

Wanasiasa si wa kuwaamini kabisa.

Mbowe nae akatuambia atakuwa Waziri Mkuu within 72 Hrs, akatuaga kabisa. Daah.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom