Mwaka 2017 nilimuokoa kaka yangu wa hiari aliyekuwa anasumbuliwa na ndoa yake

miles45

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
3,468
8,287
Kama kawaida katika harakati zangu za hapa na pale nikiwa kwenye fukwe nabalizi akatokea bro mmoja tusie fahamiana ila tulisalimiana na kila mtu akaendelea na mishe zake 2017 hiyo.

Baada Kama ya wiki mbili/tatu hivi tunakutana town Tena tukasalimiana na akaniuliza vipi umeenda Tena kule beach nikamjibu hapana ila natengeneza ratiba ya kwenda huko. Akaniomba namba na kuniambia nikiwa tayari nimjulishe twende wote nikamjibu poa.

Kiufupi huyu bro Alikuwa yupo kwenye misukosuko ya ndoa yake halafu ni wale watu wapole wasio na Mambo mengi ila mke wake ndio balaa.

Siku ya siku ikafika nikamjulisha kuwa Safari imeiva Basi akajianda tukaenda tukiwa njiani ndio akawa ananimegea mkasa mzima wa maisha yake ....kiufupi nilitangulia kumjua yeye kiundani kushinda yeye kunijua Mimi.

Huyu bro alioa mke mlokole kwelikweli lkn Cha kushangaza huyu mke alikua mjanja Sana alijificha kwenye mwamvuli wa wokovu ili makosa yake yasionekane yaani ni mwanamke Alie kuwa mshenzi Sana ila pamoja na ushenzi wake bro ndio alionekana hafai kwenye kila ugomvi unaotokea ndani ya nyumba yao ndio hivo mwanamke alionekana hana hatia.

Huyu bro alikua na familia ya watoto watatu mmoja wa ujanani Sana ni wa kiume alikua na miaka 17 wakati huo, walio fata ni miaka nane na mitatu.

Cha kushangaza huyu mke wake aliwalisha ujinga watoto wote akinza na huyo mkubwa wa kiume na kujaa chuki zidi ya baba yao na kuchukiwa vilivyo na watoto wake hasa huyo mkubwa wa kwanza.

Alinisimulia hayo akiwa na uchungu Sana ....na kiukweli huyu bro alionekana ni mtu Alie ipenda Sana familia yake sema mke wake ndio hivo.

Kisa kimoja aliniambia mkewe alikua anabeba pesa na kupeleka huko kwa mchungaji wake Kama sadaka wakati huo utakuta pesa za mtaji,ada au malengo yeye anapeleka kwa nabii huyu bro akijaribu kumuonya na kumuelewesha mke nae analianzisha eti anamzuia asiende kusali na kimjazia inzi akimtuhumu mwanaume wake anamkataza asiende kuabudu.....mke ni mama wa nyumbani katengeneza madeni kisa hilo kanisa lao ....bro anasema Alisha wahi beba hadi vitu vya ndani akapelaka huko kanisani ila ukimuambia na mwanamke nae anakuja juu eti anamzuia kuabudu.... Aisee iliniuma sana hii.

Kisa kingine ni bro aliinunulia hii familia vitu vizuri mfano raisi kuka (rice cooker) siku anaamka asubuhi anakuta wife kachukua ile sufulia ya ndani ya rice cooker ndio anapikia uji kwenye jiko la mkaa anasema bro alichukizwa na hicho kitendo na kumuambia mbona sufuria nyingine zipo kwa Nini uharibu hii ....? Wife akaja juu na kumuambia anamnyanyasa na vitu vyake na kuibuka ugomvi Tena kuwa Hadi wachungaji wakaja na ndugu wengine kusuruisha ......kifupi mabalaa ni mengi ...Hadi Alisha jaribu kumzaba makofi akaambulia kwenda selo na pesa kumtoka .

Akasema anafikilia kuitelekeza familia akaanzishe familia nyingine huko mbela ya Safari ...nikamjibu bro kuhamisha office ulio ijenga kwa miaka karibu na 30 kisa mwanamke itakugarimu Sana Cha kufanya itabidi upitie steji kuacha huku ukitoa chance ya mwanamke kujirekebisha ...ila kikubwa usimpe mimba kwa Sasa Kama unampango huo ili mtoto mdogo awe ni huyo wa miaka 3 ili isikuwie ngumu kwenye malezi. Basi baada ya kuongea hivo nikwa nimewin akili za bro na kuanza kuona anaweza kutumia akili zangu na zake zikae pembeni maana zimetumika na hazija fanya chochote zaidi ya mabalaa kuongezeka.

Basi nikamuambia kuanzia Sasa usiongeze chochote kile kwenye nyumba yako hata kijiko usinunue vilivyopo viache viendelee kutumika ila Ela ya chakula acha na usizidishe zaidi na wewe pale nyumbani pawe ni sehemu ya kwenda kulala tu ...jirudie muda unao taka na asubuhi uwahi kuondoka na usijishughulishe na chochote zaidi ya salimia watoto ambao hawajala sumu Sana za mama yao na waachie pesa ya matumizi then sepa na hiyo iwe ndio ratiba yako huku tukiendelea kusubiri steji zinazo fata. Akasema sawa ..nikimuambia hivi nikijua Kama mke wake atakua na akili atajiongeza na kuona kunamabadiliko Basi afanye chochote.

Baada Kama ya miezi mitatu mbele mwanamke akabeba vyote ndani na watoto wote mkubwa akampeleka kwa mjomba wake na Hawa wawili akaenda kuishi nao kwa Bibi yao bro mapema Sana akanicheki na kunieleza hali ilivyo nikamuambia huyo mwanamke amemisi kugombana na wewe hivyo anakutafutia upenyo Cha kufanya peleleza kimya kimya wako wapi Kama sehemu salama kaa kimya na uendeleze mishe zako Kama kawaida Wala usitake kusumbua watu ....nikamuuliza bro kwani wewe huoni aibu kila siku kuwekwa mtu Kati kwa mambo ya kipumbavu Kama haya ...? Kinyonge akasema ni kweli aibu daah kuoa huku ....? Nikamjibu usijari mambo yatakua sawa.

Ikumbukwe huko nyuma mtoto alifeli form four kwa kupata zero ..... Lkn alikataa kurudia mitihani Basi baba yake akafanya mbinu akamtafutia ukonda kwenye magari ya mikoani Cha ajabu mtoto akaenda rout Kama nne hivi na kuja kulalamika kwa mama yake kuwa kazi ni ngumu na kumjaza mama yake mambo ya uongo mama akaamini taarifa za mwanae na kulianzisha anataka kumuulia mwanae alikiwasha haswa Hadi vikao vikakaliwa na kusuruhishwa Kama kawa....hapa nikamuambia asijihusishe chochote na huyu kijana Hadi apo kijana mwenyewe atakapo jistukia na kutambua wewe ni Nani ...? Ukijipendekeza heshima yako itashuka.

Basi bana huku bro nikaanza kumzungusha sehemu mpya Kama vile mbuga tofauti tofauti na kumtengenezea hobby mpya ila hobby ya utalii ndio ilimuingia damuni ...maana tukanza kufanya Safari ndefu pale inapo jitikeza weekend ....yaani weekend tunaamua kwenda kutaliii mkoa Fulani na kurudi kwetu huku tukiendelea kula bebezi za mikoa mingine na kurudi hivo hivo ikafika sehemu kila weekend ya mwisho wa mwezi basi ni Safari....bro akanogewa Sana na hata kuvaa akabadilisha akaanza kuiga mavazi yangu kijana kutoka suruali za vitambaa 24/7 Hadi kuanza kupiga pensi na raba au vile visendo na tisheti yaani akaanza kuwa Kama black American flani hivi.

Basi wakati haya mambo yameiva yule mwanamke akaanza kulilia kurudi nyumbani bro akaniuliza nifanyaje nikamjibu muache ila mwendo ni ule ule nyumbani iwe ni sehemu ya kulala tu ....na vyakula vyake usile ....ila Ada za wale wawili zinalipwa Kama kawa na chakula anaacha vizuri tu...... Mwanamke hicho kitendo kikawa kinamuuma akaitisha kikao bila kumuambia mmewe wakati huo bro yeye ni kazi na Bata tu Hana habari na mtu siku jumamosi asubuhi tu anaambiwa Leo Kuna kikao wageni wanakuja nakuomba usiondoke .....jamaa hakua na noma akatii wito lkn alikua hata hajui ni kikao kinahusiana na nini ....

Basi by saa mbili watu wakaja kikao kinaanza kikamuhusu eti mwanamke analalamika jamaa hampi unyumba wake na anahisi mumewe anasaliti ndoa yake jamaa akabaki anacheka na kushangaa .... Jamaa akawaambia kwa heshima yenu naomba tu kikao kiahilishwe kifupi humu ndani Sina mke Nina mtu anaenitunzia wanangu. Mke wangu Alisha ondoka miezi mitatu iliyo pita ....kwa hiyo naombeni mniache niwahi kazini . Bro akaondoka na kunipigia simu Kama kawaida na kunipa michapo za chini chini kumbe mwanamke aliondoka kutokana na shinikizo la ndugu zake ili jamaa amalizie mahali kwao mambo magumu.

Basi bro anainjoy maisha yake na huku mkewe akiwepo na anamchukulia Kama beki tatu na mwanamke Alisha jaribu Hadi kujizulu ili kutafuta attention ya jamaa lkn ilishindikana .......bro alisema kwanza kimwanamke kibaya kimechoka kinatia Hadi kinyaaa na wanalala vyumba tofauti.

Ili tu kulea watoto kwa pamoja lkn kiukweli bro Ana bi mdogo muelewa Sana wanakuka nae maisha huku nyumba yake mpya ikiwa usawa wa Renta wanasubiri iishe akaanzishe kizazi kingine kile Cha kwanza kimemshinda , na yule dogo anabwia bangi tu kitaa na bro ata akimkuta hapa Wala Hana time nae , kidogo kale ka kike ka mwisho ndio wanaiva na bro kakisema kitu kanasikilizwa kwa usikivu makini Sana na hata mama yake akitaka kitu Basi anakatumia hako na lile kanisa la kudinyia na kusambalatishia ndoa za watu lilisha kufa.

NB: Mwanaume itambue thamani yako fanya kazi pata hela, achana na mafundisho ya kukuandaa kuwa mtumwa wa wanawake , ishi maisha yako aiseee hiii dunia itakua pepo kwako.....trust me utaenjoy Sana .........ila ukiwa mtumwa wa wanawake imekula kwako.
 
Kama kawaida katika harakati zangu za hapa na pale nikiwa kwenye fukwe nabalizi akatokea bro mmoja tusie fahamiana ila tulisalimiana na kila mtu akaendelea na mishe zake 2017 hiyo.

Baada Kama ya wiki mbili/tatu hivi tunakutana town Tena tukasalimiana na akaniuliza vipi umeenda Tena kule beach nikamjibu hapana ila natengeneza ratiba ya kwenda huko. Akaniomba namba na kuniambia nikiwa tayari nimjulishe twende wote nikamjibu poa.
Saaafi bro kwa kuokoa ndoa ya Bro wako
 
Kama kawaida katika harakati zangu za hapa na pale nikiwa kwenye fukwe nabalizi akatokea bro mmoja tusie fahamiana ila tulisalimiana na kila mtu akaendelea na mishe zake 2017 hiyo.

Baada Kama ya wiki mbili/tatu hivi tunakutana town Tena tukasalimiana na akaniuliza vipi umeenda Tena kule beach nikamjibu hapana ila natengeneza ratiba ya kwenda huko. Akaniomba namba na kuniambia nikiwa tayari nimjulishe twende wote nikamjibu poa.
Safi Sana blazaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom