Mwaka 2000 haukuwa "karne ya 21"! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwaka 2000 haukuwa "karne ya 21"!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Kjnne46, Jan 12, 2009.

 1. K

  Kjnne46 Member

  #1
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWAKA 2000 HAUKUWA “KARNE YA 21” !

  Neno KARNE maana yake ni miaka MIA MOJA (100). Kwa hiyo, ukianzia kuhesabu siku ya mwanzo wa kalenda (ya Magharibi) tarehe 01/01/01 Karne ya Kwanza itamalizikia tarehe 31/12/100, Karne ya pili tarehe 31/12/200 na hivyo hivyo hadi Karne ya kumi itaishia tarehe 31/12/1000. Sasa ukiendeleza mtindo huo huo utaona kuwa Karne ya kumi na tisa ilianza tarehe 01/01/1801 na kumalizikia tarehe 31/12/1900. Hali kadhalika, Karne ya ishirini ni kutoka tarehe 01/01/1901 hadi 31/12/2000, yaani MWISHO WA MWAKA 2000 NDIYO ILIISHIA KARNE YA ISHIRINI, NA TAREHE 01/01/2000 HAUKUWA MWANZO WA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA (21ST CENTURY) ambayo usahihi wake ni kuwa KARNE YA 21 ILIANZA TAREHE 01/JANUARI/2001!! Ili kufafanua zaidi hebu angalia:

  Karne ya Kwanza: 01/01/01 hadi 31/12/01 - miaka 100 (1st Century)
  Karne ya Pili: 01/01/02 hadi 31/12/02 - miaka 200 (2nd Century)
  Karne ya Tatu: 01/01/03 hadi 31/12/03 - miaka 300 (3rd Century)
  Karne ya Nne: 01/01/04 hadi 31/12/04 - miaka 400 (4th Century)

  na kuendelea hadi kufikia Karne ya 17 - miaka 1700 (17th Century)
  Karne ya 18: 01/01/1701 hadi 31/12/1800 - miaka 1800 (18th Century)
  Karne ya 19: 01/01/1801 hadi 31/12/1900 - miaka 1900 (19th Century)
  Karne ya 20: 01/01/1901 hadi 31/12/2000 - miaka 2000 (20th Century)
  Karne ya 21:
  01/01/2001 hadi 31/12/2100 -miaka 2100 (21st Century)

  Kulikoni mataifa ya Magharibi na Kisomo chao chote na utaalamu wa Hisabati wa kupindukia walionao wakahadaa Ulimwengu wote kuita Mwaka 2000 ni Karne ya ishirini na moja? Isitoshe, dunia mzima ikahangaika KUBADILI KWA GHARAMA KUUUBWA KOMPUTA ZAO ILI ZITANZUE NA PIA KUOANISHA “MABADILIKO KWENDA NAMBA MAPYA ZA 2..." WALIYOYAITA “Y2K”?? Kitu cha kushangaza ni kwamba hakuna nchi iliyoathirika kwa kutobadilisha komputa zao zote au kutofuata mapendkezo yote ya “millennium bug” (k.m. Italia na Korea ya Kusini), na hata watu binafsi wengi walishindwa kugharamia the migration to Y2K compliant systems/protocols lakini tarehe 01/01/2000 komputa zao zikafanya kazi kama kawaida. Au huu ulikuwa ni “mradi wa kibiashara” kuuza teknologia yao pamoja na Computer softwares & accessories zao ?

  The Year 2000 problem (also known as the Y2K problem, the millennium bug, the Y2K bug, or simply Y2K) was a notable computer bug resulting from the practice in early computer program design of representing the year with two digits. This caused some date-related processing to operate incorrectly for dates and times on and after January 1, 2000 and on other critical dates which were billed "event horizons". This fear was fueled by the attendant press coverage and other media speculation, as well as corporate and government reports. People recognized that long-working systems could break down when the "...97, 98, 99..." ascending numbering assumption suddenly became invalid. Companies and organizations world-wide checked and upgraded their computer systems. While no significant computer failures occurred with global significance when the clocks rolled over into 2000, preparation for the Y2K bug had a significant effect on the computer industry. The fact that countries where very little was spent on tackling the Y2K bug (such as Italy and South Korea) fared just as well as those who spent much more (such as the United Kingdom and the United States) has generated debate on whether the absence of computer failures was the result of the preparation undertaken or whether the significance of the problem had been overstated.

  Source: WIKIPEDIA http://en.wikipedia.org/wiki/Y2K

  Mnasemaje wataalamu wa IT na wasomi kwa jumla??
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu usichanganye karne mpya (ya 21) na Y2K. Officially, ilikuwa inajulikana wazi kwamba karne mpya ya 21 na kwa upande mwingine milenia ya tatu itaanza tarehe 1 January, 2001. Hiyo hofu ya kuchanganyikiwa kwa programu za kompyuta ya Y2K ni swala jingine, na sidhani kuna mtaalamu yeyote aliyesimama kutetea uhusiano wa Y2K na karne ya 21. Kilichotokea kwa watu wengi wa kawaida (ambao hawakujihusisha kwa undani ktk mambo ya kalenda) ni kwamba walimezwa zaidi na hofu ya Y2K na na pengine hizo sifuri tatu za 2000 hawakuzizoea kuziona, basi wakawa na mawazo ya karne mpya. Lakini officialy, binafsi sikuwahi kusikia nchi au mtaalamu aliyedai kwamba karne ya 21 ingeanza January 1, 2000.

  Kwa nyongeza you may CLICK HERE
   
  Last edited: Jan 12, 2009
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....duuh :confused:
   
 4. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Kweli duniani kuna mambo
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  It is true.

  When the last century turned, the general populace went with 1899 --1900 as their official transition and the intellectual establishment went with 1900 --1901 as theirs. The establishment won. Almost every turn of the century party was held on december 31, 1900.

  As the next century transition loomed, the general populace was again backing the 99 --00 transition while the establishment was holding fast to the 00 --01 switch. Who actually won? The establishment didn't stand a chance. Why not?

  a. Important cultural events are no longer determined by the establishment. Pop culture reigns supreme.

  b. 2000 was such a nice, round, even number that people couldn't resist it.

  c. The whole Y2K computer issue lent more weight to 2000 being an important and noteworthy milestone.

  d. No one really listens to scientists.
   
  Last edited: Jan 13, 2009
 6. K

  Kjnne46 Member

  #6
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa maelezo mazuri kuhusu Y2K.

  Lakini mada yangu ya msingi kwenye kichwa cha habari bado hujanifafanulia. Watoto wangu wanakupa ushahidi kuhusu "utata" uliopo katika WIKIPEDIA ingawa nimesoma hiyo link yako ambayo sehemu ya Century-no./First Day/Last Day inalingana kabisa na nilivyoandika mimi. My Question is: WHEN DID THE “21st CENTURY” ACTUALLY BEGIN? Hebu soma vifungu hivi:

  a) Year 2000

  From Wikipedia, the free encyclopedia (http://en.wikipedia.org/wiki/2000)

  The year 2000 was the target of Y2K concerns, fearing computers could not shift from 2-digit "99" to "2000"; however, many companies had already converted their software, even obtaining Y2K certification, and relatively few problems occurred.

  Popular culture also holds the year 2000 as the first year of the 21st century and the third millennium. In the Gregorian Calendar, however, this distinction falls to the year 2001 because the first century began with year AD 1 (there was no year zero), and the thousand years spanned to years 1-1001.

  b) 21st Century

  From Wikipedia, the free encyclopedia (http://en.wikipedia.org/wiki/21st_century)

  The 21st century is the current century of the Christian Era or Common Era in accordance with the Gregorian calendar. It began on January 1, 2001 and will end December 31, 2100.

  c) And this contention by the Daily Mail:

  According to the Daily Mail for 1st January 2000 the 21st Century began on that day. ... Telegraph, The Independent, The Guardian and The Times for 1st January 2000. ...
  (www.stock.org.uk/charles_phillips/stock11200.htm)

  Naomba msaada wa ziada .....
   
 7. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180


  Kuhusu Y2K. lilikuwa ni tatizo. Kumbuka South Korea ilianza kupiga maendeleo katika miaka ya 70. Hivyo computer systems zao nyingi zilikuwa tayari Y2K Compliance.

  Pamoja na hayo computer systems zina layers kama tatu. Hardware layer, OS layer, application layer. Na kila layer inaweza kuwa na algorithm tofauti ya calculate calendar. Hivyo kushughulikia suala la Y2k lilikuwa ni kitu muhimu. Lakini nchi zingine kama Tanzania, juhudi zilikuwa over the board.
   
  Last edited: Jan 14, 2009
 8. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Mkuu mie sio mtaalam wa IT bali ni Mchungaji
  Karne ya Kwanza: 01/01/00 hadi 31/12/99 - miaka 100 (1st Century)
  Kulikuwepo na mwaka wa 'zero' ndio wakaweza kuhesabu moja.
  Ndio maana tunapata karne inaishia '99.
  Asante kwa changamoto.
   
 9. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Y2K haikuwa na effects kwenye personal computers, kwa vile computer hizo zimetengenezwa hapa juzi juzi tu. Tatizo kubwa lilikuwa kwenye main frame / Servers ambazo nyingi zinarun kwenye system za zamani sana, ndo sababu hata wataalam "programmers" waliokuwa wanatafutwa kukabiliana na janga hilo ni wale wanaojua kuprogram language za kitambo, mfano COBOL. Unajuaje kwamba wao wataliano na Wakorea Banks zao haziku-upgrade system zao??
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Umeshawahi kusikia mwaka 0 AD.
   
 11. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2009
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwaka 0 hauna AD au BC, ni mwaka 00 tu.
   
Loading...