Rais wa kenya Mwai Kibaki leo akiwahutubia wazee wa Dar kwa niaba ya Watanzania amesema ''Watanzania hamjazoea kutembea'' maana yake kuwa watanzania wengi wanaishi Tanzania tu Je hi si dharau kwa Watanzania? Inamaana Watanzania huushi pwani tu na hatutoki nje ya nchi hivyo akasisitiza tuende kenya.
Hata hivyo kitendo cha serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais JK Kikwete kuipa barabara ya Old Bagamoyo yenye historia ya Tanzania na kumpa Mwai kibaki, ikumbukwe Mwai kibaki aliingia kwa nguvu Kenya na kusababisha mauaji ambayo leo hii hatosaulika kenya. Sisi Watanzania ni kipi kilichotufanya barabara ya kihistoria kupewa Kibaki?
Source ITV habari saa 2000hrs usiku
Hakuna dharau yeyote mkuu! Ni ukweli usio pingika kuwa Watanzania tu waoga sana wa kuthubutu.
Takwimu ziko wazi, ni watanzania wangapi wanao thubutu kuulizia walau kibarua tu, pale Nairobi?
Oh nchi yangu Tanzania! watoto wako wamekuwa wa aina gani? hatumu APPRECIATE mtu yeyote? kwa nini lakini?
Mkuu wakenya hawa hawa enzi za mwalimu walikuwa wakituheshimu mno, na hata kuiga mambo yetu mengi...rejea TANU..KANU...
Nini kimefanya wageuke?
umeongea vizuri sana mkuu! hawa watu wanataka sisi watanzania tumchukie mwai kibaki bila sababu. hii kasumba ya kuwachukia wakenya ililetwa na mtu ambaye sasa yupo kaburini. hawa watu bado wantawaliwa na kaburi lake. tanzania ndio maana haina maendeleo kwa sababu kuna watu bado wanendeshwa hisia zao na kaburi la mtu badala a ya akiri zao.
Ujinga wetu mkuu
Kutembea ni msemo tu lakini ukilinganisha wakenya waliopo nchini kwetu kwa nafasi mbalimbali na watz waliopo Kenya unaweza kugundua kuwa wakenya wanachangamkia fursa kwa haraka zaidi. kwa hiyo Mzee Kibaki yuko sahihi na kwamba ametoa changamoto kwa wa tz kugundua fursa nje ya Tz na kuzichangamkia. Yote hayo pia yanahitaji ujuzi na maarifa.
mara ya mwisho kusafiri kutoka hapo unapoishi ni mwaka gani?