Mwai Kibaki awadharau watanzania!

Mwai Kibaki awadharau watanzania!

Alikuwa anamwambia vasco pipa hadi linatoboka lakini hakuna ulichojifunza kwani nchi yako haina la maana. Yeye na uzee wake ameleta maendeleo makubwa Nairobi. Jifunzeni kuelewa mambo mnapoambiwa kwa mafumbo.
 
Siku 1 nilikua nakwenda Rwanda, mpakani pale nikawa na kazoezi kakubadiri hizi pesa zetu za madafu kwenye kwenye currency yao, wale jamaa wa bolder walinambia, mkuu, hii pesa yenu ya Tanzania ukituachia hapa itakaa sana, nyie Watanzania hua hamsafiri! Nakubaliana na Mwai Kibaki kwamba Wabongo wengi hatusafiri though kutokusafiri haina maana kwamba hatuna akili ingawa pia kusafiri kunakupa Exposure ya kinachoendelea sehemu nyingine, inawezekana hatusafiri kwasababu linchi letu likubwa mno, so mtu akitoka Mbeya kwa mfano na akaeenda Mwanza, au Mwanza kwenda Mtwara, kwa baadhi ya nchi hiyo distance ni kama kutembea zaidi ya nchi 4!

Bado sijaelewa, kwanini Mwai Kibaki amepewa barabara? Au kwasababu barabara hiyo inaenda Bagamoyo kwa mkuu, mwenye uelewa wa hilo tafadhari!?
 
Rais wa kenya Mwai Kibaki leo akiwahutubia wazee wa Dar kwa niaba ya Watanzania amesema ''Watanzania hamjazoea kutembea'' maana yake kuwa watanzania wengi wanaishi Tanzania tu Je hi si dharau kwa Watanzania? Inamaana Watanzania huushi pwani tu na hatutoki nje ya nchi hivyo akasisitiza tuende kenya.

Hata hivyo kitendo cha serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais JK Kikwete kuipa barabara ya Old Bagamoyo yenye historia ya Tanzania na kumpa Mwai kibaki, ikumbukwe Mwai kibaki aliingia kwa nguvu Kenya na kusababisha mauaji ambayo leo hii hatosaulika kenya. Sisi Watanzania ni kipi kilichotufanya barabara ya kihistoria kupewa Kibaki?

Source ITV habari saa 2000hrs usiku
Mkuu naona unaugua ugonjwa ambao watanzania wengi wanaugua, Ugonjwa wenyewe ni Inferiority Complex, yaani hujiamini, mzee kibaki amesema watanzania watembee hata nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kueneza kiswahili.

Mimi nadhan tungetakiwa tumsifu kwa ujasiri wake wa kuamini kuwa sisi ndiyo tunaojua kiswahili vizuri na tunapaswa kuwafundisha wengine lakini ajabu ni kwamba umekuja kivingine kabsa kutokana na wewe kuwa mgonjwa wa Inferiority complex.

Nenda Rwanda au Burudi kama hujakuta waalimu wa kiswahili wengi tu kutoka kenya, sasa mzee akisema ukweli unawashwa na kuanza kupanik tafadhali jiamini ndugu
 
Rais wa kenya Mwai Kibaki leo akiwahutubia wazee wa Dar kwa niaba ya Watanzania amesema ''Watanzania hamjazoea kutembea'' maana yake kuwa watanzania wengi wanaishi Tanzania tu Je hi si dharau kwa Watanzania? Inamaana Watanzania huushi pwani tu na hatutoki nje ya nchi hivyo akasisitiza tuende kenya.

Hata hivyo kitendo cha serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais JK Kikwete kuipa barabara ya Old Bagamoyo yenye historia ya Tanzania na kumpa Mwai kibaki, ikumbukwe Mwai kibaki aliingia kwa nguvu Kenya na kusababisha mauaji ambayo leo hii hatosaulika kenya. Sisi Watanzania ni kipi kilichotufanya barabara ya kihistoria kupewa Kibaki?

Source ITV habari saa 2000hrs usiku

Mkuu hawa viongozi wetu ndivyo walivyo usishangae pia kule kenya nako kukawa na barabara au chuo kinachoitwa Kikwete. Hii ni sehemu ya zawadi yake kwa Mwai Kibaki. Sasa jiulize kama kibaki kapewa zawadi hiyo je mataifa makubwa yamepewa nini? kama si madini yetu na rasilimali zetu zingine kupitia mikataba mibovu. Tafakari? labda pia wangetueleza kenya imeifanyia nini Tanzania mpaka kufikia hatua hiyo waliofikia. May be wana sababu nzuri.
 
mtawasema sana wakenya!! lakini ukweli ni kwamba wametuacha kwa karne nzima! waacheni wapumuwe.......!
 
Rais wa kenya Mwai Kibaki leo akiwahutubia wazee wa Dar kwa niaba ya Watanzania amesema ''Watanzania hamjazoea kutembea'' maana yake kuwa watanzania wengi wanaishi Tanzania tu Je hi si dharau kwa Watanzania? Inamaana Watanzania huushi pwani tu na hatutoki nje ya nchi hivyo akasisitiza tuende kenya.

Hata hivyo kitendo cha serikali ya Tanzania ikiongozwa na Rais JK Kikwete kuipa barabara ya Old Bagamoyo yenye historia ya Tanzania na kumpa Mwai kibaki, ikumbukwe Mwai kibaki aliingia kwa nguvu Kenya na kusababisha mauaji ambayo leo hii hatosaulika kenya. Sisi Watanzania ni kipi kilichotufanya barabara ya kihistoria kupewa Kibaki?

Source ITV habari saa 2000hrs usiku
I was flabagasted,to say the leat...Kibaki ametufanyia nini hata tumpe heshima hii kubwa?????

Kwakweli nimetafakari sana juu ya hili sikuona mantiki yeyote..
ni kipi cha kumkumbuka kwacho?
Eti amesomesha wengi alipokuwa makerere..what????
this to me sounds like private friendship between the hons,it has nothing to do with the Tanzanians.
 
That was the management decision,has nothing to do with your views.
Mind your business.
 
I was flabagasted,to say the leat...Kibaki ametufanyia nini hata tumpe heshima hii kubwa?????

Kwakweli nimetafakari sana juu ya hili sikuona mantiki yeyote..
ni kipi cha kumkumbuka kwacho?
Eti amesomesha wengi alipokuwa makerere..what????
this to me sounds like private friendship between the hons,it has nothing to do with the Tanzanians.

Oh nchi yangu Tanzania! watoto wako wamekuwa wa aina gani? hatumu APPRECIATE mtu yeyote? kwa nini lakini?
 
Wabongo bana, Anayekwambia ukweli kakudharau.....aya bana..

Hebu nenda umwambie msanii wa bongo muvi usoni MUVI ZENU MBOVU uuone moto wake..utakula matusi mpaka ukome ukome....
 
Yaani Zipuwawa ungekuwa karibu yangu ningekupa helikopta mm binafsi jana nilipoangalia ile taarifa ya habari ITV nilifedheshwa na kuhuzunishwa sana na pia nilijisikia kulia kwanini huyu mtu anatudharau kiasi hicho yani sie Watanzania hatuwezi kutoka hata nje ya mipaka yetu tunabaiki hapa tz, isitoshe kwaniini serikali yetu ya Tz hasa viongozi wetu wamembatizia barabara ya OLd Bagamoyo yuule aliyeleta vita na damu kumwagika nchini kenya na wala wananchi wa kenya hawakumchagua yeye ndiye awe ukumbusho wa barabara zetu hapa tz, kwani hapa kwetu hakuna watu wa kuasisiwa mf:Benjamin Mkapa, Mama Tibaijuka,Sinde Warioba, Freeman Mboye n.k kwani hao hawawezi kuwa ukumbusho wa barabara zetu au vitu vyetu mpaka mtu wa nje, nimejisikia vibaya sana kwa ile DHARAU ALIYOIFANYA MHE. MWAI KIBAKI JANA, na kama viongozi wanapitia thread hii waone hii comment niliyotoa hapa nimejisikia vibaya sana tena sana, lakini nawaombea Mungu awatokee viongoizi wetu wawe wanaona kwa macho ya mbeleni haaa!
 
Last edited by a moderator:
kwa nini hawakumpa barabara ya Arusha-Namanga?

wee thubutu ile ni Nchi ya Kaskazin bana... nyie kaeni na mzaramo wenu ... kule tunauliza ushatupa shilingi ngapi mkapa tukupe barabara chaliii.. nyingi tumewapa mangi wetu hata Rais kama ni dhaifu hatumpi
 
Hivi kwa nini sisi watanzania tukielezwa ukweli tunakasirika na kusema ni zarau,hiyo siyo zarau ila ni kweli kabisa hatutembei

Siamini kama Kibaki anamzidi Kikwete kwa kutembea?? Hii statement itamfanya Kikwete aongeze safari zake za nje. Kusafiri kote huko bado Kenya hawajaona??
 
Mzee kibaki ameongea kwa data idadi ya watanzania wanaotembelea dunia ni wachache mno hata Rwanda yenye population ya 9m wanatembea mno. kuna wakati kukubali ukweli ni muhimu hata kama hupendi kuusikia. Wabongo tufunguke tutembee
 
Hii sio ya kushangaza sana kwa tz.KIBAKI baada ya kugeuza matokeo ya uchaguzi uchaguzi wa kenya mwaka 2008,kulitokea mauaji ya watu zaidi ya 1500.kitendo cha viongozi wa tz kumpa tuzo ya heshima ya barabara ya old Bagamoyo mu..u.a.ji huyo wa kenya ni ishara ya viongozi wa tz kukubaliana na aina hii ya uongo usiozingatia demokrasia.Na ndo maana tunao mauaji mbalimbali yaliyofanywa na police nchini mwetu,hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya wauaji hao.SO SAD.
 
Haha, kuna Barabara pale Nairobi wanataka kuipa jina la JMK but yenyewe ni vumbi road so wanajaribu kufikiria itakuwaje, so just bos anataka naye jina lake liwe katika majiji kama vile akina Nkrumah Road, Lumumba, Mandela, Tom Mboya, Nyerere, chezea sifa ww!!
 
Mtoa mada mwendawazimu upeo wake mdogo wa kupokea hapari,sasa Kibaki kakosea nini hapo,sisi ni waoga hatuna hata confidence ya kutafuta kibarua Nairobi,badilisha title kwa kwa kusema Kibaki amaanisha nini kusema vile.
 
jana kibaki kapiga kiswahili mwanzo mwisho.....Membe baada na yeye kupiga kiswahili akaanza kupiga kidhungu ......
 
Back
Top Bottom