Mwafrika avumbua Mto nchini Marekani

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,120
7,874
Kweli Afrika tumeanza kujitambua sasa. Kuna mwafika mmoja anayeenda kwa jina la Alli Madi (pichani hapo chini) yuko kwenye mission ya kuzunguka dunia na kuvumbua vitu mbalimbali na kusambaza ustaarabu wa Mwafrika.

Moja ya mafanikio yake makubwa ya hivi karibuni ni kuvumbua mto mmoja mkubwa mjini New York ambao ameupatia jina la River KITGUM. Hii ni baada ya hivi karibuni kuvumbua mto mwingine alioupatia jina la River GULU.

Alli madi.jpg


Baada ya kutoa taarifa hiyo huko twitani, watu wengi wameonekana kumpongeza. Mmoja wa wachangiaji alimuomba katika moja ya uvumbuzi wake wa siku zijazo atumie jina la Babu wa Babu yake anayeenda kwa jina la NyawiyeOmino.

Mchangiaji mwingine (picha hapo chini) aliendelea kumpa moyo akimwambia aendelee kusonga mbele ila awe makini na wenyeji wa maeneo hayo ya New York kwa kuwa bado hawajastaarabika.

IMG_20190923_074247.jpg


Unaweza kumfollow huyu mvumbuzi huko twitani kwa jina la @allimadi.

Naona Waafrika tumeanza kujitambua.
 
Avumbue kabisa maana, maana watu wa huko bara la giza hawajitambui.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom