Mvutano uenyekiti wafukuta chadema

Status
Not open for further replies.

Alianzia HUKU

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/16464-mbowe-jiuzuru-ukinusuru-chama.html

Na bado hatakata tamaa
 
Hellow wana JF,

hoja iliyoko mbele yetu ni hoja mfuu, maana tunaacha kujadili yaliyo ya msingi katika mustabali wa hii nchi, maana migomo kila kona kila kukicha isiyo na kificho, mwanzisha mada ningelimshauri ataanzishe na maana yenye kututahadharisha kuhusiana na utawala wa sasa na mustakabali mzima wa nchi yetu badala ya kukaaa na uanzishwaji wa maada za kimbeya maana wachangiaji wengi wamekuwa wakiomba sorce ya taarifa hizi wapi sijaona amejibu wapi.

Naomba kutoa hoja.
 
Waberoya,
Thanks a lot. Contact number of Chadema Leadership you requested are as follows: Hon. Freeman Mbowe, Tel +255 784 779944; Dr. Slaa Tel +255 784 666 995 or +255 754 366995. We appreciate the interest. Keep up and our doors are always open to both to yourself as well as all those interested to work with Chadema. Cordial welcome. Dr. Slaa
 
or +255 754 366995. welcome. Dr. Slaa

Dr. Slaa;

Shehima kwako mkubwa wangu, pole na shughuli na tija yake imeonekana. Sasa mwangi wake mtauona muda si mrefu. Tumechoka.

Nilkuwa naomba Mhe hio mobile number ya Vodacom uifikirie upya mana unaendeleza ufisadi wakati wewe ni field marshall kuipinga. Field Marshall wa Ufisadi Rostam huko huko vodacom ana share mingi tu mhe. Kwani huwezi kuwa na Zantel or TTCL Mobile?

Je, mhe ukitupa na email yako itakuwaje?

Asante
 
Fikra Mbadala,
Nadhani kilichotokea Tarime ni majibu ya uhakika kuliko maneno yeyote yanayoweza kutolewa na mtu yeyote kuwa Chadema hakuna mvutano wa Makambi, yote yaliyosemwa yamepandikizwa na watu wanye kujua malengo yao na hatuna sababu ya kuwajibu.
Isitoshe, ushuhuda wa kuwa Chadema ni mmoja ni Team spirit iliyoko ndani ya Chadema, isipokuwa wale ambao sasa tuna uhakika wako kwenye pay roll ya CCM kama inaavyothibitishwa na documentary evidence ambayo ipo mikononi mwetu, na hatuna sababu ya kumumunya maneno kuyasema haya. Isitoshe wako wanaondeleza hoja ya Wangwe, lakini wangelifanya utafiti japo kidogo wangegundua kuwa swala la Wangwe kusimamishwa Umakamu Mwenyekiti kwa watu wa Tarime was not an issue and is not an issue, kwa vile Tanzania ilipofika inahitaji Chama chenye uwezo wa kuthubutu kuchukua hatua. Chadema inachukua hatua na itaendelea kuchukua hatua kila inapohitajika, provided ni kwa mujibu wa Katiba, Kanuni, Maadili na Taratibu za Chadema. Uongozi unaoogopa kuchukua hatua haujui maana ya Leadership, and Chadema wants to distinguish itself from these. Ni wazi katika kuchukua hatua wako watakaochukia, watakaoathirika, watakaolalamika na hii si kutengeneza makundi. Ndio uongozi. Ndio maana Chadema haikusumbuliwa na yote yaliyoandikwa kipindi chote na wala hayakutufanya kushindwa kufanya kazi zetu.
 


Dr.Slaa hivi msomi kama wewe bado unashindwa kutenganisha matumizi ya 'yeyote' na 'yoyote'?
Dr.yeyote huwa inaambatana na watu na yoyote ni kwa vitu.Nimeona kwa mara nyingine unafanya makosa haya.
BTW,ni swali dogo tu kama utaweza kujibu;Hivi udaktari wako ni nini?Binadamu,wanyama,falsafa au wa heshima?Manake sijapata kuona sehemu walipotaja chuo ulichopatia shahada ya udaktari.
Shukrani dokta.
 
Gogomoka,
Thanks and most welcome to JF. Nadhani tuna matatizo kadhaa. Tunaweka picha kuwa sisi tulioko humu ndio kipimo sahihi cha matakwa ya Watanzania zaidi ya 40 Million. Kwa maoni yangu baada ya kuzunguka Tanzania nzima, Wilaya zote isipokuwa za Mkoa wa Kagera, hali halisi si hii inayoelekea kupigiwa debe na wachache hawa wanaoandika humu JF. Ni hatari sana kufanya generalization ya aina hii.
Watanzania niliowaona kwenye mikutano ya hadhara na kwenye makundi na mikutano ya ndani wanakuwa "electrified" kila wanapokutana na Mbowe. Ushahidi documented upo wazi, Mbowe has been and still is a crowd puller todate. Kwa tafsiri ya kawaida, kabla mtu hajafanya conclusions, crowds hizo maana yake nini. Swali hili linahitaji kujibiwa kabla ya generalizations kama hizi, ambazo kwa kigezo chochote kile ziko biased and for obvious reasons. Ni kwa sababu hiyo nimeamua kuweka kumbukumbu sahihi kama Kiongozi wa Chadema mwenye kujua facts on the ground.

Pamoja na yote hayo, muhimu sana ni kuwa ugombea Urais, kwa msingi wowote ule, hauendi kwa ushabiki, mapenzi ya mtu binafsi bila Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria husika za nchi, Katiba na Taratibu ndani ya Chama husika. Hivyo, suala la Mbowe kugombea au kutogombea ni suala la Katiba ya Chadema, Taratibu za Ndani ya Chadema. Ikumbukwe kuwa Mbowe, au mtu yeyote ndani ya Chadema si mwamuzi peke yake bali ni vikao halali ndivyo vyenye kumteua Mgombea wa nafasi yeyote Udiwani, Ubunge na Urais. Dhana ya inayojengwa hapa ni ya udikteta wa Mbowe ambaye anajengwa kuwa "hakubaliki" lakini anajilazimisha. Nadhani dhana hii si sahihi na ikiachiwa itawapotosha watanzania bila sababu yeyote ya Msingi.
 
Dr Slaa,

Kwanza nitoe pongezi za dhati kwa kazi nzuri mlioifanya kufanikisha ushindi wa jimbo la Tarime.

Pili, sasa hivi kuna mbimu mbalimbali zimetumiwa ili kuhakikisha CHADEMA inayumbishwa,suala mojawapo ni hili la kuendelea kukichafua chama ambalo linafanywa hata na wanasiasa ambao jamii haijaweza kuwatambua kwamba wako katika siasa kwa malengo gani hasa.Linapofanywa au kusemwa jambo na mtu ambae jamii inamtambua kama mwanaharakati wa haki,huwa ni lazima jamii itamuamini hata kama ni uongo.Na uongo huu huu ukiachwa,basi utaaminika kwamba ni ukweli.Sasa tuchukulie mfano maneno anayoeneza Mch. Mtikila kwamba CHADEMA imehusika na kucheza rafu katika kifo cha mhe.Wangwe na bado ana mpango wa kusambaza nyaraka milioni moja nchi nzima,

Je,CHADEMA kukabiliana na hili Tatizo au kwa kuanzia CHADEMA kama taasisi imechukua hatua gani mpaka sasa?


Tatu, Tuongelee utaratibu uliotumika kwenye kampeni bila shaka kila mtu atakubaliana nami nikisema ulikua mzuri na makini.Je,bajeti ya uchaguzi ilikua kiasi gani au ni lini itawekwa hadharani?

Nne, Bila shaka CHADEMA imejenga imani kubwa kwa watanzania lakini kinachowanchanganya wananchi zaidi ni kwamba uchaguzi mkuu unakaribia na hakuna dalili za kuanzisha rasmi muungano wa vile vyama vyenye nia ya kweli katika upinzani.Naamanisha kama CUF kwani angalao ndiyo walioonekana kwamba ni bold katika politics zenye mafanikio ya kweli na sina uhakika sana na TLP.Je CHADEMA ukizingatia pia tarehe ya uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti ni hadi March next year tutakua tumejiandaa vya kutosha ku-balance na vyama au chama tutakachokua tunaungana nacho? pia kumbuka bado kuna chaguzi za mitaa.

Pia kuna jambo moja ambalo ni la muhimu sana,tunajua taifa liko katika wakati mgumu ,Maandamano,migomo,kurushiana mawe nk. yaani ilimradi tumekua kama vile tuko ukanda wa Gaza,sasa kuna hili suala la waalimu kunyanyaswa na mishahara yao.Ningeshauri katika zile halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA hususani Tarime,chama kiangalie kama kitaweza kufanya fund raising kuhakikisha angalao waalimu wanaongezewa asilimia kadhaa ili kurahisi au ku-buy more political credits.Najua CHADEMA kama taasisi kina limited resources but kina uwezo wa kufanya angalao jambo kama hilo na kuwaambia jamani ee sisi uwezo wetu ndiyo huo.Hapo tutakua tumepiga hatua moja mbele.

Kila la heri
 


yaleyale
kaazi kwelikweli!!
 

Mku Kakulwa,

Nadhani tunafanya jambo muhimu sana hapa,utani na masikhara mengine inabidi uweke pembeni mkuu.

Hapa tunajadili mustakabali wa chama na Taifa kwa ujumla.sasa ni bora uchungulie kwenye tovuti ya Bunge uangalie CV ya Dr.Slaa.

Tafadhali usipotoshe huu mjadala,haya mambo ndiyo yaliyotufikisha huku mkuu.
 
Kakulwa,
Asante kwa kukosoa kiswahili. Nadhani sijawahi kujitangaza kama Bingwa wa Kiswahili, au "Msomi wa kiswahili" kama unavyotaka kuonyesha. Hata hivyo, kama wewe ni mwelewa, language is only a medium of communication, japo ni vema ikatumika vizuri na sanifu, nadhani ulinielewa ndiyo maana hukuzungumzia "content" ya hoja bali umeishia kwenye cosmetics. I appreciate though.
 

na swali kuhusu udaktari wako je?
 

Sawa Mkuu,lakini mimi sioni utani wowote hapo.Nimeuliza nikitaka majibu manake kuna wanasiasa wengi sasa na hata viongozi wa serikali wanajiita madaktari,lakini ukitafuta chanzo cha udaktari huo hukipati.
sasa watuambie basi wamesoma wapi au ndiyo mambo ya kina Professor maji marefu?
 

Mkuu,

Trust me buddy,Nchimbi na Makamba wakija CHADEMA watakimbia! Manake CHADEMA kuna demokrasi,na watu wanajenga hoja.Hao woote wana hulka za kidikteta,I dont think if they are going to fit there.

Najua wakija CHADEMA itabidi wabakie kuwa Jobless manake CHADEMA sidhani kama kuna mtu atakaevumilia udikteta wa hawa watu.Ni bora wabaki huko huko kwenye uvundo.

Nakubaliana na wewe kwamba CHADEMA ni Gari kubwa na linaaminiwa na kila mtu hata CCM kimoyomoyo wana-admit ila we sema hawataki aibu tu,but all in all 2010 ni Tsunami
 

Wewe junior member wewe matata kwelikweli. Maswali yako yanaonyesha zaidi kukurupuka kuliko kutumia kichwa.

Any way, mimi si msemaji wa Slaa, lakini nadhani udaktari wake ni mambo ya canon law. Kutoka chuo kikuu flani huko Roma/vatican.
 
Tarime kweli imewakuna na huu ni mwanzo tu..Sasa humu mtandaoni mtaleta porojo...Na mawe huko mtaani mtakwepa vipi?
Ni muda wa kukata issue mkuu acha woga..Kampeni bado...Ila Dk Slaa yuko kwenye hoja ya msingi hapa kuhusu makundi mnayodai yamo chadema.
Kuhusu udokta..Hilo either atakujibu ama kama uko very interested then nenda kwenye tovuti kama Ben alivyokushauri.
Kuhusu lugha tuzingatie content na Mh mwenyewe kesha apologize kwa hilo...So back to the issue...Hakuna makundi na kama yapo yatamalizwa na vikao halali vya chama chao mkuu.
Nilishasema huko nyuma kuwa ccm ilishakufa mwalimu alipokufa mkabisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…