Mvua Kubwa ya Upepo Mkali Balaa Dar!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,443
113,452
Wajameni
Eneo ninaloishi mimi hapa Dar, kuna mvua kubwa balaa iliyoambatana na upepo mkali wa hatari inayonyesha sasa, siwezi kutoka kwenda kazini na watoto nimewazuia wasiende shule!.

Vipi upande wa eneo lako mvua hii imefika au ni kwa baadhi ya maeneo tuu?!.
 
Hata huku kwetu maeneo ya Uwanja wa ndege inanyesha sana.Sijui kama nitakwenda kazini pia.Ina upepo mkali sana.
 
Niko Boko huku. Sijawahi kuona mvua kama hii. Hamna kwenda kazini, watoto hamna kwenda shule mpaka kieleweke.
 
Basi hii mvua ni Dar nzima kama tangu Ukonga mpaka Boko!, usikute ile ya Ukonga imefika Kisarawe na hii ya Boko imefika Bagamoyo!.

Saa hizi ni asubuhi ila nje giza utadhani ni usiku wa manane!.
 
Ni hatari kubwa mvua kubwa sana na upepo wa kutosha kuezua paa kabisa na giza kubwa!!!!leo kazini saa 4!!mwanzo wa masika mwaka huu!!!
 
Wajameni
Eneo ninaloishi mimi hapa Dar, kuna mvua kubwa balaa iliyoambatana na upepo mkali wa hatari inayonyesha sasa, siwezi kutoka kwenda kazini na watoto nimewazuia wasiende shule!.

Vipi upande wa eneo lako mvua hii imefika au ni kwa baadhi ya maeneo tuu?!.

Unasema kweli?! mbona hapa Vwawa ni vumbi kabisa hakuna mvua hata tone?!
 
....tetemeko zito pia limesikika mida ya Alfajiri...huku niliko mimi... Aisee ni gharikaaa....
 
Back
Top Bottom