Andfaru
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 221
- 148
Habari zenu wakuu,
Tangu asubuhi mvua kubwa inaendelea kunyesha sehemu mbalimbali za Dar es Salaam.
Mvua kubwa hii imesababisha usumbufu, baadhi ya barabara hazipitiki kwa watembea kwa miguu na wenye magari.
Eneo la Mnazi mmoja kwenye barabara ya Bibi Titi, magari yamepaki sababu barabara hazipitiki baada ya maji kutuama barabarani.
Pia kufuatia hali hiyo maeneo ya Kariakoo baadhi ya biashara za watandika bidhaa pembezoni mwa barabara wamefunga biashara zao kufuatia mvua hii inayoendelea kunyesha.
Hata hivyo tulishaambiwa=>TAHADHARI: Mamlaka ya Hali ya Hewa yataadharisha uwepo wa mvua hatarishi
Naomba tuendelee kupeana updates ya madhara ya mvua hii, kama tujuavyo ni kawaida ya mvua ikianza kunyesha Dar es Salaam huambatana na kadhia mbalimbali.
Karibuni.