Athari za Mvua March 2024: Hali ikoje eneo ulipo?

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,485
5,818
Tangu asubuhi kumekuwa na mvua kubwa ikinyesha jijini Dar es Salaam. Huu uzi ni kujulishana athari na matokeo ya mvua hizo.

Je, ni barabara gani hazipitiki, tupite wapi? Wapi kuna mafuriko, na hatua gani tuchukue ili tuwe salama?

Tuhabarishane sisi kwa sisi.
 
1711183651116.png
 
Maji hayana pakwenda mvua Kali ikinyesha, unakuja kuandaa matukio makubwa kama nchi halafu mvua inapiga Kali imagine aibu itakayotokea hahh.
 
Maji ya mvua yanatakiwa kufwata mkondo wa bahari yaingie pale salendar bridge yazame ndani huko.
Sasa mifumo huku mitaani ni shida.
Ndio mimaji hiyo mitaani.
Na jiji hawazibui mifereji
Hapo ndo shida
 
Maji ya mvua yanatakiwa kufwata mkondo wa bahari yaingie pale salendar bridge yazame ndani huko.
Sasa mifumo huku mitaani ni shida.
Ndio mimaji hiyo mitaani.
Na jiji hawazibui mifereji
Hapo ndo shida
Pale salendar ndo mkondo wa mto msimbazi unapoingilia, jangwani kunafurika kutokana na level ya bahari kuwa karibia aawa kbs na mto msimazi hivo kufanya maji ya mto kuingia taratibu sana baharini.
Hii inaathiri maeneo mengi sana ya dar.

Ukiachana na watu kujenga vibaya lakini hizi ni athari zinatokana na kuongezeka kwa kina cha bahari.

Tusipochukua hatua itafika miaka baadhi ya maeneo yakawa hayakaliki tena kwa kujaa maji ya bahari.

Binafsi naona mradi wa mwendokasi pale jangwani pamoja na barabara ya fire magomeni zinaathiri mtiririko wa maji kwenda baharini.
 
Dar aslimia kubwa ni kama bonde maana iko chini
Siyo kweli, tatizo kubwa kabisa kwa Jiji la Dsm na Tz yote kwa ujumla ni kukosekana kwa Mipangomiji, there's the problem of Death of Town Planning profession in Tanzania and whole Africa in general, with exception of very few countries.
Endapo kama kungekuwa na Mipangomiji Imara na ya uhakika matatizo hayo ya mafuriko ya hovyo hovyo na matatizo mengineyo wala yasingekuwepo.
 
Back
Top Bottom