Mvua hizi ndipo ninapo mkumbuka mzee ruksa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvua hizi ndipo ninapo mkumbuka mzee ruksa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by masharubu, Dec 22, 2011.

 1. masharubu

  masharubu Senior Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nakumbuka vizuri kama sikosei ni mwishoni mwa miaka ya 1980 au mwanzoni mwa 1990 mvua kubwa ilinyesha nchini na hasa dsm ambapo rais wa wakati huo mzee mwinyi alitembelea sehemu zote za maafa hata kwa kutumia helcopter ambapo kwa bahati mbaya ilimkata kichwani mwandishi wake na kufariki, lakini toka jana cjaona viongozi wa kitaifa katika maafa hayo, leo hii mkuu wa mkoa anaomba life jackets kwa azam marine?wakati katika pantoni jipya zipo zimefungiwa na makufuli kwanini wasitoe zile?
   
 2. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kututembelea tu katutembelea, lakini hakuna chochote kilichobadilika, yani maji bado yanajaa tu mvua zikinyesha, ni show tu.
   
 3. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nataka nikusahihishe mafuriko hayo yalitokea mwaka 1989 na haikuwa Dar kama ulivyoeleza ilikuwa ni mikoa ya kusini. Mtwara na Lindi katika vijiji vya Mtama, Nyangao, Mahumbika, Kiwalala n.k Mhusika aliyekatwa na pangaboi alikuwa ni mpiga picha aliyejulikana kama Habib Halahala.
   
 4. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  hata hao pia wanakuja jamani, tusilalamike, wanakuja subirini
   
 5. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli viongozi wetu kwa sasa hawatuthamini tena,nilitegemea kwa kuwa serikali yote iko hapo mjini(Dar) suala hili lingepewa uangalizi wa karibu kabisa lakini aimekuwa kinyume.

  My take: Kama majanga ya namna hii yatatokea mikoa mingine kama ilivyotea kule mto wa mbu hali itakuwaje?
   
 6. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa hakuna viongozi kuna watawala na maagent wa mali za watanzania. Hakuna anayekujali wewe usiyekuwa na kitu ndg. Utakumbuka mengi lakini bila mkakati madhubuti wa kubadili uongozi wa juu tutabaki kupiga kelele tu kila siku.
   
Loading...