IRAN & NORTH KOREA: Ujasusi na mauaji nje ya ardhi zao

anarchist

Member
Apr 7, 2018
42
192
1. February 1984 Generali Gholam Ali ambaye alikuwa mkuu wa majeshi kwenye utawala wa Shah uliokuwa umepandikizwa na Marekani alijaribu kuiangusha serikali ya mapinduzi ya Iran akiwa mafichoni Ufaransa.Aliuliwa pamoja na kaka yake mjini Paris mahali ambako alikuwa mafichoni au ukimbizi wa kisiasa.Polisi walisema general Gholam alipigwa risasi na professional assasins.Dunia iliilaumu serikali ya mapinduzi ya Iran kwa kitendo hicho aidha general Ali alikuwa anatuhumiwa huko nyuma kuwa muuwaji asiyekuwa na huruma kipindi cha utawala wa Shah

2.Hamid Reza Pahlavi alikuwa mtoto wa 11 na wa mwisho wa Rais wa zamani wa Iran kabla ya mapinduzi ya mwaka 1979, Rais Shah..Hamid Reza alikuwa mwanasiasa wa upinzani aliyekuwa anaishi uhamishoni ufaransa na alikufa kifo cha kutatanisha huku mtu mmoja aitwaye Ali Amiztab afisa wa Iran akihusishwa na kifo cha bwana Hamid.

Bwana Ali Amiztab alijenga mahusiano na Hamid kwa muda mrefu huku bwana Hamid asijuwe kuwa alikuwa anajenga ukaribu na Nyoka.Afisa Hamid alikuwa kila mara akifanya contact na Hamid mpaka akapata kuaminiwa,bwana Amiztab alimweleza Hamid nia yake ya kuanzisha chama cha labour party nchini Iran chenye mlengo wa upinzani huku bwana Hamid kama mwanasiasa mpinzani akaingia mtegoni mwa Afisa Amiztab mwishoni bwana Amiztab akaomba akutane na Hamid Chitgar ana kwa ana na akapanga wakutane Vienna Austria.Bwana Hamid Reza Chitgar ambaye amekuwa akiishi kwa tahadhari kubwa kama mkimbizi wa kisiasa alitafuta marafiki wa kuongozana naye hadi Vienna ila alikosa na hakuwahi kutoka nje ya ufaransa tokea azamie ikabidi aende hivyo hivyo akimuamini mbwa mwitu aliyejivisha nguo ya kondoo.Tarehe 19 May 1987 Bwana Chitgar alisafiri kuelekea Vienna kukutana na bwana Amiztab.Tokea alivyoondoka siku ile mke wake hakupata habari yeyote jambo lililomstua na kwenda kuripoti kwenye vyombo va ulinzi vya Austria ndipo walipoanza kufuatilia lakini mnamo mwezi july miezi miwili baadaye mwili wa bwana Chitgar ulikutwa kwenye moja ya Apartment baada ya majirani kutoa taarifa polisi na mwili huo ulikuwa na majeraha ya risasi kichwani.Katika uchunguzi ulibainika nyumba ile ilipangishwa kwa mtu aliyekuwa na passport ya uturuki

3.Dr Abdulrahman Ghassemlou

Dr Ghassemlou alikuwa mwanasiasa na mwanaharakati wa wakurdi waliopo Iran na alikuwa mwiba mchungu kwa serikali ya Iran,utawala wa Iran ulikuwa unasema Ghassemlou alikuwa anatumiwa na watu wa nje na ni afisa wa nje .Mwaka 1988 serikali ya Iran iliamua kukutana na Dr Ghassemlou na walifanya kikao mara tatu ambayo yalifanyika kwa amani na walikutana tarehe 28-dec,30-dec na 20 jan mikutano yote yalifanyika Vienna Austria.Tarehe 13 July iliandaliwa kikao tena huku Tehran ikiwatuma maofisa wao Mohammed Jafar, Hadji Moustafawina Amir safari hii maafisa hawa walienda kwa mission nyingine na sio kufanya negotiation kama huko nyuma.Wakiwa kwenye chumba cha mkutano afisa Mohammed Jafar alikuwa anatoka nje sasa pindi alivyokuwa anafungua mlango kumbe ndio alikuwa anawafungulia wauaji ambao walikuwa Taghepur na asgar ambao baada yw kuingia waliwafyatulia risasi Dr Ghassemlou na wasaidizi wake na kisha wakatoweka.Mohamnad Jafar na Mustafa walifanikiwa kurudi Tehran huku Amir alikimbilia ubalozini kupata hifadhi.

4.Karim Zadeh alizaliwa Iran na alikuwa mkurdi lakini mwaka 1988 alikimbilia uhamishoni Sweden kama mkimbizi wa kisiasa na alipokelewa vizuri.Bwana Karim kupata kwake hifadhi Sweden haikumfanya asiweze kukumbana na makucha ya maofisa wa Iran.Ilikuwa tarehe 1 April dunia ikisherekea sikukuu ya wajinga ndipo maofisa wa Iran waliweza kupenya kwenye nyumba aliyokuwa anaishi msumbufu huyu wa utawala wa Iran bwana Karim na kummaliza.Ofisa aliyemuua bwana Karim alijulikana kama Reza Taslimi baada ya dereva taksi kutoa ushahidi kuwa alimsafirisha mtu huyo kutoka eneo la Nynashamn mpaka Stockholm .Cha kushangaza polisi wa nchini sweden SAPO walifanya uzembe na bwana Taslimi aliweza kukimbilia kwao Iran na polisi wa sweden walipokea lawama kedekede

5.Kazem Rajavi alikuwa balozi wa Iran wa kipindi cha uongozi wa Shah kwenye baraza la UN.Balozi Rajavi alikimbilia uhamishoni Switzerland mara baada ya mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979.

Ilikuwa 24 April 1990 ndipo alipokumbana ba maofisa wa idara ya ujasusi na usalama wa Iran ambao walimsimamisha barabarani mchana kweupe kisha kummiminia risasi. Baada ya uchunguzi wa kina mahakama ya uswizi iliikuta na hatia serikali ya Iran juu ya mauaji hayo huku maofisa 30 wa Iran ilibainika waliingia na passport feki.Mahakama ya Uswizi ikatoa warrant ya kumkamata mkuu wa Idara ya ujasusi wa Iran bwana Ali Fallshin na wana diplomasia 13 ambao walitakiwa kupewa mashitaka juu ya mauaji ya Kazem Rajavi lakini hakuna aliyekamatwa wala kushitakiwa..Mwaka 1996 Mjane wa Rajavi bibiye Zahra Rajavi aliuliwa na hitmen alipokuwa safarini kuelekea uturuki.

6.Efat Ghazi alikuwa mkimbizi wa kikurdi aliyekimbilia uhamishoni Sweden yeye pamoja na mumewe walikuwa wanaharakati wakudai uhuru wa wakurdi hivyo walikuwa wasumbufu sana kwa utawala wa Iran kumbe walichosahau ni kuwa idara ya ujasusi ya Iran ipo macho masaa 24 na huwa hawashindwi kukutimbia hata ukiwa nchi ya wapi.Ndipo maofisa walitumwa kwenda kummaliza binti yule ilikuwa 6 september 1990 mida ya saa sita na dakika 45 mchana bibiye Ghazi alipokea barua asijue ya kuwa hio barua ilikuwa ni bomu ile anaifungua tu akalipuliwa na bomu na kujeruhiwa sana aliwahishwa hospitalini lakini alifariki baada ya masaa 3 na ikagundulika mumewe pia alipelekewa barua hio ya bomu lakini polisi waliweza ku intercept.Polisi walifunga kesi kwa kusema walikosa ushahidi lakini serikali ya Iran ilituhumiwa na kulaumiwa sana

7.Mara baada ya mapinduzi ya mwaka 1979 Mahakama chini ya Ayatollah ilitangaza mbele ya waandishi wa habari hukumu ya kifo imetolewa kwa familia ya Pahlavi na maofisa wa serikali ya Shah Pahlavi akiwepo aliyekuwa waziri mkuu Bakhtiar.July 1979 Bakhtiar alifanikiwa kutoroka na kukimbilia Paris huko alipata ukimbizi wa kisiasa.Akiwa Paris bwana Bakhtiar akawa anaongoza harakati na upinzani dhidi ya serikali ya mapinduzi ya Iran ni wazi waziri huyu wa zamani alikuwa anawashwa washwa badala ya kutulia zake akawa anaiandama serikali ya mapinduzi ya Iran.July 1980 Bakhtiar alinusurika kifo baada ya watu 3 kuvamia nyumbani kwake kwa nia ya kutekeleza mauaji lkn alinusurika japo polisi na jirani waliuliwa timu ile ya wauaji 5 walikamatwa na kuhukumiwa kifo lkn baadae walirudishwa Tehran..Hii yote ilikuwa alert kwa Bakhtiar kuwa idara ya ujasusi ya Iran ipo macho masaa 24 kumuwinda

Tarehe 6 August 1991 Bakhtiar aliuliwa pamoja na sekratary wake kwa kuchomwa visu na maofisa 3 wa Iran mjini Paris.Miili yao ilipatikana masaa 36 baadae licha ya nyumba ya Bakhtiar kulindwa kwa ulinzi mkali na Mapolisi.Maofisa wawili walifanikiwa kukimbia na kurudi Tehran ila watatu Ali Rad alikamatwa uswizi na kurudishwa Ufaransa ambapo alihukumiwa kifungo cha maisha jela na mwaka 2010 Rad alipewa parole na kurudishwa Iran akiwa ametumikia jela miaka 18.Alipokelewa kama shujaa na maofisa wa Iran.Rad aliachiwa kwa mabadilishano ambapo Iran walimuachia mwanafunzi wa ufaransa aliyekamatwa kwa kosa la kuifanyia ujasusi Iran.


7.Fereydoun farrokzhad alikuwa muimba mashairi na mtayarishaji wa vipindi na mpinzani wa serikali ya mapinduzi ya Iran.Bwana Fereydoun alikimbilia Ujerumani na huko akawa anaandaa vipindi vya kuishambulia serikali ya Iran na Ayatollah na alikuwa anamdhihaki sana Khomeini kwa kejeli na kumuabisha kupitia radio show zake bwana Fereydoun alipokea vitisho vingi kutoka Tehran lakini alipuuzia na kuzidi kuongeza dozi kwenye vipindi vyake akisahau ya kuwa idara ya ujasusi ya Iran ipo macho masaa 24 hata ukiwa Bonn Ujerumani hawashindwi kutuma maofisa wao kuja kukushughulikia..Mnamo August 1992 mwili wa Fereydoun ulikutwa jikoni kwake eneo la Bonn ujerumani ukiwa na majeraha ya visu.Waliotoa taarifa hio polisi ni majirani zake baada ya kusikia mbwa wa Fereydoun akiwa ana bweka sana

8.Tarehe 17 September 1992 mwanasiasa Sharafkandi na wenzie watatu waliuliwa Kwennye mgahawa mjini Berlin Ujerumani.Watu waliovalia mask walijitokeza kwenye mgahawa na kumpiga risasi kiongozi huyo wa chama cha upinzani aliyekuwa anaishi uhamishoni Ujerumani na wenzie 3.Viongozi wa kikurdi waliokuwa wanaishi uhamishoni walilaani kitendo kile na kulaumu idara ya usalama ya Iran kwa vitendo viovu kisha polisi wa ujerumani walisema wanaamini Iran wanahusika na tukio lile licha ya ubalozi wa Iran nchini Ujerumani kukanusha vikali.Mahakama ya Ujerumani ilitoa warrant ya kukamatwa kwa Mkuu wa idara ya ujasusi wa Iran bwana Ali Fallahshin kwakuwa ndiye aliyetuma wauaji wafanikishe mauaji yale

9.Tarehe 6 July 1996 mkimbizi wa kisiasa mwenye asili ya kikurdi aliyekuwa anaishi Sweden bwana Hedayati aliuliwa na wanaodhaniwa kuwa maofisa wa Iran.Bwana Hedayati aliletewa barua iliyokuwa na bomu na alipoifungua alilipukiwa na bomu jambo lililosababisha apoteze mikono yake na macho na alifariki sababu ya vidonda hivyo miaka miaka minne mbele(Alilipukiwa na bomu 1990 akafa 1996).

10.Saeed Karimian alikuwa muanzilishi na ceo wa Chombo cha habari cha GEM TV iliyokuwa inapatikana Dubai na kurushwa kwa lugha 18.Bwana Karimian alikuwa raia wa uingereza na alihukumiwa jela miaka 6 na mahakama ya Tehran kwa kusambaza Propaganda dhidi ya Iran lakini alikuwa hayupo katika ardhi ya Iran.Saeed Karimiam huenda alisahau au hakujua umafia wa idara ya ujasusi ya Iran na mission walizozifanya kwenye ardhi za nchi za ulaya kwa wale walioonekana kama kirusi kwa serikali ya Iran..Tarehe 29 April 2017 Bwana Saeed Karimian akiwa na rafiki wake kutoka kuwait wa kibiashara walipigwa risasi Instambul Uturuki gari lililotumika kwenye mission ya kumuua Karimian lilikutwa limechomwa moto huku polisi wasijue cha kufanya.Serbia ilitangaza kuwa ilimkamata raia wa Iran aliyekuwa na passport feki akijaribu kutoroka na kumuhusisha na tukio la mauaji ya Saeed Karimia.



*MAUAJI YA NORTH KOREA NJE YA ARDHI YAO*


1.Timu ya makomandoo 31 wa North korea walitumwa south korea kwenye mission ya kuingia ikulu na kumuua rais Park Chung hee.Wakati wakiwa wamejificha milimani juu kabisa kwenye jiji la Seol wakagunduliwa na wananchi na wakazi wa maeneo ya pale makomando wakawakamata wale mashuhuda na badala ya kuwaua wakaanza kuwahubiria ukomunisti na kisha wakawaachia kwa kuwapa onyo wasimwambie yeyote yule.

Hio ilikuwa kosa kubwa wale watu wakaenda kuripoti polisi na jeshi likapewa taarifa lakini wale makomando waliweza kuepuka kugunduliwa wakavaa nguo za jeshi la South korea na kuelekea ikulu ya South korea walipofika mita 100 karibu na ikulu walizuiwa na kuhojiwa ndipo wakaanza kurushiana risasi na wale makomando hivyo ikabidi wakimbie na watoroke walifanikiwa kutoroka lakini inadhaniwa wachache waliuawa au walijiua walipojaribu kurudi North na mmoja alikamatwa..

Huku zaidi ya wasouth korea 90 wakipoteza maisha


2.Ulipuaji wa Bomu Burma 1983


Rais wa South korea alitembelea Burma kwa ziara ya kikazi mwaka 1983.Huku maofisa wasijuwe lolote kama North korea walituma majasusi wao Burma kwenda kutekeleza mauwaji ya rais wa South korea wa wakati huo.Majasusi hao watatu waliotumwa kutekeleza mission hio walitega bomu kwenye kwenye moja ya chumba lakini bomu hilo lililipuka dakika chache kabla Rais Chun Doo hwan kuwasili.Maofisa 17 wa south korea wakiwemo mawaziri 4 waliuliwa na shambulio hilo na wa Burma 4 walikufa.Gari la Rais Chun lilichelewa kuwasili sababu ya foleni na hio ikawa pona yake .

Maofisa 3 wa North korea walihusika na mission hio na inasemekana walilipua bomu hilo mapema sababu walisikia kingora hivyo wakadhani Rais Chun ndio anawasili.Baada ya shambulio hilo walikimbia lakini mmoja aliuliwa baadae na 2 kukamatwa.

3.Mauaji ya Choi Duk Keun

Kuna mamia ya wa North Korea wanafanya kazi ngumu Urusi sasa wapo wanaokimbia na kuomba ukimbizi sasa kuna afisa kutoka South Korea bwana Choi Duk Keun alikuwa anawashwa washwa akawa anawapa uangalizi na kuwasimamia wakimbizi hao kutoka North korea. Inasemekana bwana Choi Duk alichomwa sindano ya sumu nyumbani kwake alipokufia na palikutwa na matundu mawili ya sindano kwenye shingo yake.

4.Yi Hang Yong alikuwa na ukaribu na Kim Jong Un sababu mama yake Yong aliwalea kaka na dada zake Kim Jong un ambao ni Kim Jong Nam na dada yake.Yi Hang Yong alifanikiwa kwenda Urusi kusoma chuo lakini alivyomaliza elimu yake aliasi na kukimbilia korea kusini mnamo tarehe 15 February 1997 akiwa karibu na anapoishi katika eneo la Bundang watu wawili ambao wanadhaniwa kuwa makomando wa jeshi la North Korea walimpiga risasi bwana Yong na hatimaye Yi Hang Yong kufariki.wauaji wa Yi hawakukamatwa.

5.Kim Jong Nam ni kaka yake na Rais wa sasa wa taifa la North Korea Kim Jong Un.Mwaka 1998 Kim Jong Nam aliteuliwa kuwa kiongozi wa wizara ya ulinzi wa jamii kisha akapelekwa kuwa mkuu wa kitengo cha IT na 2001 Kim Jong Nam alimpeleka baba yake China kumkutanisha na maofisa wa China kuhusiana na soko la IT.Kim Jong Nam alikuwa anaandaliwa kuwa mkuu wa nchi lakini kwa uzembe alioufanya na kumdhalilisha baba yake akiwa Tokyo ndoto za Kim Jong Nam kupewa nchi zikayayuka.Mara baada ya mzee kufariki uongozi ukakabizshwa kwa Kim Jong Un na hapo ndipo kim Jong Nam alipoanza kuwashwa washwa akawa anashirikiana na nchi adui kama Japan na akawa anamsimanga Rais Kim Jong Un kuwa atashindwa uongozi na atafeli sababu ni mdogo ,hana uzoefu na ataidumbukiza nchi na huo utakuwa mwisho wa utawala wake.Kim Jong Nam akawa anaandika vitabu akishirikiana na waandishi wa habari wa Japan na mambo mengine kedekede akisahau Kim Jong Un ni simba hivyo kumchezea sharubu ni kama kujirahisishia kuonana na israeli mtoa roho.

Timu ya majasusi ikaandaliwa kwenda kummaliza Kim Jong Nam na safari hii walifunga safari hadi kuala lumpur Malaysia wakimwinda Kim Jong Nam aliyekuwa huko kula bata sasa siku Kim Jong Nam anajiandaa kuondoka Malaysia na kurudi zake Macau ndipo alipokutana na mbwa mwitu wenye njaa waliotumwa kuua.Kim alishambuliwa na wanawake 2 ambao walimkaba kwa nyuma na kumwekea kitambaa kilichokuwa na sumu iliyopigwa marufuku kutumiwa na makubaliano ya silaha za sumu ya mwaka 1993.Kim aliwahishwa hospitalini lakini alifariki.


Serikali za Nchi kama Iran,Korea Kaskazini na Urusi wamekuwa na matukio ya kuua wale wanaoonekana wapinzani wa utawala zao na wamekuwa wakiwawinda nje ya mipaka ya nchi zao hivyo kuhatarisha usalama wa watu waliokimbia makucha ya watawala wao.Wengi wameuliwa wakiwa uhamishoni huku wengine wakiwa na ulinzi imara.
 
Back
Top Bottom