Mvi ni dalili ya uzee au ni kitu gani.......................... .......? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mvi ni dalili ya uzee au ni kitu gani.......................... .......?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 12, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kama mvi ni kipimo cha busara.......... Kwa nini zifichwe?

  Kwa zamani ingekuwa ni muhali mkubwa mtu kuuliza swali la aina hii, kwa sababu mvi zinahesabiwa kama dalili ya busara, bila shaka zikihusianishwa na kuona mengi ambayo ni wenye umri mkubwa tu waliokuwa na nafasi hiyo. Lakini leo, mvi ni kisirani na karibu kila mtu anajaribu kuzikimbia, kwani kuendalea kuwa kijana ni sifa kubwa. Kwa sasa uzee unanuka na kila mmoja anajaribu kuukimbia kwa njia mbalimbali ikiwemo ya kukana umri na kujirudisha nyuma kimatendo. Kwa kifupi hii ndiyo historia ya mvi, usiziogope bure!

  Karibu rangi zote asilia za nywele zinatoka kwenye kitu kiitwacho melanin, ambacho huzalishwa na mwili kutokana na seli zinazofahamika kama melenocytes. Nywele zinapobadilika na kuwa nyeupe ina maana kwamba, melenocytes haizalishi tena melanin. Mabadiliko haya ya nywele kutoka rangi nyeusi na kukosa rangi (mvi) siyo hatua ya siku moja bali mwaka na miaka, kwani nywele moja hubadilika baada ya muda mrefu na nyingine na nyingine. Siyo hatua ya siku moja tu. Kwa kadiri mtu anavyozeeka ndivyo ambavyo uwezo wa mwili kuzalisha melanin unavyopungua.

  Uwezo huu huanza kupungua mtu anapofikia umri wa miaka 35 au 40. Lakini watu wengine huanza kuota mvi wakiwa na umri wa miaka hata 20 tu. Je, hii nayo inatokana na nini?
  Pengine ni jambo la ajabu kwamba kuvuta sigara kunatajwa kama sababu ya kuchochea mtu kupata mvi akiwa na umri mdogo. Ukiwachunguza wavuta sigara wazuri, utagundua kwamba wameanza kuota mvi mapema kuliko umri wa miaka 35 au 40. Matatizo kwenye kiungo kinachodhibiti ukuaji mwilini, yaani thyroid huweza pia kusababisha mtu kupata mvi kabla ya kufikisha umri wa miaka 35. Pia ukosefu wa vitamin B12 unatajwa kwa sababu nyingine.Kuna watu ambao hata kama wana umri wa miaka 60 bado hawataki kuona nywele nyeupe vichwani mwao .

  Watu hawa huangaika huku na kule kutafuta dawa kuondoa mvi na pengine kutumia rangi ya nywele ili kufanya rangi ya nywele nyeupe zisionekane. Huu ni kama mwendawazimu kwa kiasi fulani. Kwanini? Kwanza kuna ukweli kwamba nyingi kati ya hizo zinazodaiwa kuwa rangi za kuondoa mvi, zina athari katika mwili wa mtumiaji. Lakini wendewazimu mkubwa zaidi ni kitendo chao cha kukataa ukweli ambao inabidi wajivunie.
  Mvi bado ni dalili ya busara. Kama umefikia umri wa kuota mvi na hujafanya jambo lolote la maana na hujatoa mchango wowote wa maana kwa familia yako au jamii unamoishi ni lazima utaficha mvi zako. Kwanini? Kwa sababu utaona haya sana kuonekana kwamba umri wako ni mkubwa lakini hujafanya lolote.

  Ninaposema mchango wa maana sina maana ya fedha au mali, bali zaidi nina maana ya mawazo ya kujenga na pengine kuandaa misingi ya kujenga kwa nia ya kuleta maendeleo baadaye.
  Hebu chunguza kwa makini, utagundua kwamba watu wote wanaojaribu kuficha mvi ni wale watu ambao wametawaliwa sana na vionjo na tamaa ya miili yao kuliko maendeleo ya binadamu. Ni wale watu ambao hata kama wana fedha, hawajajua hasa wako hapa duniani kwa sababu gani. Hivi ndivyo ilivyo kwa sababu watu wa aina hii huhofia sana umri, huhofia sana kufa kwa sababu hawajakamilisha walichokuja kukifanya duniani kwasababu hawajajua bado.
   
 2. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mvi ni dalili ya ujinga unakaribia kufika.
   
 3. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mara nyingi huwa hivyo!
   
 4. papag

  papag JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  ​basi mimi ni mjinga namba moja kwa sababu umri nilionao na mvi zilizokuwepo kichani na kwenye ndevu ni balaa
   
 5. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  ni kweli ndugu Mtambuzi...binafsi nilikuwa na rafiki O-level ambaye alikuwa na mvi kichwan lakin alikuwa na matendo yenye busara ingawa sijui ni kwa nini akawa na ilhali ni under 20 inawezekana ni urithi.
   
 6. kamwendo

  kamwendo JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 80
  ni kweli ndugu Mtambuzi...binafsi nilikuwa na rafiki O-level ambaye alikuwa na mvi kichwan lakin alikuwa na matendo yenye busara ingawa sijui ni kwa nini akawa na mvi ilhali ni under 20 inawezekana ni urithi.
   
 7. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sa hata mimi ni kama wewe, ni wachache wenye akili we watazame wengi wao wanazipaka rangi ndevu/nywele zao kua nyeusi huoni kama wajinga.
   
 8. papag

  papag JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  sasa ile hali ya kupaka dawa au piko ili ziwe nyeusi hapo ndio ujinga unapoanzia.kwa sababu mtu akikuangalia usoni anajua tu hili zee.na kama bado yanki anajua juu huyu bado dogo
   
 9. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa hio tunakubaliana wengi wao ni wajinga.
   
 10. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Exceptions zipo, lakini mvi ni dalili ya uzee. wanaokuwa na mvi at 20s or 30s, ni matatizo ya genes. Wanaopaka rangi nyewele ili ziwe nyeusi na hivyo waonekane bado vijana -hii ni psychological problem-wanajua umri wao, lakini hawataki kukubaliana na hali halisi. Mimi nilikuwa mmoja wao na pamoja na ku-dye nywele zangu mara kwa mara bado niliendelea kuamkiwa na watoto na vijana: "babu shikamoo". Mwishowe ilibidi niache.
   
 11. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Basi mie nina upungufu wa vitamini B12 cause nina mvi mbili tatu na umri wangu bado kabisa..
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  aisee mimi ni mvivu sana wa kusoma, nitarudi baada kumalizia nilipofika!
   
 13. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  tabasamu ni ishara ya furaha,
  Chozi ni ishara ya kilio,
  Jasho ni ishara ya kuchoka,
  Mvi ni ishara ya ..... : (a) uzee (b) inheritance (c) kuishi miaka mingi (d) U-Lowasa
   
Loading...