Hahahahahahahahha hivi sasa ukiulozwa shida yako nini utawajibu nini?
Unasema?! Si mpaka nitake kuuliwa!
Nagonga mara 2 tu... najua mlango kugongwa mara 2 watakausha kusikilizia kujua ni nani! Then, najifanya kupiga cm na kuongea kwa sauti hadi wasikie: "Hoyaa nipo mlangoni kwa chige hapa lakini inaelekea hayupo!"
Nikifika hapo nakausha... najua ndani watashangilia kuona Jini Kisirani halijui kwamba wapo! Lakini hapo hapo kapresha kataanza kuwapanda kwamba how come niseme hawapo wakati wameacha viatu nje!
Hisia za kuibiwa viatu lazima ziwakate stim huko ndani kisha hapo hapo nawasindikizia jungu nikijifanya naendelea kuongea na cm: "Yah, nimegonga mlango lakini kimya!"
Nikifika hapo, nakausha; kisha napigilia nyundo: "sio rahisi bhana, mbona Sikitu keshampiga chini wiki 2 sasa! Nahisi kama hayupo kwa Suzy basi kwa Subira!"
Napiga hilo jungu huku nikijua ndani yupo na Jolie Jolie, kisha nachana sanda kabisa: "We humfahamu Subira wewe?! Yule demu wa... enhee, huyo huyo! Sema dah, mwana pale ndo hasikii wala haoni... juzi tu kamnunulia kiwanja Boko!"
Nikifika hapo nategeshea sikio kusikilizia timbwili huko ndani... kumbe huku Jolie Jolie kule kuna Suzy na Subira; Sikitu nae kapigwa chini juzi tu hapa!
Jolie Jolie na tuviatu twako twa buku jero, Subira mwenzio kanunuliwa kiwanja Boko! Hapo usipotoka nduki nguo ya ndani mkononi sio mimi!