Muuzaji si anajulikana………………....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muuzaji si anajulikana………………....!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 18, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa ni mwaka 1988 nikiwa nimekuja Dar kwa kaka yangu baada ya kumaliza kidato cha nne na kufeli vibaya huko kijijini. Tulikuwa tukiishi kariakoo mtaa wa Sukuma. Kaka yangu alikuwa amepanga chumba kimoja na alikuwa ni muajiriwa serikalini katika ule mpango wa Direct employment baada ya kumaliza kidato cha sita mwaka mmoja uliopita. Nilikuja ili kaka yangu anisaidie kupata kibarua huku mjini.

  Alikuwa bado hajaoa, ingawa alikuwa na rafiki yake wa kike. Kuna wakati huyu rafiki yake alikuwa anakuja kisha wanananiliu, halafu anaondoka. Mara nyingi ilikua ni usiku ambapo ilikuwa ikimlazimu kaka kunipa hela ili niende sinema za usiku pale Odeon au Avalon. Hizi sinema za usiku zilikuwa zikianza saa sita usiku na kuisha asubuhi. Siku moja kama ilivyokuwa kawaida ya kaka, alikuja huyo mpenzi wake, akanipa hela ili niende hizo sinema za usiku ili wapate muda wa kujivinjari kama ilivyo kawaida yao. Alikuwa anajua kuwa mimi ni mpenzi wa sinema kwa kuwa huko kijijini kulikuwa hakuna hayo mambo ya sinema.

  Nilipofika pale Odion nikawakuta wasichana fulani na kwa jinsi walivyokuwa wamevaa nikajua ni wale wasichana wanaojiuza usiku maeneo ya Magoti. Nikiwa bado nina tongotongo za ushamba wa kijijini nikajitutumua na kumfuata mmoja na kumuomba niwe naye kwa usiku ule.‘Kwa nini unanitongoza kama vile nimekuwa Malaya?' Aliniuliza baada nya kumwambia shida yangu. Kwa akili yangu ya kijijini nilijua ni Malaya anayejiuza lakini anajifaragua tu. 'Kwani muuzaji si anajulikana tu. Wewe sema dau lako twende tukamalizane.' Nilisema kwa kujiamini. Yule msichana alikasirika na kuanza kunishushia matusi. Wale wenzake watatu nao wakaingilia. Halafu ghafla ikatokea mijamaa miwili iliyoshiba hasa. Wale wasichana bila kuulizwa wakawa wanashitaki kwa ile mijamaa. Bila hata kuuliza ile mijamaa ikanivaa kutaka kunipiga, nikajifanya nawatishia kuruka sarakasi za Kichina kama Bruce Lee huku nikitoa mlio kama wa Paka.

  Weweee…………., ile mijamaa ilivaa na kunitandika kisawasawa, waliokuja kuniokoa ni walinzi wa pale kwenye sinema, lakini nilikuwa nikitoa damu mdomoni na uso ulikuwa umevimba kama kiboko. Wale walinzi waliniuliza ninapoishi nikaawambia, ikabidi wawaombe vijana fulani waliokuwa wanaishi maeneo hayo ya Kariakoo wanisindikize nyumbani, kwani nilikuwa hoi hata kutembea nilikuwa nachechemea.
  Wakati huo ilikuwa ni usiku wa manane. Tulipofika nyumbani wale jamaa waligonga mlango kwa fujo hadi wapangaji wote katika nyumba ile wakaamka.

  Miongoni kwa majirani walioamka kulikuwa na mabinti fulani nilikuwa nikiwaringia kwa kiingereza changu cha bush kuwakoga kuwa ni msomi, na walikuwa wananichukia kweli kutokana na tabia yangu hiyo ya kujifanya mjuaji. Nilipowaona wale mabinti niliishiwa na nguvu kwani nilijua kila kitu kitakuwa peupe. Kaka aliponiona katika hali ile alishtuka sana na kuwauliza wale jamaa walionisindikiza, ni kitu gani kimenipata.
  Wale jamaa walikuwa kama waandishi wa habari, kwani hawakumung'unya maneno, walisimulia kila kitu bila kuficha. Niliwaona wale mabinti wakikonyezana kisha wakacheka kicheko cha umbeya na kusema, ‘leo msomi kakutana na wasomi wenzie.' Sikujibu kitu nilibaki kuwangalia huku nikiwa nimetahayari.

  Kaka alikasirika sana na alinichukua na kunipeleka hospitali kwa matibabu, lakini aliniahidi kwamba nikipona lazima anirudishe kijijini kwani hayuko tayari kuishi na muhuni. Ni kweli kaka alikuwa amedhamiria, kwani baada ya siku tatu nilipata nafuu na alinipeleka stendi pale Kisutu na kunipakia kwenye basi kunirudisha kijijini. Nilirudi jijini Dar mwaka mmoja baadae nikiwa nimepambazukiwa.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Cantalisia, King'asti na Husninyo................marufuku kuchangia huu uzi..................Nikiwaonaaaaaa!
   
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Naomba kujua mdogo wangu Cantalisia, Wifi yangu King' na Niece wangu Husny ni wepi katika hilo kundi... Wale watatu wenye mabaunsa AMA wale washobokaji wa kiingilish cha Bush? lol

  Nimeipenda hii Mtambuzi.


  On a serious note; Uvaaji wa sasa mijini ukiwa jogoo wa shamba waweza fikiri kweli yupo sokoni....:eyebrows:
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hahahahahahaaaa!shikamoo baba!hahahaha!ngoja nimalizie kucheka kwanza narudi baba,kwan cjaona kbs hilo katazo lako lol!
   
 5. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hahaha bruce lee kakutana na jack chan,movie za kichina bana
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  hahaahahahahahahahahahahahahah lol....
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Canta si umekatazwa usikatize hapa? umeanza kiburi kwa babako eeeh? lol
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hahahaha,Msomi umekutana na wasomi wenzio, hapa kama nakuona uso mdogo unapeta peta macho tuu...
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  dah pole sana mtambuzi
   
 10. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Usingetokea hakyanani ningejihudhuru kuchangia huu uzi!! Baba yenu nomaa, sijui alitoka buza na uhaba kiasi gani masikini lol!!!
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kabisa!

  Na mara nyingine huwa nafikiri zaidi na kudhani pengine ni kweli wapo 'sokoni' isipokuwa ni aina tofauti tu ya soko....kuna ile inaitwa 'niche market' (i.e. wanakuwa wamelenga wateja wa aina fulani tu!)
   
 12. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Heshima yako sisy,mbona cjaoona jaman!wala cjakatiza ndio kwanza nataka niweke kambi hapa leo lol!mdingi noma kumbe zile za nyangema ataka kuitwa 2pac hazikumpita lol,leo caichii huu uzi nimeshajitolea kupokea viboko badae!
   
 13. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Wakwetu hata angeweka ulinzi wa mgambo wa jiji lzm ningetia maguu!jaman nyie huyu mdingi wetu ni noumer!kumbe alishawahi kuwa bruc lii!ukinionea dada angu king mwambie aje mbio mdingi kamwaga radhi huku!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hawa wanangu wananipa presha sana, jambo dogo tu kama hili, basi litafika kwa mama Ngina.............Hawana dogo hawa na ndio maana nimetoa angalizo.
  lakini da AshaDii uvaaji huo wa vijiguo vifupi vya kuonesha maungo zamani hizo ilikuwa ni adimu sana labda kama utatembelea Magoti ya wakati huo. ni kweli vile vibinti vilikuwa vimetokea ughaibuni, baba yao alikuwa mwanadiplomasia kule na walikuw awako likizo nikauvaa mkenge. nilikuja kuyajua baadae hayo.
   
 15. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  niseme wazi heading ya uzi huu ilinipa hisia za kumjua alieanzisha uzi huu. Big up mtambuzi.
   
 16. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Jana nimekutana na kadada kamevaa kikaptura hicho, chepesiii kama cha kulalia yaani kila kitu wazi!! Niambie sasa alivojichora hiyo mimake up, dah kinyango hakifai, mwendo wake ungecheka uzimie kama anafanya matangazo vile!!!
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280

  We endelea tu, habari yako utaipata nyumbani......................Mtoto hujui la mwadhini wala la mnadi swala!
   
 18. S

  STIDE JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nadhani ni waleee watatu wenye Mabaunsa, maana wale washobokaji wa ki-english hawakutajwa idadi!!
  Pole sana mkuu nadhani sasa unalijua vyema jiji!!
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hata wewe kumbe umemjua eh!
   
 20. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Aisee, unajua siku hizi mimi ni kunguru muoga, yaani nikionana na wale wadada pouwa nawapitia mbali maana huwezi jua ni yupi yuko sokoni na ni yupi asiye sokoni mambo yote kama Mamtoni mwanangu
   
Loading...