doriani
Member
- Nov 24, 2019
- 42
- 38
Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania kumekuwa ni jambo la kupigiwa mfano kwa upande mmoja na lenye kutiliwa mashaka kwa upande mwengine kutokana na kukosekana ushahidi wa kisheria unaothibitisha kuwa umefanywa kihalali kwa mujibu wa hati ya Mkataba wa Muungano.
Hizi ni nchi mbili ambazo ni Jamhuri tena zilikuwa huru na kila moja ilikua na kiti chake Umoja wa Mataifa. Jamhuri hizi zilikuwa na mabaraza yake ya kutunga Sheria Bunge kwa upande wa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, kwa mujibu wa sheria za kimataifa vyombo vya kutunga Sheria vina umuhimu mkubwa katika mchakato wa kuziunganisha nchi.
Kazi ya Mbunge ya kuidhinisha Muungano ya nchi hutanguliwa na hatua ya kuwashirikisha wananchi kwa kuwauliza iwapo wanataka nchi zao ziungane. Hilo halikutendeka Tanganyika wala Zanzibar. Wengi wanaamini kwamba Muungano wa Tanzania hauna uhalali wa kisheria kwa sababu masharti ya uhalali wa Muungano huo yalikuwa ni pamoja na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar baada ya kukubaliwa na Marais wa nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar).
Kuna kumbukumbu za kuridhiwa na Bunge la Tanganyika lakini hapana ushahidi hadi hivi sasa wa kuridhiwa kwa Mkataba huo na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
Kifungu cha (Vlll) cha Mkataba wa Muungano kinaeleza hivi: "Mkataba huu wa Muungano utahitaji kuthibitishwa kwa kutunguwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na Mkataba kupitishwa na kuundwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufwata masharti yaliokubaliwa. "
Maelezo ya kuthibitisha madai haya yametolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo wa Pili wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Makamo Mwenyekiti wa CCM.
Amesema:" Mimi binafsi nilikua mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, kwa wakati mmoja au mwengine, kwa cheo kimoja au chengine kutokea kuanzishwa kwa Baraza hilo hapo January 1964 hadi mwaka 1984 na nimeshindwa katika kumbukumbu zangu kupata ushahidi wa kufanyika kikao cha Baraza la Mapinduzi kama Zanzibar au Dar es Salaam ili kuthibitisha Mkataba wa Muungano".
Hebu mpaka hapa na itoshe kuweza kuujadili mada hii.
Sent using Jamii Forums mobile app