Muungano una uhalali wa kisheria?

Muungano una uhalali wa kisheria?

Ahahahaaaa [emoji3][emoji23] [emoji1787] Mayalla umenikumbusha ujanani mwangu, early 70s
Kwetu huko tulikuwa tunawavizia wakitoka sokoni au hata kanisani. Ni kubeba mazima mabegani na ukishafikisha ndani ni NDOA tayari hiyo [emoji1787][emoji23]. Yaani asubuhi yake yeye mwenyewe huona aibu na kuridhia kubaki kuwa muolewaji. Hata kupigana kesi zutu ziliishia huko huko . Hakuna kuperekana POLICE [emoji3][emoji1787]. Ukipigwa nawe vizia . Maisha yalikuwa mazauri hatukuwa na kina Corona .

Lakini ipo siku moja lazima muungana huu utakufa. Kumbuka USSR

Odhis *
Kwetu bado ipo,japo wanabeba kama tayari mnauhusiano,mwanaume akiamua unaenda tu,maana anakuwa ametoa mwariko kwa angalau vijana watatu,asubuhi namapema anatumwa mshenga kwa binti kwenda kutoa taarifa ili wasimtafute,na kulipa faini.

Ila huu muungano wetu changamoto,hasa kwenye suala la kutangaza habari za CORONA
 
Kuwepo kwa Muungano wa Tanzania kumekuwa ni jambo la kupigiwa mfano kwa upande mmoja na lenye kutiliwa mashaka kwa upande mwengine kutokana na kukosekana ushahidi wa kisheria unaothibitisha kuwa umefanywa kihalali kwa mujibu wa hati ya Mkataba wa Muungano.

Hizi ni nchi mbili ambazo ni Jamhuri tena zilikuwa huru na kila moja ilikua na kiti chake Umoja wa Mataifa. Jamhuri hizi zilikuwa na mabaraza yake ya kutunga Sheria Bunge kwa upande wa Tanganyika na Baraza la Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, kwa mujibu wa sheria za kimataifa vyombo vya kutunga Sheria vina umuhimu mkubwa katika mchakato wa kuziunganisha nchi.

Kazi ya Mbunge ya kuidhinisha Muungano ya nchi hutanguliwa na hatua ya kuwashirikisha wananchi kwa kuwauliza iwapo wanataka nchi zao ziungane. Hilo halikutendeka Tanganyika wala Zanzibar. Wengi wanaamini kwamba Muungano wa Tanzania hauna uhalali wa kisheria kwa sababu masharti ya uhalali wa Muungano huo yalikuwa ni pamoja na kuridhiwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar baada ya kukubaliwa na Marais wa nchi mbili (Tanganyika na Zanzibar).

Kuna kumbukumbu za kuridhiwa na Bunge la Tanganyika lakini hapana ushahidi hadi hivi sasa wa kuridhiwa kwa Mkataba huo na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.

Kifungu cha (Vlll) cha Mkataba wa Muungano kinaeleza hivi: "Mkataba huu wa Muungano utahitaji kuthibitishwa kwa kutunguwa sheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya watu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Baraza lake la Mawaziri, na Mkataba kupitishwa na kuundwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar kwa kufwata masharti yaliokubaliwa. "

Maelezo ya kuthibitisha madai haya yametolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo wa Pili wa Jamhuri ya Muungano pamoja na Makamo Mwenyekiti wa CCM.

Amesema:" Mimi binafsi nilikua mjumbe wa Baraza la Mapinduzi, kwa wakati mmoja au mwengine, kwa cheo kimoja au chengine kutokea kuanzishwa kwa Baraza hilo hapo January 1964 hadi mwaka 1984 na nimeshindwa katika kumbukumbu zangu kupata ushahidi wa kufanyika kikao cha Baraza la Mapinduzi kama Zanzibar au Dar es Salaam ili kuthibitisha Mkataba wa Muungano".

Hebu mpaka hapa na itoshe kuweza kuujadili mada hii.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu kuu za kiusalama zilizotufanya kuung'ang'ania muungano hazipo tena. Uwepo wake utabaki ktk siku ambazo ipo madarakani, tena kwa pande zote mbili za Bara na Visiwani.

Vinginevyo wananchi wengi kutoka pande zote mbili wameshauchoka, hasa upande wa Zanzibar. Muda utaamua kuhusu jambo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kisheria japo ni kweli Zanzibar haiku ratify muungano ila umehalalishwa na performance ya vipengele vya muungano.

Kama ili uhalali wa ndoa sio cheti cha ndoa ni consummation ya ndoa.
Mkichukuana na mtu, mkaishi kinyumba kama mke na mume, mkafanya tendo la ndoa kwa ridhaa yenu, kisheria itahesabika kama ndoa, hata kama hamna cheti cha ndoa, inaitwa presumption of marriage, ni ndoa yenye haki zote ispikuwa haina talaka.

Hivyo mkataba wa muungano ni mkataba halali hata kama mwanzo Zanzibar haikuridhia, lakini kitendo cha Zanzibar kutimiza vipengele vya muungano, kunahesabika ni kuridhia by performance.

Hili tumelizungumza sana humu
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani? - JamiiForums

Pia articles of union za muungano ni makubaliano yaani agreement na sio mkataba sio contract. Kila mkataba ni agreement ila sio kila agreement ni mkataba. Ili agreement iwe mkataba lazima iwe na sifa ya kuwa enforced by law, Articles of union ni agreement for life, not enforceable by law na hauna kipengele cha kuvunja mkataba, hivyo muungano wetu adhimu ni for life na tutaulinda kwa gharama yoyote
Je, Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu ya Muungano?!. - JamiiForums

P

Ahsante kwa maelezo...



Cc: mahondaw
 
Hongera sana Mheshimiwa nahodha
 

Attachments

  • Nahodha- isingekua muungano,Zanibar tungevurugana tu.mp4
    39.7 MB
Back
Top Bottom