Muundo huu wa Muungano utatuumiza sisi Wazanzibar!

Mkuu Kashorobana,

Mumeumizwa wapi wakati kama mnajua mnaumizwa mbona hakuna alodai kutoka hadi muda huu vipi halafu sisi hatukimbilii Oman si raisi juzi juzi katoka huko huko na yule membe sijui mamba ama ndo yalee baniani baya kiatu chake dawa eehh

Huu muungano wa nchi na kimkoa uvunjike bwana hakuna sababu yoyote ya kuwa na muungano na watu wanaolialia kama wanawake wakati wanatunyonya sisi watanganyika. Tanganyika hoyeeee
 
Bendera na mawimbo ya taifa yanawasaidia wakagua magwaride... sisi Wanzibar wananchi twatake fedha mifukoni jama!


Hawa wanzanziari waliograb ardhi Huku bara itakuwaje? Watarudi pemba na unguja? Rasmu iseme hatima ya ardhi ya tanganyika
 
Bendera na mawimbo ya taifa yanawasaidia wakagua magwaride... sisi Wanzibar wananchi twatake fedha mifukoni jama!

Unataka fedha ijae vipi mifukoni wakati siku nzima unashinda kwenye vijiwe vya kahawa unacheza Draft na bao tu??
 
Bendera na mawimbo ya taifa yanawasaidia wakagua magwaride... sisi Wanzibar wananchi twatake fedha mifukoni jama!

Mzee mtapewa pesa mkivunja muungano? Waarabu wanawadanganya sana. Yaani mtapewa pesa mifukoni! Si watanganyika hatuutaki huo muungano. Najivunia kuwa mtanganyika.
 
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,
Tulisema humu mtandaoni usimwamshe aliyelala(Tanganyika).
Kelele za waZanzibari za kutaka kujitoa Muungano na kutaka kubebwa na serikali ya Muungano, haya ndiyo matokeo yake.
Kwwa muundo uliopo Tanganyika haifaidiki sana kiuwakilishi na hata kiutawala.
Sasa Zanzibar ile kibri ya kupitisha katiba ya GNU ya Znz kuwa nchi ilitushangaza wengi.
Kwa muelekeo wa muungano, Znz ndio watkuwa waamuzi kubaki au kujitoa, nyufa ziko dhahiri.
 
Hawa wanzanziari waliograb ardhi Huku bara itakuwaje? Watarudi pemba na unguja? Rasmu iseme hatima ya ardhi ya tanganyika
Mimi nsona chess inayochezwa ni kula kete muhimu kwanza.
Huko mbele hilo la Wazanzibari kama foreigners kusurrender ardhi ni lazima litakuja, kama si kesho basi kesho kutwa.
Hili valangati walilianzisha wenyewe.
 
Suali sio serekali ngapi,ni mamlaka kamili.zanzibar kwanza.

"Zanzibar ikijitenga kwa tamaa au ulevi wa madaraka basi hamtokaa salama,dhambi ya ubaguzi itawatafuna milele hamtokaa salama kamwe,mtaanza hamtaki muungano mtakuja tena hatutaki pemba/unguja ziunganee then mtaendelea hamtokaa salama"--JK nyerere
 
Wazanzibar Wakivunja muungano basi siku hyo hyo Tanesco wakate nyaya zile za tegeta ambazo zinaingilia kunduchi baharani kupeleka umeme znz.
 
"Zanzibar ikijitenga kwa tamaa au ulevi wa madaraka basi hamtokaa salama,dhambi ya ubaguzi itawatafuna milele hamtokaa salama kamwe,mtaanza hamtaki muungano mtakuja tena hatutaki pemba/unguja ziunganee then mtaendelea hamtokaa salama"--JK nyerere

Maneno ya nyerere ni msahafu au biblia?
 
Unataka fedha ijae vipi mifukoni wakati siku nzima unashinda kwenye vijiwe vya kahawa unacheza Draft na bao tu??

Kwani Vijana wenu wanaoshinda kwenye maandamano wao wanapata je Pesa?
 
Wachangiaji... Suala la kuwa muungano uwepo sio hoja... Tunataka uwepo.... Hapa twajadili muundo tu!
 
Me nawahurumia wanawake tu na watoto pale purukushani za hawa jamaa zitakapo anza. Lakini hawa vijana wachoma makanisa wasepe tu. Wakiamua kuchoma makanisa yote wakiwa na nchi yao watajijua wenyewe.
 
Maneno ya nyerere ni msahafu au biblia?

Tuliza mtori jomba, nyama ziko chini, kwani msahafu na bibilia si vilikuja na meli jomba..we tulia uone kama maneno yatatimia, kuhusu kuwa bibilia au msahafu hilo halikuhusu.
 
zanzibar padogo sana kuitengeneza nchi yao na wabara hawakutambua wazenji wanataka nn. Bila kificho wanataka nchi yao. Mtazmo wa tusiwalazimishe saana kuwa kama sisi.
 
Lakini nyie ndio mlianza chokochoko kwamba bara inawaumiza basi nasi tukadaka hoja yenu. Mlitakiwa muikatae hoja ya serikali tatu tokea mwanzo pale viongozi wenu walipoanza kuupigia kelele muungano uliopo. Kwa sasa umechelewa sana ndugu yangu. Hata sie bara tumechoka na ndugu zetu kuuwawa zenj kwa kisingizio cha muungano. Bora tuwache mtembee wenyewe. Lakini usife moyo kuna mambo ya msingi bado yako kwenye muungano.
Najua Viongozi wetu wanapenda huu muundo kwa sababu ya Madaraka. Lakini kwa mwananchi wa Kawaida wa Zanzibar huu muundo hauna tija kwetu. Tusubiri tuone.

Kasheshe @ Bububu,
 
Muungano ni kitu kizuri sana hasa huu wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe.., oops samahani nadhani nilitaka kusema Zanzibar na Tanganyika ambao ghalama kubwa za kuuendesha zimekuwa zikibebwa zaidi na bara. Jambo moja ni kwamba unafiki hautakiwi katika jambo hili. Ikiwa kumekuwepo na kelele nyingi kutoka ubande wa Zanzibar kwamba Muungano haufai na wamekuwa wakitaka kujiondoa (tangu enzi za Nyerere) nadhani hii ni fursa kwao kusimamia kile wanachokitaka ili tusipoteze mihela mingi katika miaka michache ijayo kulazimika kubadili tena katiba ili kuuvunja muungano. Wakati ni huu!

Kiuchumi nadhani itakuwa ni bora Muungano uvunjike maana kwa kiasi kikubwa kwa miaka angalau kumi hadi 20 ya mwanzo tangu kuvunjwa muungano Tanganyika itanufaika kwa kuuza bidhaa nyingi kwenda Zanzibar na kutuingizia pesa za kigeni. Ikumbukwe Tanganyika itaweza kuuza katika nchi ya Zanzibar kuanzia mkaa hadi umeme na kuingiza pesa za kigeni Tanganyika.

Pendekezo langu ni bora Tume ya marekebisho ya katiba ikaja na katiba mbili; moja ni ya Tanganyika, na ya pili ni ya Muungano ambayo hii ya pili ndiyo itakayokuwa mwongozo katika masuala yanahusu muungano. Nasema hivi kwa sababu Zanzibar wenyewe wanayo katiba yao. Hivyo kwa kuwa na katiba ya Muungano itarahisisha mambo pindi muungano ukifika ukomo, ni suala tu la kuichukua katiba ya Muungano na kuiweka katika aidha makumbusho ya taifa au kuitumbukiza baharini katika mpaka wa Tanganyika na Zanzibar!
 
waende zao hatuna hajanao tupunguze na matumizi yasiyo ya lazima, kama galama za umeme, vyuo vikuu, matibabu nk.
Watuchie nafasi zetu kariakoo, namanga, buguruni kwa mnyamani, magomeni mapipa na kwingine kulipokaliwa na wapemba kibao.

tiger one sikubaliani na wewe....acha ubaguzi wewe
serikali tatu sawa ila tusianze kubaguana....hizo serikali ni kwa ajili ya kujitawala lakini bado tutakuwa watanzania.
 
Back
Top Bottom