Muswada wa Sheria ya DNA wapitishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Sheria ya DNA wapitishwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Apr 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,783
  Trophy Points: 280
  Muswada wa Sheria ya DNA wapitishwa


  Thursday, April 23, 2009 11:53 AM
  BUNGE la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imepitisha muswada wa sheria ya kusimamia matumizi ya Teknolojia ya DNA ya binadamu nchini
  Muswada huo ulipitishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Makyusa Bungeni jana.

  Mwakyusa alisema, sheria hiyo itatumika kutambua magonjwa ya urithi kabla na baada ya mtoto kuzaliwa, kuchukua tahadhari na kutengeneza tiba ya magonjwa hayo.

  Alisema muswada huo ambao utatungwa kwa sheria itakayotumika katika tafiti na tiba, kinga na vilevile kuwalinda wananchi watakaoweza kuathirika na matokeo ya uchunguzi ya teknolojia hiyo.

  Vilevile alisema sheria hiyo italinda katika kugundua makosa mbalimbali ya jinai na migogoro ya kijamii ambayo kwa sasa yanakwenda kinyume na sheria hizo.

  Amesema matokeo ya uchunguzi wa DNA ya binadamu yatathibitisha uhalali wa mtoto kwa mzazi pia na Mahakamani, wapelelezi, wanasheria itawasaidia kutoa hukumu na hata kuwaachia huru watu aliohukumiwa kimakosa na kwa wale waliobambikiziwa kesi ambazo haziwahusu.

  Muswada huo ulipitishwa baada ya kuungwa mkono na wabunge mbalimbali wakiwemo na wabunge watano wa upinzani.
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  This is now really high time Tanzania is putting herself on the map?
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Najua hii sheria itakuwa na mapungufu mengi, hebu wenye uwezo wa kuiweka hapa atusaidie tuichambue mapungufu yake

  Masa
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Atakaye upata auweke hapa kwa ajili ya kusomwa na wana jf.
  Thanks
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jus thinking big,Hivi wabunge wengi kama Chitarilo wanapo nyosha mkono kupitisha mswada kama huu wa DNA hivi anaelewa chochote kuhusu DNA?

  Nadhani kuna umuhimu wa sheria za nchi kurekebishwa na kuweka kiwango cha elimu ya Mbunge, vinginevyo hawa wawakilishi wetu vihiyo watakuwa wanaendelea kupitisha vitu ambavyo hata hawaelewi maana yake, na tutaishia kuwa na ma buzwagi na IPTL kibao!
   
Loading...