Musukuma: Tuanze na V8 za Mawaziri kuweka mfumo wa gesi ili kubana matumizi

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,865
4,693

Your browser is not able to display this video.

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma ameishauri serikali ianze kufunga mifumo ya gesi katika Gari zote za mawaziri ili kuokoa gharama kutokana na gari hizo kutumia mafuta ambayo gharama yake ni kubwa ukilinganisha na gesi.

Musukuma amesema hayo leo Aprili 25, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akichangia Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2024/2025
 
hapo ndipo shida ilipo unakaa foleni masaa matatu
shida ya tz ndo hyo tunaanzisha ktu kwa mbwembwe ili uendelezaj hakuna, unapromote ktu kwa nguvu zote wakat huo una vituo sijui 2 vya refill kama sio uwendawazimu ni nn, wakitaka hii ishu ifanikiwe wajenge refill stations za kutosha pia waje na mobile refill stations, vinginevo hamna ktu
 
hapo ndipo shida ilipo unakaa foleni masaa matatu
Yani mm nimekaa tuu nimekumbuka Foleni ya kituo flan ...maana haiwezekani uwe unasema una bana matumizi alafu umepoteza 3 hours kupata hiyo huduma. .. wakati huo huo somebody make more than 1 million ??
 
Ndio shida ya TZ promoting and branding tunatumia nguvu sana ...ila ku sustain na management ni zero kabisa
 
HUYU AKIPEWA UWAZIRI HIYO HOJA HATAISEMA TENA
NA KAMA KWELI ANATAKA SERIKALI IBANE MATUMUZI BASI IANZE KUPUNGUZA MISHAHARA YA WABUNGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…