Musoma: Tujikumbushe 1980 - 1990

Musoma: Tujikumbushe 1980 - 1990

majita road pale jioni kuna kasoko unaenda kununua chengu wa kukaanga.

story za wajeda kuteka mabasi.
shule ya msingi nyamatale kuna mburumatale za kutosha.

story za mtu kaokota bastola au risasi kwenye jalala la ffu pale kamunyonge.

ngorika trans chai moto andazi moto.
tanganyika bus mwanza musoma ndio ilikuwa ya kwanza kuwa na video ukiacha farai coach nissan dissel ya dar kupitia nairobi.

mji ulikuwa mtulivu hauna vurugu yoyote.mtoto wa miaka saba hata utembee usiku hakuna wa kukudhuru.
 
mwigobhelo samaki bei rahisi sana pale ukiwahi asubuhi.

ila maji machafu hapafai kuogelea hadi usogee huku karibu na musoma hotel.
 
farai coach
mikate ya united
watoto kuvuka barabara ya ndege/runway kwa miguu. shotcut ya watu wanaotokea mwisenge kuja kwenye hizo shule

matengere
mazara
nakumbuka siku tunamuaga mwinyi pale uwanjani
umitashumta
mitihani ya ujirani mwema mnabeba madawati kwenda shule jirani.
maloko.
sangara kule aliitwa chengu.
matani.
mcc.
mchakamchaka.
siku ikija ile ndege kubwa ya jeshi au airtanzania mnawahi kushangaa. au ile foka au ndege ya buyoya alipokuwa anakuja kupata darasa kwa nyerere.
beach...
litungu wakura wakitahiriwa.

mitunge
We jamaa tulisoma wote nini umepiga mulemule

Hakuna aliekulia musoma enzi izo asijue MCC ukumbi wenye kila mchezo na burudani, havipo tena hivi.

Tuliosoma Kamunyonge kuangalia ndege kubwa zilizotua uwanjani kuanzia foka na zile kubwa za jeshi tena tukiwa karibu kabisa na running way ilikuwa kawaida, ili land tunalala chini, badae tunaenda darasani kuzichora

umitashumta uwanja wa Mwisenge kuogelea mwanzo mwisho.

Enzi izo kulikuwa na mashindano ya magari, na Pikipiki watu kama MAMAz na MaZida akichora 8 tunasema kapiga norinda.

Kwenda mjini uwanja wa ndege tunavuka kwa kutaim ndg hata kama ipo juu inazunguka utakimbia uiwai mara kadhaa ndege iliwakuta watu katikati ya running way nakulazimika kurudi juu.

Bwawa la kitaji tuliamini lina mashetani ukipita karibu kama mtoto utavutwa ndani

Tulienda majita na gari kama Ndomi na Bukwaya

Kila wikiendi au jioni tukitoka shule basi tunaangalia kama meli imekuja ikiwa imekuja tunakusanyana tunapakizana kwenye phonex kisha tunashindana kwenda bandarini kupanda meli, tulipahta sana Custom, bandarini tuliingia melini tunakula mashudu na mikate huko mpk jioni.

Wakati mwingine meli kubwa tulipotea na kulazimika kutafta wafanyakazi wa meli watutoe nje.

Stand ya zamani kulikuwa na na Tax (cab) za njano na mpangilio mzuri wa namba, ha ha baba angu alipenda sana kutumia namba 50 na 61 zilikiwa nzuri sana, enzi hizi za mwinyi pesa nje nje tax kama baiskel.

Tuliamini sana story za miujiza ya nyerere na kila ndege yake ilipotua Musoma ale uwanjano watoto wate wa Kamunyonge PS tulisimama madirishani kuchungulia Foka imekuja na Nyerere

I miss Home meen miaka mingi sijakwenda.
 
MIMI KILE KISWAHILI CHA KUWEKA MANENO KAMA, YAANI JA, LILE JAMAA JO, YULE MJASTI, NASKIA NENGE, KANUNUE JOJO
Hapa mpaka nimecheka , ja na mjasti. Longtime sana nambie mjasti hata sijui maana yake ilikuwaga kutoka wapi
 
kuna mzee mmoja mkoloni saana alikuwa anaishi nyasho nyuma kidogo krbu na kanisa la sabato kamunyonge.

akiwepo utakuta kibao mlangoni YUPO
asipokuwepo HAYUPO
au akilala AMELALA

wazee wa kijita wenye prinsipo zao hao
ahahahaaa
Mzee mtaragala Chirangi, alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa kama sijakosea, mpk Rais Kikwete amewai kum salute mara kadhaa katika hotiba zake mara ya mwisho wakati anaachia Urais alimtaja kwasasa Marehemu
 
Kwa taarifa yenu. Lile eneo lililoko kati ya stendi. Mtaa wa kusaga, mtaa wa sokoni, na barabara ya Nyerere lilikuwa bustani nzuri katikati kukiwa na maji yatiririkayo. Sina uhkika lakini bustani hiyo imeendelea kulipiwa na serikali ya uingereza kuitunza mpaka ikaleta mzozo halmashauri kwa kuwa hela hizo zilikuwa zinaliwa na wajanja.
 
kuna mzee mmoja mkoloni saana alikuwa anaishi nyasho nyuma kidogo krbu na kanisa la sabato kamunyonge.

akiwepo utakuta kibao mlangoni YUPO
asipokuwepo HAYUPO
au akilala AMELALA

wazee wa kijita wenye prinsipo zao hao
ahahahaaa
Mtaragara Chirangi hakuwa mkoloni. Hakuwahi kumtawala mtu. Alikuwa na principal zake tu. Alikuwa mtu wa mpira sana kiasi cha kufikia kuwa makamu mwenyekiti wa FAT taifa.
 
Mtaragara Chirangi hakuwa mkorofi. Alikuwa na principal zake tu. Alikuwa mtu wa mpira sana kiasi cha kufikia kuwa makamu mwenyekiti wa FAT taifa.
Ameandika mkoloni sio mkorofi
 
Mtaragara Chirangi hakuwa mkoloni. Hakuwahi kumtawala mtu. Alikuwa na principal zake tu. Alikuwa mtu wa mpira sana kiasi cha kufikia kuwa makamu mwenyekiti wa FAT taifa.
kumbe alikuwa mtu mkubwa na kama angekuwa monjo basi big la kisembu
mkuu enzi zile napita pale nilikuwa katoto mwanzoni mwa miaka ya tisini.
yaani hata kama kunashortcut nililazimisha kupita pale angalau nijue anafanya nini au ameweka kibao yuko wapi mida hiyo.
bado yuko hai au ameshatutoka huyo mkulu
 
Ja mimi mpk leo niko musoma tokea nimezaliwapo 1995 nimeona mengi mazuri na mabaya ndani ya musoma tokea ile ajari ya meli iliyo lipuka enzi zile kule kastamu
enzi ya makundi ya ugomvi kama west lawama,mbio za vijiti,jamaica mokers,jitume,mdomo wa furu n.k
nakumbka kile kiwanda cha mikate cha mugube na winners
nimesoma shule nyingi za msingi lakn kama
musoma
iringo
mwisenge
john bosco
o level ni mwisenge secondary but a level nimesoma moshi majengo
daah.. Nakumbuka enzi hizo kanjanja na msomi ndo walikua na tv cable
enz za nyanganira na didi msira koko walikua wapinzani kwenye siasa mtaa wa iringo
tulikua tunaogelea kwa marwa jenelo ila maji yalikua marefu kweli
nawakumbka sana hawa maticha mwalimu harrison na mwalimu temu wangap wanawakumbuka?

Musoma love you..
 
Rudini go tuleko chengu bhana.
Vita ya musoma tech na Mara secondary
 

Attachments

  • 2017-06-28 12.53.08.jpg
    2017-06-28 12.53.08.jpg
    225.1 KB · Views: 68
  • tmp_3914-2017-06-28 12.53.08313439712.jpg
    tmp_3914-2017-06-28 12.53.08313439712.jpg
    225.1 KB · Views: 60
  • tmp_3914-2017-06-28 12.53.081239770949.jpg
    tmp_3914-2017-06-28 12.53.081239770949.jpg
    225.1 KB · Views: 63
Back
Top Bottom