Jirani na kwangu hapo... hahaa haa..CABIN wao wanaita kwa mzee KIBINI
Niliwahi kufika sehemu hiyo maharufu ukifika musoma na siku ya kutaka kuondoka na zawadi ya sato/sangara fresh wa kukaanga unapelekwa au kutajiwa hapo.
Mwigobero yupo mshikaji tulimaliza naye la saba hapo town.. Nilikwenda na wife miaka ya nyuma alinipa mzigo wa kutosha samaki.. Siku hizi hakuna kitu hapo.Shibe ya kutosha enzi hizo ukienda Mwigobero samaki kwa koleo,soko la Nyasho au Kamunyonge, jinumbu jifuru ugari wa udaga we achaaaa!!!
Vipi bado hizo kitu sangara/sato zinaandaliwa hapo au ndiyo mpaka vibali!!Jirani na kwangu hapo... hahaa haa..
Muda mkuu na mimi sijaenda mitaa, tunakumbuka enzi tu..Vipi bado hizo kitu sangara/sato zinaandaliwa hapo au ndiyo mpaka vibali!!
Nakumbukia Tembo beach sehemu ya kula bugi nyakati za wikiend baada ya masomo musoma alliance, maeneo ya Sheraton, bweri,Muda mkuu na mimi sijaenda mitaa, tunakumbuka enzi tu..
Muda mkuu na mimi sijaenda mitaa, tunakumbuka enzi tu..
Bila shaka hapa unamuongelea Engineer wa Telecommunications Joseph Bwahna [Joseph 90"]Bwana alimaliza digrii ya engineering kwa first class, na alikuwa ameajiriwa kufundisha chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ila aliamua kurudi kuendeleza biashara za nyumbani na kuziweka katika levo mpya; nilipta kwenye baa yake mwanzoni mwa miaka ya tisini ilikuwa inatesa sana pale Musoma.
Hata George Masatu alitokea Musoma huko huko ingawa kipaji chake kilianza kupanda akiwa Pamba ya MwanzaWachezaji mahiri wa mpira wa Miguu..
Enzi hizo Ahmad Omary Nyarujoya alichezea Young Africans akitokea Musoma.
Ally Mchumila/Mkombozi pia alichezea Young Africans akitokea Musoma.
Marehemu Nico Bambaga alichezea Simba na Malindi akitokea Musoma..
Kulikuwa na vipaji sana enzi hizo kina Bita John aliyewahi kuchezea Pamba FC .
Miaka ile timu za mpira wa miguu kama Usagishaji,RTC ya Musoma,Pamba ya Musoma.
Waamuzi maarufu wa mpira wa Miguu enzi hizo Mzee Abdi..kina Okuku..sijui kama bado wako hai.
Dunia inaenda kasi sana.
Mtaa wenye madanguro uliitwa mtaa wa Rutiginga, hiyo bkb ilitokana na kina dada toka bukoba waliokuwa wakijiuza pale mtaani.Zamani sana miaka ya sabini mtaa wa Kusaga ulikuwa wa madanguro, wenyewe wakiuita BKB-sikuwahi kutafuta kujua maana yake kwa vile nilikuwa mdogo sana;
Inawezekana ni kwa vile majina ya Kusaga na Rutiginga ni ya ukoo mmoja. Mbunge wa Musoma mwaka 1965 alikuwa Rutiginga kama sikosei jina hili, na ndilo lilopewa mtaa huo. Rutiginga, Kusaga, na Msonge, aliyekuwa na na biashara ya duka na Taxi, walikuwa na undugu na mama yangu mzazi ndiyo maana nikaijua Musoma miaka ya sitini na sabini. Nilikutana na binti mmoja wa Msonge sekondari. Kutokana na wanaume kuoa wake wengi, hao akina Kusaga walikuwa pia na muunganiko na ukoo wa Majinge, ambaye alikuwa mtemi wa eneo hiloMtaa wenye madanguro uliitwa mtaa wa Rutiginga, hiyo bkb ilitokana na kina dada toka bukoba waliokuwa wakijiuza pale mtaani.
Sio Mwigobole ni "MWIGOBERO"Kwanza kabisa wasalamu wanajumia hapa Jukwaani, baada ya kamaliza mfungo na Kisha sikuu ya Eid tunarejea kama kawaida.
Kwa vijana wa sasa ambao tumezaliwa Mkoani Mara katika wilaya ya Musoma Miaka ya 1980,1990. Kuna baadhi ya radha tulizipata kupitia mkoa wetu pendwa pamoja na matukio mengine ya kusitikitisha na kufurahisha kipindi hicho. Kwa kweli huwa nikikumbuka mpangangilio wa zile shule za msingi pale Musoma mjini huwa napata stajabu na kuwapa hongera waliofanya ubunifu ule.
1. Shule ya msingi Azimio
2. Shule ya msingi Mwembeni
3. Shule ya msingi Iringo
4. Shule ya msingi Mkendo.
Ukirudi katika viunga vya mji kwa wakati huo tuko wadogo Mida ya Jioni mitaa ya Iringo hapa kuna soko jioni unaenda kujipatia kichwa cha samaki sangara kwa Jina maarufu "Spika" Hahaha kwa kweli ilikuwa raha sana.
Kwa upande wa majina maarufu kipindi hicho MAMAS HOTEL, TAJIRI PANJU, SHARIFU (Sasa marehemu), KAKINDA, SULTAN (hapa walikuwa wanauza koni), JUMBA LA SINEMA, MILANGO MMOJA, KITAJI, CHAMBIRI, MSETI, MUSOMA BUS (na mengineyo utaweka unalokumbuka)
Sehemu za kutisha kipindi hicho ilikuwa ni makoko huko tuliambiwa kuna mtego wa Nyuki na huko ndio mafagio yalikuwa yanatoka. Habari mbaya nayokumbuka ilikuwa ni ajali ya Boti kuzama na iliua karibia watu wote waliokuwa wanaenda kuchukua Dagaa vizingani kama sikosei ilikuwa 1992 au 1993 maiti zikaletwa pale Mwigobole Mji mzima ulikuwa ni vilio tupu.
KAMA KUNA KITU UNAKUMBUKA UNAWEZA KUWEKA HAPA TUJIKUMBUSHE NA MUSOMA YETU.
Sahihi. Miaka hiyo mtaa wa Kusaga waliishi wahindi. Ukivuka mtaa wa sokoni ndiko yalikokuwa makazi ya waswahili.Inawezekana ni kwa vile majina ya Kusaga na Rutiginga ni ya ukoo mmoja. Mbunge wa Musoma mwaka 1965 alikuwa Husein Kusaga Rutiginga kama sikosei jina hili, na ndilo lilopewa mtaa huo. Hussein na Msonge, aliyekuwa na na biashara ya duka na Taxi, walikuwa na undugu na mama yangu mzazi ndiyo maana nikaijua Musoma miaka ya sitini na sabini. Nilikutana na binti mmoja wa Msonge sekondari
Ni kweli: Msonge kwangu alikuwa kama mjomba. Aliuwawa na majambazi kwa kudhani aliwadhulumu biashara fulani ya magendo.Sahihi. Miaka hiyo mtaa wa Kusaga waliishi wahindi. Ukivuka mtaa wa sokoni ndiko yalikokuwa makazi ya waswahili.
Nilimfahamu mzee Msonge, kama nakumbuka vyema aliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi.
Musoma naifahamu vizuri sana. 😆😆 Lakini nafikiri Kusaga ni hiyo barabara inayotokea hapo kwenye round about.Halafu kweli wewe unaijua Musoma vizuri sana. Nimeangalia tean Google maps na kuamini kuwa Kusaga ilikuwa huo mtaa A, halagu Rutiginga ulikuwa huo mtaa B
Ninataka kwenda kutembelea Musoma tena tangu mwak 1975 nilipoondoka, na siku moja tu nilipokuwa hpo kusimamia wanafunzi wa engineringi kwenye kiwanda cha samaki mwaka 1995. Unaweza kunipa tips za wapi pa kutembelea leo? Ni Miaka 50 imepita kiasi kuwa sina rafiki tena mjini hapoMusoma naifahamu vizuri sana. 😆😆
Hata mimi nina zaidi ya miaka 6 sijafika huko, lakini Musoma si mji unaokua kwa kasi sana.Ninataka kwenda kutembeklea Musoma tena tangu mwak 1975 nilipoondoka. Unaweza kunipa tips za wapi pa kutembelea?