Musoma: Tujikumbushe 1980 - 1990

Musoma: Tujikumbushe 1980 - 1990

Mzee mtaragala Chirangi, alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa kama sijakosea, mpk Rais Kikwete amewai kum salute mara kadhaa katika hotiba zake mara ya mwisho wakati anaachia Urais alimtaja kwasasa Marehemu

Huyo aliwahi kushika vyeo kadhaa hapo Musoma, ikiwemo uongozi wa chama cha Mpira.
Mzee mtaragala Chirangi, alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa kama sijakosea, mpk Rais Kikwete amewai kum salute mara kadhaa katika hotiba zake mara ya mwisho wakati anaachia Urais alimtaja kwasasa Marehemu
 
Kulikuwa na mpiga zeze maarufu. Mzee Nyang'ombori. Alikuwa haoni lakini aliweza kutoka kwake Buhare kwenda sokoni na stendi kupiga zeze lake akiomba.
Moja ya nyimbo zake ulihusu ndege aliyetua Musoma akiwa kavalishwa pete, "inyonyi iyo yasokele Roma"
 
Pale kanisa katoliki musoma kulikuwa na Padre James akimaliza misa anavua joho anaanza kupiga makofi watoto waliokuwa wanacheza kanisani.
Miaka ya mwanzoni 70 hiyo.
Huyo Padre alitokea Tabora. Ukiambiwa historia yake hutaamini. Tuliosoma pale RC Primary School (sasa Mwembeni) tunakumbuka ukali wake. Ila baadae alibadilika na kuwa Mchungaji!!
 
Umemsahau kichaa maarufu pale mitaa ya kati akiitwa Matinde
Sijui kama bado yupo huyu alikuwa akitembea na furushi la mizigo.

Alikuwepo tabu, pia kichaa huyu kukaa uchi kama dakika tu.

Alikuwepo Mungu baba, huyu alikuwa akitembea na machuma anaogopwa vibaya.

Miaka ya 94/95 alikuwepo mwingine karibu na kambi ya jeshi ile ya Kamnyonge kwenda Nyamatare aliitwa Nyango huyu nae alikuwa moto, akibeba mawe mtaa unafungwa

Alikuwepo Kakinda matata sana ila matisi ndio kwa wingi.

Alikuwepo mwingine alikuwa anavaa shuka hivi ukimpa pesa anaimba katondo Mariam nemuka. Ha ha ha zamani sana hii. Sijui kama wapo tena hawa
 
mkuu huu uzi ni kwa vijana waliozaliwa Musoma mjini sisi wa vijijini hatutakuwa na mchango ingawa maeneo tajwa tunayafahamu kiasi
 
Ja mimi mpk leo niko musoma tokea nimezaliwapo 1995 nimeona mengi mazuri na mabaya ndani ya musoma tokea ile ajari ya meli iliyo lipuka enzi zile kule kastamu
enzi ya makundi ya ugomvi kama west lawama,mbio za vijiti,jamaica mokers,jitume,mdomo wa furu n.k
nakumbka kile kiwanda cha mikate cha mugube na winners
nimesoma shule nyingi za msingi lakn kama
musoma
iringo
mwisenge
john bosco
o level ni mwisenge secondary but a level nimesoma moshi majengo
daah.. Nakumbuka enzi hizo kanjanja na msomi ndo walikua na tv cable
enz za nyanganira na didi msira koko walikua wapinzani kwenye siasa mtaa wa iringo
tulikua tunaogelea kwa marwa jenelo ila maji yalikua marefu kweli
nawakumbka sana hawa maticha mwalimu harrison na mwalimu temu wangap wanawakumbuka?

Musoma love you..
Nipooooooooo Sana holy holm
We jamaa tulisoma wote nini umepiga mulemule

Hakuna aliekulia musoma enzi izo asijue MCC ukumbi wenye kila mchezo na burudani, havipo tena hivi.

Tuliosoma Kamunyonge kuangalia ndege kubwa zilizotua uwanjani kuanzia foka na zile kubwa za jeshi tena tukiwa karibu kabisa na running way ilikuwa kawaida, ili land tunalala chini, badae tunaenda darasani kuzichora

umitashumta uwanja wa Mwisenge kuogelea mwanzo mwisho.

Enzi izo kulikuwa na mashindano ya magari, na Pikipiki watu kama MAMAz na MaZida akichora 8 tunasema kapiga norinda.

Kwenda mjini uwanja wa ndege tunavuka kwa kutaim ndg hata kama ipo juu inazunguka utakimbia uiwai mara kadhaa ndege iliwakuta watu katikati ya running way nakulazimika kurudi juu.

Bwawa la kitaji tuliamini lina mashetani ukipita karibu kama mtoto utavutwa ndani

Tulienda majita na gari kama Ndomi na Bukwaya

Kila wikiendi au jioni tukitoka shule basi tunaangalia kama meli imekuja ikiwa imekuja tunakusanyana tunapakizana kwenye phonex kisha tunashindana kwenda bandarini kupanda meli, tulipahta sana Custom, bandarini tuliingia melini tunakula mashudu na mikate huko mpk jioni.

Wakati mwingine meli kubwa tulipotea na kulazimika kutafta wafanyakazi wa meli watutoe nje.

Stand ya zamani kulikuwa na na Tax (cab) za njano na mpangilio mzuri wa namba, ha ha baba angu alipenda sana kutumia namba 50 na 61 zilikiwa nzuri sana, enzi hizi za mwinyi pesa nje nje tax kama baiskel.

Tuliamini sana story za miujiza ya nyerere na kila ndege yake ilipotua Musoma ale uwanjano watoto wate wa Kamunyonge PS tulisimama madirishani kuchungulia Foka imekuja na Nyerere

I miss Home meen miaka mingi sijakwenda.
 
Nawasikilizia tu mbona hamjamkumbuka yule mwehu aliyekuwa na toroli na saa zingine alikuwa akiwanasa wehu wenzake wa kike anaoa.
 
Daaaah kuna mengi sana ya musoma kukumbukia
Kama sehemu Kama kwa saa8 ilikuwa imesheheni majambazi,wezi kila uchafu wa kila aina vilabu ya pombe hasa gongo

Musoma samaki walikuwa bei poa sana miaka hiyo ukila sangara kila siku unaonekana masikini sana.Dagaa walikuwa kisukumizio hawa kuwa mboga.matoto ya sangara almaarufu kama MADEGERE/MAJULIJULI yalikuwa bei poa sana.
Maeneo ya baruti na mkumbuka BRYSON Mzee wa video show.
Watoto wa mzee lyambwiga wakolofi balaaa ukipiga m1 wana kuja mji mzima mpaka na mbwa.maeneo ya Rwamlimi.
Musoma ilikuwa poa Sana lkn sasa hivi imefulia balaaa .
 
Uchaguzi Mkuu 1990 Nilipata kibarua cha kuwa msimamizi wa kituo cha kupiga kura, Bweri. Wagombea Jimbo la Uchaguzi Musoma Mjini: Urais alikuwa ni Alhaji Ali Hasan Mwinyi na Kivuli
Ubunge: Abel K. Mwanga na Stephen Maryogo. Chama Kilikuwa Kimoja tu.
Mshindi: Abel K. Mwanga.

Sijui wako wapi hawa wanasiasa wa enzi zetu Musoma.
 
We jamaa tulisoma wote nini umepiga mulemule

Hakuna aliekulia musoma enzi izo asijue MCC ukumbi wenye kila mchezo na burudani, havipo tena hivi.

Tuliosoma Kamunyonge kuangalia ndege kubwa zilizotua uwanjani kuanzia foka na zile kubwa za jeshi tena tukiwa karibu kabisa na running way ilikuwa kawaida, ili land tunalala chini, badae tunaenda darasani kuzichora

umitashumta uwanja wa Mwisenge kuogelea mwanzo mwisho.

Enzi izo kulikuwa na mashindano ya magari, na Pikipiki watu kama MAMAz na MaZida akichora 8 tunasema kapiga norinda.

Kwenda mjini uwanja wa ndege tunavuka kwa kutaim ndg hata kama ipo juu inazunguka utakimbia uiwai mara kadhaa ndege iliwakuta watu katikati ya running way nakulazimika kurudi juu.

Bwawa la kitaji tuliamini lina mashetani ukipita karibu kama mtoto utavutwa ndani

Tulienda majita na gari kama Ndomi na Bukwaya

Kila wikiendi au jioni tukitoka shule basi tunaangalia kama meli imekuja ikiwa imekuja tunakusanyana tunapakizana kwenye phonex kisha tunashindana kwenda bandarini kupanda meli, tulipahta sana Custom, bandarini tuliingia melini tunakula mashudu na mikate huko mpk jioni.

Wakati mwingine meli kubwa tulipotea na kulazimika kutafta wafanyakazi wa meli watutoe nje.

Stand ya zamani kulikuwa na na Tax (cab) za njano na mpangilio mzuri wa namba, ha ha baba angu alipenda sana kutumia namba 50 na 61 zilikiwa nzuri sana, enzi hizi za mwinyi pesa nje nje tax kama baiskel.

Tuliamini sana story za miujiza ya nyerere na kila ndege yake ilipotua Musoma ale uwanjano watoto wate wa Kamunyonge PS tulisimama madirishani kuchungulia Foka imekuja na Nyerere

I miss Home meen miaka mingi sijakwenda.
Umenikumbusha Tax namba 61 ilikuwa maarufu sana na kiwango.
 
Asanteni Sana wadau mbali mbali mliotoa mada tuikakumbuka Musoma yetu enzi hizo kwa kweli nimefurahi Sana na pia huu ndio udugu WA kweli. Shukrani pia Jf kwa kuupa nguvu uzi wangu...
 
Unamkumbuka Sang'e wa Mjini. Wachezaji mpira kina Chamwenyewe, Idd wa Mara Spurs. Bend ya Mara Jazz na mtindo wao wa Sensera na mengineyo mengi
Mkuu nakumbuka pia mtaa WA mkendo Kati pale kulikuwa na wachezaji mpira wakina CHUMILA nadhani walicheza Simba na Yanga ya enzi hizo.[/QUOTE]
Raha nyingine ilikuwa mechi kati ya Musoma Alliance na Mara Sekondari. Ilkuwa lazima wapigane ngumi. Kulikuwa na dogo toka Musoma Alliance, aliitwa Sabuni. Alikuwa mchezaji mzuri sana.
 
Mkuu nakumbuka pia mtaa WA mkendo Kati pale kulikuwa na wachezaji mpira wakina CHUMILA nadhani walicheza Simba na Yanga ya enzi hizo.
Raha nyingine ilikuwa mechi kati ya Musoma Alliance na Mara Sekondari. Ilkuwa lazima wapigane ngumi. Kulikuwa na dogo toka Musoma Alliance, aliitwa Sabuni. Alikuwa mchezaji mzuri sana.[/QUOTE]
Hao walikuwa na ugomvi WA kihistoria walikuwa hawapendani Sana.
 
Hahahhaass noma sana ebu walisoma mwembeni tufahaniane,waliomaliza 2000 kwenda chini darasa la saba
 
Mmenikumbusha mbali sana sana,umitashumta,hahahass maroko hatari,pia harakati za kushindana kupiga matoke mazur enzi hizi marks ni 150,kuna watu walipiga hesabu 49.namkumbuka marehemu mwalimu mkuu maks karuguru pale mwembeni,
 
Back
Top Bottom