Kimilidzo
JF-Expert Member
- Jan 3, 2011
- 1,346
- 613
Hali ya kiuchumi katika mji wa Musoma si ya kuridhisha hata kidogo. Baada ya kukaa wiki mbili mfululizo pale mjini nimegundua hali imekuwa mbaya zaidi kiuchumi compared na mara ya mwisho nilienda. Ikiwa ni katikati ya msimu wa utalii mahoteli ya Musoma hayajai, wateja wengi wa mahoteli pale ni watumishi wa serikali waliodaka viposho vya semina na sio watalii.... Ukienda katika Beach kuanzia Tembo Beach hadi Matvilla beach unagundua kuwa beach zao ni za kiwango cha kidunia yani World Class, lakini hakuna watumiaji, ukiagiza Samaki wa kuchoma unaweza kupata baada ya saa mbili kwa kuwa hakuna stock hotelini kwa vile walaji hakuna, inabidi jamaa afuate sokoni fasta ndio akuchomee. Mji uko kilometer zisizozidi 60 kuingia mbuga ya Serengeti, unapishana na makumi ya magari ya kubeba watalii yakielekea mbugani, yana namba za kitanzania, ukisoma ubavuni yana anuani za Arusha, Dar au Moshi, watu wa Musoma wako busy kununua Noah na Hiace za kubeba abiria zikiwa na majina ya timu za Uingereza. Hawataki kugusa biashara ya kupeleka watalii mbugani
Karibu miji yote Tanzania siku hizi ukitembelea utakuta sekta ya ujenzi imepamba moto, maghorofa yanakwenda juu kwa kasi sana na ukiangalia kwenye ubao unaona Client pale ni mzawa fulani, lakini pale Musoma nimeona jengo linajengwa na mfuko wa hifadhi ya jamii, na ni kama ndio property pekee inayoendelezwa pale mjini.
Ukipita katika vijiji vinavyouzunguka mji utakuta hali ya chakula ni mbaya sana, mihogo ina ugonjwa wa Batobato na Mahindi yalikosa mvua hivyo wananchi wana njaa kali.
Lengo langu sio kuwaponda wana Musoma, ila nawapa Challenge kuwa wakati umefika muamke na kufanya kitu kuendeleza rasilimali zilizopo kule Musoma ili maisha yabadilike. Kuna kila rasilimali pale. Mind u that mkoa wa Mara una dhahabu kila kona na Samaki kibao ziwani. Kweli mnakubaliana na hii hali ya hotel inayochaji shs 50,000 malazi siku moja kuwa na wateja wawili karibu wiki nzima wakati wazungu wanatumia muda mwingi kwenye magari kufika Serengeti??
Najua ni sera mbovu za CCM kutoendeleza uwanja wa ndege wa Musoma, lakini na nyie mjiongeze, acheni kuporomosha majumba Mwanza na Dar, nendeni nyumbani mkaweke fursa za ajira kwa ndugu zenu...
Najua kuna wana JF kibao wa kutoka Mara kama Etaro, Nata, Ngoreme, Chacha, Mwita nk, Hebu tuelezeni kunani pale, mbona maisha yanazidi kuwa magumu?