Museveni tumia akili japo kidogo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,684
729,848
Wakati mashine ya kutibu cancer kwa njia ya mionzi ikiwa imeharibika kwenye hospitali kuu nchini Uganda na kusababisha wagonjwa zaidi ya mia mbili kukosa tiba kila mwezi, Museveni ametumia Shilingi bilioni 15 kwa siku moja tu kwenye sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo

Awali mashine hiyo iliyokuwa iliharibika mara kwa mara ilipigwa marufuku kutumika na kamati ya baraza la nyuklia duniani kutokana na madhara yake kwa mafundi na wa wagonjwa

Kwasasa inadaiwa nchi haina fedha na itabidi kusubiri si chini ya miaka miwili kuweza kupata mashine nyingine
 
hii ni habari kama nyingine, ipo mitandaoni sana...
hata bbc wametangaza kuharibika kwa mashine ya mionzi....
 
Africa bhana!...... Mtu anashinda uchaguzi baada ya kugandamiza democrasia na kuiba kura halafu anatumia billion 15 kujipongeza na kusherekea!
 
Kwa kweli haya mambo yanasikitisha sana aisee.
Nimejiuliza kweli nchi kama Uganda wanashindwa kununua iyo Machine??
Pesa zote Museven anazotumia ovyo na kwa anasa kwanini asinunue iyo Machine??
Hakika Mimi nitamuombea Trump ashinde na aanze na viongozi Wahuaji na wasio na huruma kama Museven na Nkurunzinza.
Africa hakuna kitu kabisa, wacha Watu weupe watudharau kwa nguvu zote aiseee
 
Wakati mashine ya kutibu cancer kwa njia ya mionzi ikiwa imeharibika kwenye hospitali kuu nchini Uganda na kusababisha wagonjwa zaidi ya mia mbili kukosa tiba kila mwezi, Museveni ametumia Shilingi bilioni 15 kwa siku moja tu kwenye sherehe za kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo
Awali mashine hiyo iliyokuwa iliharibika mara kwa mara ilipigwa marufuku kutumika na kamati ya baraza la nyuklia duniani kutokana na madhara yake kwa mafundi na wa wagonjwa
Kwasasa inadaiwa nchi haina fedha na itabidi kusubiri si chini ya miaka miwili kuweza kupata mashine nyingine

Kina JK wa dunia hii ni wengi sana, angalia Mugabe kalitumia dola laki 6 kufanya birthday wakati wananchi wake wanakufa kwa njaa! Eeh Mungu linusuru bara la Afrika na viongozi vijizijizi kama hivi!
 
bushland mwanzoni nilimchukulia kawaida lakini baadae nikawa na maswali mengi juu yake kisha nikaamua kumpotezea, naikumbuka hiyo post

Mi nilivyomwelewa bushland ni kama alimaanisha ninavyofikiri kwamba Bibi Faiza anakukubali ila hawezi kuadmit, ila sasa anaishia kucriticise kila unachoandika.

Ni secret admire wako huyu ila hajataka kusema.
 
Back
Top Bottom