Leo ninafuatilia kwa umakini kabisa sherehe za kuapishwa Rais mteule Uhuru Kenyata na Makamu wake William Ruto. Baadhi ya Marais wa nchi za kiafrika walihudhuria katika sherehe hii ya kihistoria nchini Kenya.
Katika hotuba aliyoito Rais wa Uganda Mzee Museveni amesema mambo mengi ya msingi ikiwamo biashara na uzalishaji wa bidhaa nchi za kiafrika na namna ya ushirikiano wa wanachama wa nchi za kiafrika, pamoja na kuwapongeza vyombo vya habari kwa ukomavu wa utoaji na upashanaji habari.
Mhe. Museveni amesema hataki kusikia habari za ICC (International Criminal Court) nchini kwake Uganda. Amesema kwa kiingereza na akarudia tena kwa kiswahili. Akasisitiza kuwa masuala ya waafrika waachie waafrika wenyewe watayamaliza. Wakati anatoa statement hiyo nimemwona Mhe. Kikwete anacheka kwa kutokutegemea kauli hiyo na kama kawaida yake, Nikamwona Mhe. Kibaki anashangaaa, Nikamwona Mhe. Kagame ametulia kabisa, nikamwona Mhe. Mugabe akipongeza sana kauli hiyo na Mhe. Kaunda na hata rais Kenyata walionyesha kabisa sura za kukubaliana na kauli hii. Kwa mbali niliwaona wanaharakati mbalimbali pia kufurahia kauli hii.
Jambo la msingi hapa ni kwamba ni lazima kweli nchi za kiafrika kuwepo na msingi wa kutokuingiliwa na mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi na kivita, maana wana lengo na kuwaweka (kuwapandikiza ) vibaraka wao na kuwaondoa watu makini ambao wana msimamo na uchungu wa nchi zao.
Na ukiangalia kwa hakika watu wengi wanaopelekwa ICC mara nyingi ni wale ambao wanaonekana kikwazo cha mataifa tajiri kama Marekani na marafiki wake.
Nimeipenda, Mungu ibariki Afrika.