Historia na cv ya Musa Ndile:
Historia na cv ya kamanda musa ndile, kijana huyu machachari katika medani ya siasa na mtu mwenye ushawishi wa mkubwa na wa hali ya juu alizaliwa mjini sumbawanga, ingawa asili yake ni mtu mbeya, alianza harakati zake za kuwatetea wanafunzi akiwa secondari ya makuzani kabla ya kuhamia mbozi mission a mbako aliendelea na harakati za kupinga uonevu kwa wanafunzi wenzake ingawa alipata vikwazo vingi vikiwemo kusingiziwa kesi nyingi lakini pamoja na tuhuma hizo dhidi yake alishinda kesi na baadae aliendelea na masomo, baada ya kumaliza hapo kamanda musa ndile alijiunga na sangu high school mbeya ambapo akiwa katika harakati za kuwania urais wa shule hiyo alifanyiwa zengwe kali, ikumbukwe kuwa huyu kamanda alikuwa anaushawishi wa hali ya juu na mara zote alikuwa hawezi kuona watu wanaonewa akaacha bila kupinga vikali uonevu huo hali hii ilimpelekea kuukosa urais wa shule kitu ambacho bado hakikumkatisha tamaa ya kupigania haki na maslahi ya wanafunzi na wakati huo alikuwa kiongozi wa dini pale shuleni,
Harakati za musa ndile zilipamba moto alipojiunga na chuo pale ifm mwaka 2010, wakati huo alikuwa akiishi mabibo hostel, hostel ya chuo kikuu cha dsm ambapo musa ndile alikuwa akishinda na wanaharakati mbalimbali kujadili kwa kina mambo ya siasa, changamoto za vijana na maendeleo ya taifa letu, akiwa mwaka wa kwanza aliongoza mapambano makali pale ifm ya kuwatetea wanafunzi 1,700/= waliokuwa wanazuiliwa kufanya mitihani kwa sababu ya kukosa ada jambo ambalo lilikuwa linapelekea wanafunzi hao kufutiwa usajili pale chuoni na baadae wakafanikiwa. Mwaka 2011 bwana musa ndile alifanikiwa kuwashawishi wanafunzi kumchagua rais makini ndugu moses mngodo na baadae musa ndile akafanikiwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi ifm, kweli tuliokuwepo pale chuoni tunajua ukweli na umahiri wa musa ndile katika mambo mbalimbali yaliyokuwa na maslahi kwa wanafunzi kama vile kurejeshewa fedha za refund tabriban mill 600 ingawa alipata vikwazo, vitisho na kesi nyingi kutokana na harakati zake.
Ushiriki wa musa ndile kikamilifu katika harakati za kuishinikiza serikali kuongeza fedha za kujikimu kutoka sh.5000/= hadi sh. 7500/= zilizofanyika katika chuo kikuu cha dsm ulimpa nafasi musa ndile kuchaguliwa mwaka 2011 kuwa katibu mtendaji wa tume/kamati ya kusululisha migogoro baina ya serikali na vyuo vikuu akiwa na mwenyekiti wake fahami mastawily pamoja na wanaharakati wengine kama nusrati hanje na jacquline aisaa, kazi waliyoifanya kwa takribani zaidi ya miezi sita na kukutana na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mnamo tar 04/10/2011 na kumtaka ayafanyie kazi madai ya wanafunzi vyuoni, ikumbukwe kuwa miaka ya 2010 mpaka 2011 kulikuwa na migomo mingi katika vyuo mbalimbali kama ifm, udsm, imtu, muhimbili ambapo muhimbili ilisimamishwa kuwa na serikali ya wanafunzi jambo ambalo kamati hiyo ilikuwa inapinga vikali uonevu huo uliokuwa umefanywa na serikali.
Ukiacha historia hiyo kamanda musa ndile amekuwa kaimu mwenyekiti wa chaso pale ifm baada ya kufanya vizuri katika harakati za kukijenga chama baadae mwaka 2013/14 akawa mwenyekiti wa chaso tawi la ifm na mjumbe wa kamati tendaji chaso mkoa wa dsm. Jambo ambalo lilimfanya ajenge chama kwa kasi kubwa sana na kuaminiwa na watu wengi zaidi.
Mbali na hayo musa ndile alifanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi pale chuoni mwaka 2014 kabla ya kumaliza chuo,
Ameshiriki kuratibu zoezi la kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo kwa kiwango kikubwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za chama kama vile uchaguzi wa madiwani kule mianzini mbagala, uchaguzi wa mbunge kule chalinze, kawe pamoja na shughuli nyingine kama vile kuratibu makongamano ya bavicha na chama kwa ujumla.
Kwa hitimisho: binafsi kazi aliyoifanya kamanda musa ndile katika kujenga na kuimarisha chama vyuoni hasa ifm haiwezi kusahaulika kirahisi wala kupuuzwa kwani amepitia changamoto nyingi ikiwemo kushindwa kumaliza masomo kwa wakati kwa sababu ya siasa achana na kesi nyingi za siasa alizokuwa anasingiziwa pale chuoni kwa sababu ya harakati zake za kujenga chama.
Na kwa msingi huu,
Sisi tunaofahamu mabadiliko makubwa ya kisiasa na kiutendaji yaliyofanywa na musa ndile akishirikiana na wanafunzi wengine kutoka vyuo mbalimbali , tunaojua mchango wake katika harakati za kuwatetea watanzania na kukijenga chama chetu tunadhani , tunaamini na tunapenda kusema, kamanda musa ndile anafaa kuwa "mratibu muhamasishaji wa bavicha taifa" kwani ushawishi wake, umahiri, ujasiri, utashi wake pamoja na uadilifu wake ni nguzo muhimu kwa chadema hatika harakati za kuwaelimisha na kuwahamasisha vijana ili tuweze kukijenga chama chetu kwa maslahi ya taifa.
Asanteni sana: