Ukatibu Mkuu Bavicha: Nani kumrithi Mwita?

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
NANI KUMRITHI MWITA UKATIBU MKUU BAVICHA?

By Malisa GJ,

Usiku wa leo Baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) litampata Mwenyekiti wake mpya na Makamu Mwenyekiti watakaoongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano hadi 2024 (kama hawataunga mkono juhudi).
_
Kesho Kamati Tendaji ya BAVICHA taifa itamchagua Katibu Mkuu mpya atakayechukua mikoba ya Kamanda Julius Mwita na kuongoza sekretarieti ya baraza hilo kwa miaka mitano. Yafuatayo ni maelezo mfupi (Profile description) ya wagombea watano watakaochuana kesho kumpata Katibu Mkuu mpya.

1. CPA, PETER KITALIKA
Amezaliwa mwaka 1990. Ana shahada ya uhasibu kutoka chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), na ameidhinishwa na bodi ya wahasibu nchini (NBAA) kuwa Certified Public Accountant (CPA).

Uzoefu katika siasa: Alijiunga na Chadema mwaka 2011 akiwa kidato cha tano. Kwa miaka 8 ndani ya Chadema ameshika nafasi mbalimbali ikiwemo kuwa Mwenyekiti wa msingi kata ya Mtwango, Mwenyekiti wa Chadema tawi la chuo cha uhasibu Arusha (IAA), na Mratibu CHASO mkoa wa Arusha. Kwa sasa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kupitia Wilaya ya Mufindi. Nje ya siasa Kitalika ni Mhasibu na Mshauri wa masuala ya biashara.

2. HEMED ALLY
Amezaliwa mwaka 1989. Ni msomi mwenye shahada ya usimamizi wa kodi, kutoka chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

Alijiunga na Chadema mwaka 2015. Kwa sasa ndiye Mkuu wa Idara ya uenezi ya chama hicho. Ameshiriki programs mbalimbali za kujenga chama ikiwemo "Chadema ni msingi" katika kanda ya Pwani, Kusini, Nyasa na Kaskazini. Yeye ndiye aliyesimamia matibabu ya Tundu Lissu mjini Nairobi kwa niaba ya chama.

Mwaka 2015 aliratibu vuguvugu la "4U Movement" lililounganisha vijana wasomi kumuunga mkono aliyekua mgombea Urais wa UKAWA. Mwaka 2017 alichaguliwa kuwa miongoni mwa waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi mkuu nchini Kenya.

Katika elimu yake amewahi kuwa kiranja mkuu (Shule ya msingi Ruvu), Kiranja wa mazingira (Shule ya Sekondari Galanosi) na Kiranja mkuu (Shule ya Sekondari Edmund Rice, Arusha). Pia amekuwa Rais wa serikali ya wanafunzi Chuo cha Usimamizi wa fedha IFM mwaka 2013/14.

Nje ya Siasa Hemed ni mtaalamu wa masuala ya Kodi, Mjasiriamali, na mchambuzi wa mambo ya kisiasa (Political analyst).

3. GWAMAKA MBUGHI
Amezaliwa mwaka 1989. Ana shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni Mwanafunzi wa Shahada ya Sheria (LLB) chuo kikuu huria cha Tanzania.

Uzoefu wake katika Siasa; amekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Ileje na Katibu wa BAVICHA mkoa wa Mbeya (2014/19). Mwaka 2015 alikua mmoja wa watia nia ya ubunge jimbo la Ileje. Gwamaka ni Balozi wa Umoja wa vijana barani Afrika (United Youth of Africa) tawi la Tanzania.

Ameshiriki operesheni mbalimbali za kujenga chama katika mikoa mbalimbali nchini. Ameratibu program ya Chadema ni Msingi Kanda ya Nyasa na Kanda ya Pwani. Gwamaka ni miongoni mwa vijana waliopewa fursa na Chadema kushiriki katika program mbalimbali za vijana kimataifa. Nje ya Siasa, Gwamaka ni Mchumi na Mjasiriamali.

4. NUSRAT HANJE.
Amezaliwa mwaka 1989. Ni msomi mwenye shahada ya sarufi ya Kiswahili (B.A in Kiswahili Linguistics) kutoka Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

Uzoefu wake katika siasa; ameshiriki operesheni mbalimbali za kujenga chama tangu ikiwemo Chadema ni msingi katika kanda ya Pwani, Kati, Kaskazini, Magharibi na Serengeti. Mwaka 2015 alikua mtia nia ya ubunge katika jimbo la Kigamboni, na mwaka 2017 alikua mtia nia ubunge wa Afrika Mashariki. Ameshiriki mafunzo ya uongozi ndani ya Chama kupitia program mbalimbali ikiwemo Young Politicians in Africa.

Katika safari yake ya elimu amekuwa Makamu wa Rais, shule ya sekondari Benjamin Mkapa, na Mbunge katika serikali ya Wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mwaka 2015 akiwa na wenzie wanne walishiriki program maalumu ya kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea ubunge na mgombea urais.

Baadhi ya wagombea waliopata fursa hiyo ni Joseph Haule (Mikumi), Sam Ntakamulenga (Urambo), John Heche (Tarime V), Ester Matiko (Tarime mjini), Ester Bulaya (Bunda mjini), Joseph Selasini (Rombo), Godbless Lema (Arusha mjini), Patrobas Katambi (Shinyanga mjini), Anthony Komu (Moshi V), Mathias Lyamunda (Bahi), Fanuel Mkisi (Vwawa) na wengine wengi.

Maeneo yote walizunguka kwa gharama zao mwenyewe (bila ufadhili wa chama) na hii inadhihirisha 'committment' ya Nusrat katika kujenga chama. Nje ya siasa Nusrat ni Mwalimu na Mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

5. NOEL C. SHAO
Amezaliwa mwaka 1989. Ni msomi wa Shahada ya mipango na Maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Ni mwanachama wa Chadema na Mwenyekiti wa BAVICHA tawi la Kisale jimbo la Ubungo. Ameshiriki operesheni mbalimbali za ujenzi wa chama ikiwemo Chadema ni msingi katika mikoa ya Dar, Pwani, Kilimanjaro, na Arusha.

Kwa sasa ndiye Katibu Mkuu wa Taasisi ya Umoja wa kizazi cha Kuhoji nchini (UTG), tangu mwaka 2016 baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na Ndugu Ben Saanane. Kupitia UTG Noel ameratibu shughuli mbalimbali za kudai demokrasia na haki za binadamu nchini ikiwemo kuomba uchunguzi huru kutoka taasisi za kimataifa kufuatia matukio ya watu kupotea katika mazingira yenye utata.

Alishiriki pia katika kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe ya kupinga Wakurugenzi wa Halmashauri kuwa Wasimamizi wa uchaguzi. Noel ni Afisa Uhusiano (PRO) wa Kamati ya mshikamano ya watu wa Tanzania na Sahara Magharibi (Tanzania Sahrawi solidarity committee) inayopigania uhuru wa taifa la Sahara Magharibi kutoka utawala wa kimabavu wa Morocco.

Nje ya Siasa, Noel ni Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii kupitia gazeti la Mwananchi, na ni mtaamu wa miradi, ambaye anafanya kazi na shirika la kimataifa la GSC, akisimamia mikoa ya kanda ya kaskazini kama Afisa mradi.!
FB_IMG_1575924752760.jpg
 
Kwa hiyo umeweka picha za hao wagombea wote watano na kisha ukatoka hapo na moja ya kujitegemea ukimaanisha hatujaelewa au?

Tumekuelewa na tumeshajua kuwa umepigia kampeni (KANDA bongomani).
Wajinga hawatanielewa kama na wewe ulivyojificha kwenye kichaka cha karanga! Mgongo lazima uonekane

MATAGA
 
Katika mwaka ambao Bavicha Hawana wagombea umahiri na Machachali ni mwaka huu!

Anyway kila la heri kwa watoto wetu hawa!
 
Katika mwaka ambao Bavicha Hawana wagombea umahiri na Machachali ni mwaka huu!

Anyway kila la heri kwa watoto wetu hawa!
You are not serious!! Unless ungesema maarufu ila kiuwezo wote hapo wapo vizuri hasa Nusrat Hanje ana IQ kubwa sana ni orator pia na Hemed ni mzuri hasa kwenye organization.

Mmoja kati yao atatufaa sana
 
Back
Top Bottom