Tamko la DEOGRATIUS KISANDU mgombea uenyekiti BAVICHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la DEOGRATIUS KISANDU mgombea uenyekiti BAVICHA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, May 18, 2011.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kisandu.jpg  DEOGRATIUS KISANDU

  MGOMBEA UENYEKITI BARAZA LA VIJANA CHADEMA,

  Mimi Deogratius kisandu ninawania nafasi ya mwenyekiti wa Baraza la vijana Chadema Taifa katika uchaguzi utakaofanyika mei 28, 2011.

  Nimesukumwa kugombea nafasi hiyo kutokana na uwezo nilionao katika uongozi, ikiwa ni pamoja na uzoefu, kwakuwa nimewahi kushika nyazifa mbalimbali na kuzimudu vilivyo ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na jamii kwa ujumla.

  Niliwahi kuwa mwalimu wa taaluma katika shule ya sekondari ya sister Irene iliyopo wilaya ya kahama na Mwamala sekondari iliyopo wilaya ya Nzega.

  Mimi nimeamua kugombea nafasi ya uenyekiti kwa sababu ninaiweza kutokana na kujihusisha na uongozi katika chama nikiwa Kaimu katibu wa wilaya ya Lushoto na nafasi nyingine za ngazi ya chini ambazo nimewahi kuzishika awali.

  Natambua uwepo na uhitaji wa watanzania katika rasilimali tulizonazo katika Taifa letu. Mimi nitawaongoza vijana wenzangu kutumia upembuzi yakinifu, kutokomeza nidhamu ya uwoga, unafiki na kupigania haki za wanyonge wa Taifa hili,ili kuwapo ukombozi wa pili wa Tanzania yetu. Ukombozi huu utaletwa na sisi vijana.

  Mahitaji ya vijana ndio wajibu wangu wa kwanza kwa ukombozi wa pili wa Taifa letu.

  Natambua sisi vijana ndio chachu ya mabadiliko katika Taifa lolote Duniani kutokana na nguvu, ubunifu na wingi wetu, hivyo nitawaleta vijana pamoja kwa ushirikiano wa pamoja.

  Nilizaliwa juni 28, 1983 kahama, Shinyanga. Nilianza masomo ya Elimu ya msingi shule ya msingi kahama kati ya mwaka 1990-1996. Elimu ya sekondari 'O' level nimesoma katika sekondari ya Kishimba mwaka1999-2002 na Tabora Boys kati ya mwaka 2003 na 2005 kwa masomo ya 'A' level'

  Mwaka 2007 nilihudhuria mafunzo ya "Crash program" katika chuo cha ualimu Tabora kwa ajili yakufundisha shule za sekondari.

  Kwasasa nipo mwaka wa pili wa masomo katika chuo kikuu kishiriki cha Tumaini(SEKUCO) kilichopo Lushoto nachukua masomo ya Shahada ya kwanza katika Elimu maalum,Siasa na Utawala.

  Mwaka 2010 niligombea ubunge jimbo la Lushoto kwa tiketi ya Chadema na kuwa mshindi wa pili,huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Henry Shekifu.  Aidha, kwasasa ni mwenyekiti wa Chadema Students Organization(CHASO), umoja ulioanzishwa mwaka 2009 kwa ajili ya kuwauunganisha wanafunzi wote wa elimu ya juu, kati na sekondari nchini kote.

  Lengo langu ni kuwajenga vijana kuwa viongozi bora wa baadae pia kuwa na itikadi moja ya vijana nchi nzima ili wawe tayari kushika nyazifa mbalimbali za kulitumikia Taifa kila watakiwapo kufanya hivyo.

  Nikiwa mwenyekiti wa CHASO nimeeneza harakati zangu katika chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM), Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Chuo kikuu cha Tumaini tawi la Lushoto,Chuo kikuu cha Arusha, Chuo kikuu cha Makumira na shule mbalimbali za sekondari ambako yamefunguliwa matawi.

  Kauli mbiu yangu ya kuwahamasisha vijana wenzagu ni "VIJANA TUFUNGE MIKANDA KWA UKOMBOZI WA PILI WA TAIFA LETU" nikiwataka vijana wenzangu wasirudi nyuma katika harakati za kupigania haki zetu na Taifa kwa ujumla, ili kuwa na Taifa linalojali Usawa na Ajira katika nafasi mbalimbali.

  Nataka kuijenga BAVICHA mpya yenye tija kwa vijana wote wa kitanzania ili kila mmoja anufaike na uwepo wa baraza la vijana.Kuvunja makundi na kuleta umoja wenye tija na nia moja ya kujenga BAVICHA na chama kwenda kushika dola 2015.hivyo 2015 ni mwaka wa CHADEMA.

  KWA USHAURI 0655 025 609.
  Deogratius Kisandu
   
 2. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkuu, kamwone daktari haraka kabla hali haijawa mbaya zaidi
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  SHIBUDA aishambulia CCM


  Mbona cjaona shibuda alipoishambulia ccm au macho yangu
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kuna kitu humu jf, jana kulikuwa na taarifa heading inanhusu zito then ndani mambo ya uchaguzi cdm. so wt this?
   
 5. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Wewe hufai kuwa kiongozi maana ni muongo. Kwani ukiweka heading inayoendana na content watu hawatasoma post yako? Ningekuwa mpiga kura ningeku-disqualify kwa hili-maana hujiamini na sio muadilifu. Huu ni wakati wa kujenga chama, sio kuwania uongozi hata kwa mbinu haramu...
   
 6. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uongo hujidhihirisha mapemaaaaaaaaaaaaaa......
  sorry Bw Deo Kisandu kama ningekuwa one of the voters nisingekupa kura yangu..........wewe ni muongo....umekwisha...
  Tubu kabla mambo hayajakuendea kombo..
   
 7. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,632
  Trophy Points: 280
  hii si mala ya kwanza kutokea.unakuta mtu habari inatofautiana heading na kilchomo ndani.hii mod inabidi aifanyie kazi.watu wote wa cdm wanajiamini so sidhani kama mtu anaweza kumtumia shibuda.
   
 8. T

  TwendeSasa Senior Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  crap..utawadanganya umma wa tz
   
 9. m

  msambaru JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Bangi mbaya eeeh!
   
 10. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Big up bro, simama imara usiogope majina ya watu nenda mbele zaidi
   
 11. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wakuu, msiwe wepesi sana kutoa hukumu kwa huyo Deo japo simfahamu.

  Ninachokiona hapa huyu sio Deo Kisandu wala sio mpambe wake bali ni adui yake mwenye lengo mahsusi la kumuharibia aonekane ni mtu wa hovyo.
   
 12. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwambie ajitokeze atolee ufafanuzi kuhusu hizo headings na maelezo yanamhusu yeye. Akikaa kimya watu watajua ni yeye au wapambe wake.
   
 13. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  inamaana hizo comment hujaziona hapo juu hata utueleze kwa nini imetokea hivi? wake up bwana.
   
 14. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,222
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ........................
   
 15. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Una akili sana Butola!:A S thumbs_up:
   
Loading...