Muongozo wa kununua vifaa vinavyotumia processor za intel

sleep issue ilikuwa solved na updates, ilikuwa toka 2015 sidhani kama bado ipo 2017.

jamaa anasema yake haizimi kabisa, unless sijamuelewa.
Hazimi kabisa ila power button kale kataa kanaendelea kuwaka na feni inafanya ila display inakuwa imezima
 
Mi laptop yangu hata celewi imeandikwa Intel (R) Pentium (R) CPU 2020m @2.4GHz 2.4GHz ni saidie hapo mzee
 
Me nahitaji full set, en vp processor za amd zpo vizur?
inategemea kama ni zile APU sio mbaya sana utafanya mambo mengi, japo cpu ni ndogo ila zina gpu nzuri kuliko intel za kawaida.

ila.kama ni hizi fx achana nazo sababu hazina gpu kabisa, itabidi ununue gpu separate.

full set tafuta kwa 300,000 i5 unapata 3rd gen, then hio 50,000 tafuta monitor unapata used sema itakuwa ya kawaida zile za inch 17.
 
Kama kuna fundi wa Software yupo Mbeya nataka aniwekee windows 10 mpya kwenye laptop yangu ni screen touch na awe na Microsoft package 2016 isiyo na matatizo
 
Computer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.

Processor ni nini?

Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?

-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.

-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
processor_01.jpg


Familia ya processor za intel

Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.

1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.

2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop

3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.

4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.

5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.

6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.

7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.

8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.


Generation ya processor(muhimu)

Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.

- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.

- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140

Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.

Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail

Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.


Herufi za mbele ya processor(muhimu)

Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.

Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?

1. Herufi kwenye processor za desktop.

Bila herufi &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770

K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.

R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.

brix1_s.gif


S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.

T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T

2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)

Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.

M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M

U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U

Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y

HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ

MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ

MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX

Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
First of all, Salut boss for the excellent clarification bro...... My Questions will follow soon......
 
NATUMAINI MU WAZIMA WA AFYA LEO TUJADIRI KIDOGO KUHUSU PROCESSOR SPEEDS TOFAUTI ZAKE NA UBORA WAKILA MOJA .

Thread hii kuiandika kw s ki swahili asee ni chenga ko itabid usome ilivo andikwa kizungu mana nenonka intel hamnannamna ya kulitafsiri kabsa kwa kiswahili.

View attachment 380743
Intel is a great processor manufacturing company but they have a way of confusing the buyers with fancy names like Core i3, Core i5 and Core i7. I am sure you would have heard these terms at least once in a while and wondered what they mean. Today we will discuss the basic differences between Core i3,i5 and i7 processors which i think would help you a lot in choosing your next PC.

[https://i0]

History

In the early days, CPU power was completely taken as the clock speed at which it runs. The clock speed of a CPU gives us a nice understanding on how fast a CPU works but not actually how powerful it was. For example a CPU with a 3.0 GHz runs faster than a CPU with 2.5 GHz but the later one may be able to do more work per cycle enabling it to outperform the first one. Intel introduced naming the CPU’s differently (AMD was the first to do though but it didn’t work well for them) using ‘Core’ naming to move out of the clock speed race.

Difference between Intel Core i3, i5 and i7 in a Nutshell

To conclude in a statement, Core i7s are better than Core i5s, and Core i5s are better than Core i3s. The main reason here being performance. In general, Core i3 chips are found in budget PCs and low-end laptops. For a normal user who does browsing and watching videos, Core i3 works just fine. Core i3s have a low Cache size.

The mainstream or mid-range systems usually have i5. Systems with Core i5 are good for a moderate user and light gamer.

The Core i7 CPUs are reserved for – and found usually in – high-end, expensive laptops and PCs. These are used by users who wish to do video editing( For example using premier pro), Lot of Gaming and other CPU intensive stuff.

Number of cores: Core i3, i5 and i7

The first thing you’ll notice from the table is that Core i5 and i7 processors have four cores, while Core i3 models only have two. Out of all the differences between the Intel processor ranges, this is the one that will affect performance the most.

Each core is effectively its own processor – your PC would still work (slowly) with just one core enabled. Having multiple cores means that the computer can work on more than one task at a time more efficiently, which will help keep your system running snappily even if you have tasks, such as an antivirus scan, running in the background.

Having several cores can also drastically increase the speed at which certain programs run. This doesn’t apply to all applications, as creating software that takes advantage of multiple cores is difficult. While two cores are now the accepted minimum in a processor, if you generally only tend to have a handful of tabs open in a web browser and your most demanding application is a word processor, you won’t see a huge benefit from a quad-core chip. However, modern games benefit from quad-core chips as does video encoding.

Typically all the Core i3s comes with Hyper-Threadingcapabilities in them. Some versions of Core i5s have Hyper-Threading and Turbo boost features enabled.

Coming to the big brother- i7, it has comes with anywhere from 2 to 8 cores with Hyper-Threading, Turbo boosting and Overclocking abilities.

Core i7s are the best Intel has to offer for general consumers while Core i3s being the most affordable in the series ( forget Pentium).

share idea yako Ulonayo kwakuonhezea kukosoa au kuchangia chochote unachokijua......
Thanks
 
laptop chache sana duniani haziruhusu kuongeza ram, naweza kwenda kkoo nikanunua laptop used ya 150,000 nikanunua hdd ya 1tb kwa 100,000 na ram 4gb kwa 30,000 jumla gharama ni 280,000 hapo sababu we unaangalia ram na storage ukiingia kichwa kichwa utauziwa laki 6 hadi 8. cpu na gpu ni muhimu sana sababu ni ngumu kuongezeka.
Naomba nifahamishe kuhusu hii kitu gpu mkuu maana sielewi inakuwaje na pia utaiangalia mf. Kwenye laptop utakayotaka kuinunua?
 
hamna kitu hapo mkuu, kwa kifupi cpu zote zinazoanziwa na N mwanzon zina core za Atom ambazo hazina nguvu kabisa. uzuri wake zinakula umeme kidogo watts 2 hadi 10 na zinakaa sana na charge ila perfomance yake ni ovyo
Mkuu hivi hizi core za Atom kifupi utazigundua kwenye processor zinazoanziwa na herufi gani na gani?
 
Back
Top Bottom