Muokoeni mama yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muokoeni mama yangu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mazeejoh, Feb 21, 2012.

 1. M

  Mazeejoh Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante kwa kufungua hii mail. Nimatumaini yangu utapata muda wa kunisikiliza na kuguswa kiasi cha kunishauri haraka iwezekanavyo kwani hali ni mbaya...

  Nalazimika kuanza kwa maelezo yafuatayo ili base of argument and the problem itself ieleweke.

  Sisi tumezaliwa watatu wote wakiwa ni wannaume (1978,1980,1985), Baba ni Mtanzania na Mama ni mtanzania. Tulilelewa kenya wote baada ya kuwa mama alikuwa ana fanya kazi kama mwalimu wa HIgh School kule. Baba alikuwa anafanya kazi kama mwalimu pia lakini 1985 aliachishwa kazi baada ya kuwa mlevi na mgomvi mgomvi tofauti na nidhamu ya taaluma inavyotaka. Alipoachishwa kazi mama akawa yeye ndiyo bread winner wa familia. In 1987 baba alituaga kwamba anakwenda nyumbani (TZ) atakuja baada ya wiki moja huyo ukawa mwanzo wa story iliyojaa Hasira, maudhi, kilio, hofu, upweke n.k. maishani mwa kila mmoja wetu.
  Wiki moja ikazaa mwezi, mwaka, miaka 2,5, 10 hadi 13.

  Ndani ya maika hii yote mateso mama aliyopitia sipati maneno ya kutosha kuelezea, maana hata niandikapo hii post roho inauma sana. Alifanya kila awezalo kutuelimisha, kutulisha, kutuvisha na kutulea katika maadili mema. Alijinyima kila aina ya starehe ili tupate mahitaji yetu, alijituma hadi kununua ngombe wa maziwa ili kujiongezea kipato cha kuendesha familia huku gharama zingine zikimuelemea, kidogo kidogo akapata shamba la eka mbili hili likawa tulizo kwani tulilima vyakula na kahawa ambayo ilimsaidia kulipa ada za shule kwa sisi wote. Yalikuwa ni maisha ya taabu sana, Namshukuru mungu hamna kati yetu aliyemuongezea maudhi kwa kuhitaji kisichowezekana. Raha nyingi za ujanani tulizikosa kwani hela ya kuvaa vizuri, kusoma shule bora, kula vizuri, na vitu vingine vizuri vizuri ambavyo wenzetu walikuwa wakivipata hatukapata, T.V. yenyewe hatukuwa nayo, radio ilikuwa ni hadi betri zipatikane sana sana mwisho wa mwezi. Hali iliendelea hivyo hadi mimi nilipomaliza Form 4 ilibidi nimpumzishe mama kwa kualisha miaka miwili ili wadogo zangu wapate ada ya kumalizia masomo yao. Nilibaki nyumbani na mama yangu nikiwa kama house boy sasa kwani kazi zote zilikuwa zangu mama akienda shule. Hapo ndo mama hata afya yake ikiwa afadhali kwani alipata mda wa kupumzika. Baada ya miaka miwili nikapata nafasi ya kujiunga na college ya Printing and Press Operation, mama akauza ngombe mmoja ilinipate fees ya kujiunga, kweli nikajitahidi kadri ya uwezo wangu na baada ya miaka miwili nikahitimu kwa CREDIT jambo ambalo lilimtia mama furaha sana.
  Mapenzi kama upofu fulani

  Katika kupekua barua zake, mama akakuta barua ya zamani sana ikitokea Tanzania. Mama akapata wazo la kufatilia senders postal address ili kujua hatma ya Baba kwani kwa kipindi chote hichi hatujawahi kusikia lolote kutoka kwake. Mara nyingi tulifikir kwamba kafa. Akakusanya hela ya kutosha na kutuaga kwamba anakwenda kumtafuta baba. Alifanikiwa kuja hadi Dar es Salaam na baada ya kufuatilia mwenye anuani ya barua akabahatika kufika kwa Baba Mkubwa wangu. Baba alipatwa na shock ya kufa mtu baada ya kumkuta mama kule jioni aliporudi. Alishindwa cha kusema na kujielezea ikabaki ameduwaa. Baada ya maongezi na mealewano ikaeleweka kwamba lazima sisi (watoto) turudi kwenye chimbuko letu (TANZANIA) ukizingatia wote ni wakiume. Basi mama akarudi na kutupa habari yote, ilikuwa vingumu kuamini na kuelewa eti baada ya miaka Ishirini na Miwili tungeweza kuondoka na kuacha kila kitu lakini kutokana na kuweka furaha ya mama mbele ikabidi tukubaliane nalo.

  BABA ANARUDI
  Baada ya mwezi mmoja toka mama arudi toka Dar es salaam. Baba akawasili, lakini tofauti na mategemeo yetu alikuwa hafanani na mafanikio ambayo tulidhani angekuwa nayo baada ya miaka yote hiyo. Tukampokea na kuamini huu ndo mwanzo mpya wa maisha na familia kwa ujumla. Cha kushangaza wote wawili waliamua kuuza kila kitu ambacho mama yangu alikuwa nacho ilikuja Tanzania waanze upya. Hiyo kwangu ilikuwa dalili ya baba hayupo hali njema ki fedha. Tukauza kila kitu na kuhamia Tanzania. Fedha iliyopatikana ndiyo ikawa kianzio, ikumbukwe mama hajastaafu hivyo ukasukwa mpango ahamishiwe shule jirani na mpaka wa TARIME na KENYA ili aweze kumalizia miaka yake na kupata pension yake. Mama akawa anakwenda asubuhi Kenya anafundisha na jioni anarejea Tanzania. Mshahara wake ukawa unalisha familia kwa sababu Baba hana kazi, mshahara huo huo ukawa unatumika kuwalipia wadogo zangu shule za sekondari hapa Tanzania. Baada ya miaka miwili mama akaja na idea ya kuanzisha shule, ikabidi baba atumie uwenyeji wake na wakapata eneo, mama akatoa hela ikawa kodi ya jengo na baby care class ikaanzishwa. Mama akalazimika kupata mkopo ilikuwezesha Baby Class itabuke ikiwa pamoja na huduma zake, waalimu wawili, uji na chakula cha mchana vikawa vivutio vvya vya wanafunzi kuongezeka. Pakawa na ongezeko kubwa la wanafunzi hadi wazo likawa kuanzisha shule kubwa. Basi Mama aakarudi benki tena na kuchukua mkopo mkubwa zaidi, likapatikana eneo kubwa na majengo matatu yakajengwa.

  Wazazi wangu walienda hatua moja mbele wakafunga ndoa kanisani, hili lilitokea baada ya kubaini baba anawatoto wengine hapa Dar es salaam. (3 watatu wakike 1 dume) baba alibisha sana na kumshawishi mama kwamba ili aamini yupo naye tu na hana mpango wa kado basi wafunge ndoa.. Mama alipostaafu pension yake ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba Baba akawa anaitamani. Akaanza visa kwamba haheshimiki kwenye familia kwa sababu hana kazi maalum, akaanza kumlaumu mama eti ndiye anayeharibu familia, eti anatushawishi sisi watoto tudharau baba. Haya yote kwa sababu baba anapenda sana pombe, mara kadhaa amekutwa na vimwana akijirusha, hadi disko, aibu kweli kwa mama na familia kwani wote ni watu wazima na mama ni mzee wa kanisa. Sasa sisi hatukulelewa katika misingi ya ulevi na kujirusha kiasi hicho lazim tutofautiane naye. Lakini hili likawa chanzop cha kuleta vurugu za kumnyima mama usingizi. Ili kumtuliza mama akamnunulia Canter ambayo angeweza kufanyia biashara ya kusafirisha samaki na mazao, yeye akawa akipata hela haonekani nyumbani analewa hadi mtaji, zikiisha analianzisha nyumbani ili apate hela na kuendelea na ufuska wake. Upande wa pili shule imehsakuwa ngumzo katika wilaya ya MARA, kwani hivi sasa ina Boarding na DAY hadi darasa la SABA, ina magari matatu ya kusafirisha watoto na zaidi ya yote matokeo yake yamekuwa ngumzo MARA nzima. Kwa miaka miwili mfululizo imekuwa imeshikilia nafasi ya kwanza wilayani na kufaulisha wanafunzi asilimia 85%. Credit zote ni kwa mama kwa sababu she has been behind the steering all the way. Baba kazi kubwa bi kunywa na kuspend. Anaiba hadi ATM kadi ya account ya shule na ku draw hela bila ridhaa ya mtu yeyote an kuspend anavyotaka.

  Sasa ametangaza kwamba vyote ni vyake, nyumba, magari shule kila kitu ni chake. Anauwezo wa kufanya chochote awezalo bila ushauri wa yeyote yule. Mimi nimeoa na nina motto mmoja hapa DAR, mdogo wangu ameoa ni mwalimu na ana mtoto mmoja anaishi nyumbani tarime, mdogo wetu wa mwisho yupo SAUT Mwanza mwaka wa tatu. Kwangu na wote tunaamini huku nikumuonea mama kwani jasho lote ni lake.
  SWALI LANGU NI JINSI GANI NITAMUOKOA MAMA ILI?

  Kumuajibisha baba kwani ni dhahili siyo responsible but in human?

  Mali ziwe salama?

  Baba asiweze kuuza au kuingia mkataba wowote bila kuhusisha familia yote.?

  Kumdhibiti baba asifanye vurugu?

  Kuhakikisha nia ya mama kwamba vyote vifaidi watoto wa tumbo lake tu litimie.?
  Ahsante kwa kufungua hii mail. Nimatumaini yangu utapata muda wa kunisikiliza na kuguswa kiasi cha kunishauri haraka iwezekanavyo kwani hali ni mbaya...

  Nalazimika kuanza kwa maelezo yafuatayo ili base of argument and the problem itself ieleweke.

  Sisi tumezaliwa watatu wote wakiwa ni wannaume (1978,1980,1985), Baba ni Mtanzania na Mama ni mtanzania. Tulilelewa kenya wote baada ya kuwa mama alikuwa ana fanya kazi kama mwalimu wa HIgh School kule. Baba alikuwa anafanya kazi kama mwalimu pia lakini 1985 aliachishwa kazi baada ya kuwa mlevi na mgomvi mgomvi tofauti na nidhamu ya taaluma inavyotaka. Alipoachishwa kazi mama akawa yeye ndiyo bread winner wa familia. In 1987 baba alituaga kwamba anakwenda nyumbani (TZ) atakuja baada ya wiki moja huyo ukawa mwanzo wa story iliyojaa Hasira, maudhi, kilio, hofu, upweke n.k. maishani mwa kila mmoja wetu.  Wiki moja ikazaa mwezi, mwaka, miaka 2,5, 10 hadi 13.

  Ndani ya maika hii yote mateso mama aliyopitia sipati maneno ya kutosha kuelezea, maana hata niandikapo hii post roho inauma sana. Alifanya kila awezalo kutuelimisha, kutulisha, kutuvisha na kutulea katika maadili mema. Alijinyima kila aina ya starehe ili tupate mahitaji yetu, alijituma hadi kununua ngombe wa maziwa ili kujiongezea kipato cha kuendesha familia huku gharama zingine zikimuelemea, kidogo kidogo akapata shamba la eka mbili hili likawa tulizo kwani tulilima vyakula na kahawa ambayo ilimsaidia kulipa ada za shule kwa sisi wote. Yalikuwa ni maisha ya taabu sana, Namshukuru mungu hamna kati yetu aliyemuongezea maudhi kwa kuhitaji kisichowezekana. Raha nyingi za ujanani tulizikosa kwani hela ya kuvaa vizuri, kusoma shule bora, kula vizuri, na vitu vingine vizuri vizuri ambavyo wenzetu walikuwa wakivipata hatukapata, T.V. yenyewe hatukuwa nayo, radio ilikuwa ni hadi betri zipatikane sana sana mwisho wa mwezi. Hali iliendelea hivyo hadi mimi nilipomaliza Form 4 ilibidi nimpumzishe mama kwa kualisha miaka miwili ili wadogo zangu wapate ada ya kumalizia masomo yao. Nilibaki nyumbani na mama yangu nikiwa kama house boy sasa kwani kazi zote zilikuwa zangu mama akienda shule. Hapo ndo mama hata afya yake ikiwa afadhali kwani alipata mda wa kupumzika. Baada ya miaka miwili nikapata nafasi ya kujiunga na college ya Printing and Press Operation, mama akauza ngombe mmoja ilinipate fees ya kujiunga, kweli nikajitahidi kadri ya uwezo wangu na baada ya miaka miwili nikahitimu kwa CREDIT jambo ambalo lilimtia mama furaha sana.  Mapenzi kama upofu fulani

  Katika kupekua barua zake, mama akakuta barua ya zamani sana ikitokea Tanzania. Mama akapata wazo la kufatilia senders postal address ili kujua hatma ya Baba kwani kwa kipindi chote hichi hatujawahi kusikia lolote kutoka kwake. Mara nyingi tulifikir kwamba kafa. Akakusanya hela ya kutosha na kutuaga kwamba anakwenda kumtafuta baba. Alifanikiwa kuja hadi Dar es Salaam na baada ya kufuatilia mwenye anuani ya barua akabahatika kufika kwa Baba Mkubwa wangu. Baba alipatwa na shock ya kufa mtu baada ya kumkuta mama kule jioni aliporudi. Alishindwa cha kusema na kujielezea ikabaki ameduwaa. Baada ya maongezi na mealewano ikaeleweka kwamba lazima sisi (watoto) turudi kwenye chimbuko letu (TANZANIA) ukizingatia wote ni wakiume. Basi mama akarudi na kutupa habari yote, ilikuwa vingumu kuamini na kuelewa eti baada ya miaka Ishirini na Miwili tungeweza kuondoka na kuacha kila kitu lakini kutokana na kuweka furaha ya mama mbele ikabidi tukubaliane nalo.

  BABA ANARUDI
  Baada ya mwezi mmoja toka mama arudi toka Dar es salaam. Baba akawasili, lakini tofauti na mategemeo yetu alikuwa hafanani na mafanikio ambayo tulidhani angekuwa nayo baada ya miaka yote hiyo. Tukampokea na kuamini huu ndo mwanzo mpya wa maisha na familia kwa ujumla. Cha kushangaza wote wawili waliamua kuuza kila kitu ambacho mama yangu alikuwa nacho ilikuja Tanzania waanze upya. Hiyo kwangu ilikuwa dalili ya baba hayupo hali njema ki fedha. Tukauza kila kitu na kuhamia Tanzania. Fedha iliyopatikana ndiyo ikawa kianzio, ikumbukwe mama hajastaafu hivyo ukasukwa mpango ahamishiwe shule jirani na mpaka wa TARIME na KENYA ili aweze kumalizia miaka yake na kupata pension yake. Mama akawa anakwenda asubuhi Kenya anafundisha na jioni anarejea Tanzania. Mshahara wake ukawa unalisha familia kwa sababu Baba hana kazi, mshahara huo huo ukawa unatumika kuwalipia wadogo zangu shule za sekondari hapa Tanzania. Baada ya miaka miwili mama akaja na idea ya kuanzisha shule, ikabidi baba atumie uwenyeji wake na wakapata eneo, mama akatoa hela ikawa kodi ya jengo na baby care class ikaanzishwa. Mama akalazimika kupata mkopo ilikuwezesha Baby Class itabuke ikiwa pamoja na huduma zake, waalimu wawili, uji na chakula cha mchana vikawa vivutio vvya vya wanafunzi kuongezeka. Pakawa na ongezeko kubwa la wanafunzi hadi wazo likawa kuanzisha shule kubwa. Basi Mama aakarudi benki tena na kuchukua mkopo mkubwa zaidi, likapatikana eneo kubwa na majengo matatu yakajengwa.

  Wazazi wangu walienda hatua moja mbele wakafunga ndoa kanisani, hili lilitokea baada ya kubaini baba anawatoto wengine hapa Dar es salaam. (3 watatu wakike 1 dume) baba alibisha sana na kumshawishi mama kwamba ili aamini yupo naye tu na hana mpango wa kado basi wafunge ndoa.. Mama alipostaafu pension yake ilikuwa nzuri sana kiasi kwamba Baba akawa anaitamani. Akaanza visa kwamba haheshimiki kwenye familia kwa sababu hana kazi maalum, akaanza kumlaumu mama eti ndiye anayeharibu familia, eti anatushawishi sisi watoto tudharau baba. Haya yote kwa sababu baba anapenda sana pombe, mara kadhaa amekutwa na vimwana akijirusha, hadi disko, aibu kweli kwa mama na familia kwani wote ni watu wazima na mama ni mzee wa kanisa. Sasa sisi hatukulelewa katika misingi ya ulevi na kujirusha kiasi hicho lazim tutofautiane naye. Lakini hili likawa chanzop cha kuleta vurugu za kumnyima mama usingizi. Ili kumtuliza mama akamnunulia Canter ambayo angeweza kufanyia biashara ya kusafirisha samaki na mazao, yeye akawa akipata hela haonekani nyumbani analewa hadi mtaji, zikiisha analianzisha nyumbani ili apate hela na kuendelea na ufuska wake. Upande wa pili shule imehsakuwa ngumzo katika wilaya ya MARA, kwani hivi sasa ina Boarding na DAY hadi darasa la SABA, ina magari matatu ya kusafirisha watoto na zaidi ya yote matokeo yake yamekuwa ngumzo MARA nzima. Kwa miaka miwili mfululizo imekuwa imeshikilia nafasi ya kwanza wilayani na kufaulisha wanafunzi asilimia 85%. Credit zote ni kwa mama kwa sababu she has been behind the steering all the way. Baba kazi kubwa bi kunywa na kuspend. Anaiba hadi ATM kadi ya account ya shule na ku draw hela bila ridhaa ya mtu yeyote an kuspend anavyotaka.

  Sasa ametangaza kwamba vyote ni vyake, nyumba, magari shule kila kitu ni chake. Anauwezo wa kufanya chochote awezalo bila ushauri wa yeyote yule. Mimi nimeoa na nina motto mmoja hapa DAR, mdogo wangu ameoa ni mwalimu na ana mtoto mmoja anaishi nyumbani tarime, mdogo wetu wa mwisho yupo SAUT Mwanza mwaka wa tatu. Kwangu na wote tunaamini huku nikumuonea mama kwani jasho lote ni lake.

  SWALI LANGU NI JINSI GANI NITAMUOKOA MAMA ILI?

  Kumuajibisha baba kwani ni dhahili siyo responsible but in human?

  Mali ziwe salama?

  Baba asiweze kuuza au kuingia mkataba wowote bila kuhusisha familia yote.?

  Kumdhibiti baba asifanye vurugu?

  Kuhakikisha nia ya mama kwamba vyote vifaidi watoto wa tumbo lake tu litimie.?
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  very interesting and so sad
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Duh embu ngoja wataalam wafike.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Sisi tumezaliwa watatu wote wakiwa ni wannaume (1978,1980,1985).....kwa sasa mtakuwa 34,32 na 27....nyie ni watu wazima na mko huru kujiamulia kwa manufaa ya mama yenu

 5. M

  Mlavumbi Orijino Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimepata hasira mpaka nakosa uwezo wa kufikiri ngoja nipoe kwanza, poleni sana kwa mliyopitia, story yako inatufundisha vitu kadhaa katika maisha. Pole bro
   
 6. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu pole kwa matatizo yanayoikumba ndoa ya wazazi wako. Umejieleza vizuri, ila hujatuambia kama walioana ndoa ya kanisani, msikitini, kimila au waliamua kuishi tu kinyumba.
  Kiufupi wakati baba yako anawaletea vitimbi kule Kenya, mama yako alikuwa na nafasi nzuri ya kuomba talaka wakati ule kwani angeweza kuleta ushahidi wa cruelity anayowafanyia ila hakufanya hivyo kwa hiyo haitakuwa sabcu nzito mahakamani ila itakuwa kama kuelezea tabia ya huyo baba yenu.
  Pili, alipowaacha kenya na kuja TZ kwa muda wote huo mama aliweza kuomba talaka pia kwa kuwatelekeza au presumption of death ila hakufanya hivyo napo pana tatizo.
  Alipoamua kumfata mdingi hapo ndo inadhihirisha kukubaliana na mambo ya mumewe pamoja na vitimbi vyote akamtafuta mwenyewe tena sio baba kamtafuta. Hiyo inaweza kuwa kitu tunaita CONNIVANCE kisheria.
  BUT:
  Mama amefahamu baba anawatoto wengine inamaana alifanya uzinzi, hapa ndipo mama anaweza kuleta ushahidi kama anataka kupeleka petition ya DIVORCE. Huo ni ushahidi tosha na mkiunganisha na CRUELITY na ulevi na utumiaji wa mali za familia hovyo bila manufaa. Ila kumbuka ni kama mama anataka divorce kama walioana kisheria.
   
 7. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Pole. Nimepata fundisho fulani kupitia stori yako. Nami nasubiri kwa hamu wataalam wanasema nini katika hili.
   
 8. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Ila kumbuka unasema kiwanja baba yenu alisaidia katika kuwashauri wanakijiji wawauzie, pamoja hela anaweza kuwa alitoa mama ila hiyo tayari ni joint effort towards that property, mama akiomba divorce na ikakubalika, wanapokuja kugawa mali baba anaweza kupewa sehemu ya mali.
  Wale watoto waliopatikana kwenye uzinzi hawahusiki na mgawanyo hapa.
  Otherwise inaonekana nyie hamumpendi huyo mzee kutokana na vitimbi vyake ila mama anamchukulia poa kama mzazi mwenzie kwani yeye ndiye mwenye uamuzi na sio nyinyi hamuwezi kufanya kitu ukichukulianyie ni wakubwa kabisa itakuwa ngumu kwenu. Mama anatakiwa afahamu ana uwezo wa kukusanya ushahidi tosha wa hiyo CRUELITY, ADULTERY na pia mengineyo kama ulevi wake, na ufujaji wa mali ya familia nk.
  Kumbukeni, baba atapata sehemu ya mgao wamali kama wataachana, maana amecheza karata dume, unajua alijua akibaki kenya ile mali asingepata mgao ndo maana akamsolicit mama auze waanze upya.
  Katika kuanza upya mama akajikuta anamtumha mzee katika ujenzi wa hiyo shule na mali nyinginezo so hiyo ni JOINT EFFORTS TOWARDS THE ACQUIRING THE MATRIMONIAL PROPERTY.
  Mama anasababu zote za kuomba na kupata divorce ila akumbuke kuna sehemu ya mali baba atakuwa entitled. Otherwise nitafuteni for further consultation and representation in the court.
   
 9. L

  LISAH Senior Member

  #9
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole bro inatia hasira sana.
  Hawa na mfumo wao dume ndio maana wanawake wa kenya wameamua kuwatwanga mingumi!

  Hebu wanasheria na akina anania Nkya msaada wenu hapa unahitajika kumkomboa huyu mama.
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,117
  Trophy Points: 280
  Kabla ya kufanya maamuzi hebu mhusishe na MUNGU pia, sijui unaonaje wazo langu maana binadamu wataishia kuku-confuse zaidi na MUNGU huyu usimtafute wala kumshirikisha kwa kubadili dhehebu wala usifikirie kulipa kisasi. Asante
   
 11. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Kama hawakuoana ila waliishi tu kama mke na mume hapo kuna suala la mahakama ifanye PRESUMPTION OF MARRIAGE kama itatimiza vigezo vyote ambavyo nadhani vipo. Then mahakama itapresume kulikuwa na marriage ili kumsaidia mama apate haki yake although kumbuka baba atapewa mgao katika mali.
  Mama afanye maamuzi na wala msimuingilie.
   
 12. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Punguza hasira, hata wanaume wanapata matatizo makubwa kutokana na wanawake.
  Sheria ya ndoa ipo wazi katika kutoa haki kwa wanaume na wanawake, na kutokana na story ya huyu mwenzetu sioni kama huyo mama yake baada ya mateso yote kama alilazimishwa kukaa na huyo mwanaume.
  Alikuwa na uwezo wa kutomtafuta, lakini out of love aliamua mwenyewe so hapa hakuna mahusiano na mambo ya mfumo dume.
  Mianya ya kisheria ipo wazi tena kwa mama msomi na mwenye uelewa kama huyu, its her love to the husband hapo ndo tatizo, watoto wake ni wakubwa na wasomi nao wanashindwa kuingilia sababu hiyo ni ishu ya wao wazazi na huyo mama kuamua.
  Ona jinsi anavyomlea huyo baba hadi kumnunulia gari, hapo kuna mfumo dume upi? Nadhani huyo mama anamapenzi kwa mumewe sema tu amepata bahath mbaya.
  Tuelewe, sheria ipo wazi na mahakama zinawasubiri watu wa jinsia zote, tatizo ni kwamba, marriage conflict ni private matter so anatakiwa aamue na hapo hakuna mfumo dume.
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pole sana! Tusubiri wanaojua sheria..
   
 14. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Du! Pole sana mkuu kwa yote mliyopitia. Naamini wadau wengine watakusaidia zaidi. imenisikitisha sana hii issue.
   
 15. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Mkuu pole sana kwa hilo tatizo mimi sio mtaalamu wa sheria ila mawzo yangu yanaweza kuwa msaada kwako
  Linapokuja suala la kugombea mali kati ya wanandoa linakuwa ngumu kwenu nyie watoto kulitatua kawa sababu hizi zifuatazo:-
  1. Wakati wanaanzisha hiyo miradi waliiandika kwa majina yapi ya mume au mke? Kinachowaponza wanawake ni kuandikisha miradi yao kwa jina la waume zao kitu ambacho ni hatari kwao.
  2.Pili mama yenu kama hatakuwa willing kwa ajili ya kuitetea mali yake nyie watoto mtaishia kupigana bastola. Muulize mama yenu kama yuko tayari kuachana na baba yenu maana wewe unaweza ukawa unahangaika huku jf kumbe mama bado anamuhitaji mme wake.
   
 16. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Hilo la kwanza uliloliongea kisheria halitambuliki, jitahidi usome post zangu hapo juu utaelewa, usijaribu kutoa ushauri wa kisheria wakati tupo wenye fani hapa.
  Kuandika majina hakuna uhusiano wakati wa mgawanyo wa mali, soma post zangu vizuri itakufumbua ufahamu nawe pia.
  Usitie uvivu kusoma mkuu au wewe ni mathematician? Wao ndo wanapata tabu kusoma maandishi mengi.
  I urge you to please read the posts nilizoweka hapo ili usie ukatoa ushauri mwingine wa namna hii although umesdma hujui sheria so pitia upate ufahamu tupo kwa ajili yenu kuwapa kaufahamu.
   
 17. 1

  19don JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  pole sana ndugu mtangulizeni mungu kitikakulitatua jambo hili,
   
 18. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa mkuu ndio nikadeclare interest mwanzoni kuwa mimi sio mtaalamu wa sheria ila majina ya umiliki yanaletaga taabu, ikiwa pale mwenye dhamiri ya kukudhulumu anapojua udhaifu wako uko wapi.
   
 19. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Hiyo labda ni kwenye mashauri mengine yanayohusu mikataba ya kibiashara ndipo umiliki huwa unaleta tabu, yani mkataba wa ndoa ni kitu kingine, una taratibu zake wakati wa mgawanyo wa mali, ukisoma kesi ya BI Hawa d/o Mohammed.V. Ally s/o Seif, imeelezea mgawanyo wa mali na mambo mengine mengi tu. Suala la kuandika jina halinauzito wakati wa kugawana kinachoangaliwa ipi mali ilipatikana wakati wa ndoa period.
   
 20. M

  Mazeejoh Member

  #20
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No prob
   
Loading...