Mungu Yuko wapi?

Wewe sio mwili wewe ni nafsi yaani roho... Kama unabisha sema Mungu yupo ukiwa umefumba mdomo.....


Baada ya kutekeleza hilo zoezi mtafute nani aliye sema hivyo ilijali wewe umefumba mdomo wako ujakenue hata punje ya jino lako moja kuonekana nje.... Ukimpata aliye sema hivyo njoo kwenye huu uzi unitag ukimkosa tena sema huku umefumba mdomo kuwa mimi ni mbumbavu... Afu mtafute tena nani kasema Mpaka umpate....
 
Kuna watu zaidi wanalala na kuamka kuliko watu ambao wameona mbingu na Moto. So mtu mwenye akili timamu anajua ana chance kubwa kuamka kesho kuliko kwenda sehemu fikirishi baada ya kufa
Ndio hauna uthibitisho wala uhakika wa kuamka hiyo kesho, ukisema una chance tena kubwa ya kuamka kesho itabidi utupe sababu za msingi za kuwa na hiyo chance huwezi kusema et kwa sababu nimeona wengi waliyolala na kuamka.
 
Hivi jamani naomba kuuliza kile kilichotokea brazili baada ya kumziaki YESU na kumtukuza shetani ilikuwa ni mambo ya hali ya hewa tu ya liangukia siku Ile au ni MUNGU mwenyewe alishusha Ile dhoruba

Maana naona watu hawazingatii kabisa hili swala yani
 
Umegusa mule mule yaani Asante.
 
Ni sahihi kabsa ulivyofikiri kulinganisha na ulicho aminishwa .
Sijaaminishwa...Mungu Kama ni mmoja kwa Nini kila mtu anakuja na yake. Ni kitu ambacho ukikaa mwenyewe unaweza fikiria ukajua ni uvushaji tu
 
Nitajie nchi ya kiislamu ambayo haina mafuta na haina partnership na marekani afu Ina maendeleo na amani. Ukipata, niite mbwa nimekaa pale.
 
Tofauti inakuja kwenye nini? Maana umetoka kusema kwamba imani(faith) ni kuamini(kukubali) kitu bila uthibitisho, haya hebu eleza huko kuamini unayemuona na kuona anachofanya.
Mi Nikiona mtu ni mwizi mwizi sitamuamini katika vitu vyangu coz najua ye Ni mwizi. Ila we unaamini kitu ambacho hakina uthibitisho wowote tofauti ndo hiyo.
 
Hapo umeleta hoja mpya kama unazungumzia hao wanaoenda kwenye imani fulani kwa sababu za wepesi wa kimaisha tu hawana imani basi hilo ni suala lengine.
 
Bro..hiyo ni akili yako..ndo maana tuna mawazo tofauti...Kama hiyo akili ndo Mungu bac binadamu wote tungekuwa na dini moja lakini dini zipo 10k, coz hizi ni fikra za watu. Hamna kitu kiitwacho roho, fikra zipo katika ubongo. Hizo dhana za roho nafsi moyo ni dhana za watu wa kale wasioelewa mwili wa binadamu, Kama unabisha tikisa ubongo kidogo tu uone Kama utakuwa sawa. Soma biology form 2 itakusaidia
 
Ndio hauna uthibitisho wala uhakika wa kuamka hiyo kesho, ukisema una chance tena kubwa ya kuamka kesho itabidi utupe sababu za msingi za kuwa na hiyo chance huwezi kusema et kwa sababu nimeona wengi waliyolala na kuamka.
It's a better explanation than kusema naamini Mungu yupo coz Kuna kitabu Cha miaka 3000 Cha mababu wayahudi au waarabu wamesema yupo. Na uthibitisho kuwa nitaamka kesho coz najiskia vizuri Leo. That is a better explanation than kusema ni by chance, sio chance,
 
Maswali yako ni mengi sana yanahitaji darasa ili upate majibu yako
 
Mungu yupo mkuu ila habari za yesu, mhamedi sijui manabii mm ndo huniambii kitu huwa sielewi kabisa sababu manabii hadi sasa wapo wanaendele kujitokeza tu
 
We mjuaje niambie kilichotokea Brazil. Maana Kama unaweza amini bikra kazaa unaweza amini chochote kile. Event ya 2019 rio mafuriko yametokea 2023 mkoa mwingine mbali kabisa. Leo hii dar wamtukane Mungu afu 2028 litokee bukoba tetemeko utasema kisa dar wamemtukana Mungu. Jifunze kutafuta habari za ukweli sio story za mtaani, hio issue hata ITV hawajatangaza nor BBC na wewe unakubalikubali tu Kama ulivyokubali mtu kutembea kwenye maji...tumia akili sio matako
 
Umeongelea utajiri na umasikini wa kiuchumi lakini hujaongelea elimu.

Waarabu wakiamini Mungu hapo hakuna contradiction na hoja yangu, kwa sababu hawana elimu.

Na hata hao waarabu kadiri wanavyoongeza uchumi na elimu, imani ya Mungu inashuka.



 
Hapo umeleta hoja mpya kama unazungumzia hao wanaoenda kwenye imani fulani kwa sababu za wepesi wa kimaisha tu hawana imani basi hilo ni suala lengine.
Ndo ukweli...mtu anataka adake pisi ya kiislamu anasilimu anavaa makanzu anadaka pisi. Mtu hawezi ajiriwa au kupandishwa cheo katika institution ya kiislamu anasilimu anapata...fikiria bac
 
Mi Nikiona mtu ni mwizi mwizi sitamuamini katika vitu vyangu coz najua ye Ni mwizi. Ila we unaamini kitu ambacho hakina uthibitisho wowote tofauti ndo hiyo.
Hapo umeeleza upande wa kutokuamini na si kuamini, umetoa sababu za kutokumuamini huyo mtu. Sasa mtu ambaye hujui kama ni mwizi utamuamini kwa uthibitisho upi?
 
Ndo ukweli...mtu anataka adake pisi ya kiislamu anasilimu anavaa makanzu anadaka pisi. Mtu hawezi ajiriwa au kupandishwa cheo katika institution ya kiislamu anasilimu anapata...fikiria bac
Ndio nasema hicho ni kitu tofauti si suala la imani hilo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…