Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Msingi wa hoja zako ni nini?
 
Sijakuelewa,,, kwa hiyo anaitaj Mambo tan?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakuaje kama Mungu ndio kafanya wale wawe waharifu kwa uwezo wake aliokuwa nao ?



Mungu hana sifa ya kutenda ubaya au kusababisha ubaya au kumfanya mtu atende ubaya, matendo yote mabaya ni mkono wa shetani au unaweza sema ni msukumo wa tamaa mbaya za nafsi yake, na hapo ndipo mtu anaposhikwa na hatia kwamba alifanya mabaya kwa nafsi yake huku akijua kuwa hayo anayofanya ni mabaya na hapo Mungu ahusiki aslani.
 
Una uhakika kijana na unalo andika humu

UBAYA KAFANYA MUNGU, MWENYEWE

HESABU 21:6
"; Bwana akatuma nyoka za moto, kati ya watu , wakawauma, watu wengi wakafa";


Kwa kitendo cha Mungu kutuma nyoka kuua watu huo ni uzuri au ubaya ?

HUU KAUSABABISHA kwa PHARAO mpaka pharao akawa mkaidi na jeuri

KUTOKA 4:21
";Bwana akamwambia Musa, utakaporudi Misri , angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini NITAUFANYA MGUMU MOYO WAKE, naye HATAWAPA ruhusa hao watu waende zao";

Kwanini unamlaumu farao kutokuwaruhusu waisrael waende, kumbe ule ugumu kaufanya Mungu mwenyewe kwenye moyo wa Farao ?
 



Sasa Mungu akimuadhibu kiumbe wake aliyemuumba mwenyewe kosa lipo wapi??, si kamuimba yeye mwenyewe na anajua mapungufu yake!!.

Vipi we dogo!!
 
Loo! Hunishawishi ng'0! Hata kwa ndumba nyama siachi kula aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe nawe vipi???!, mbona unachekesha, kwani umeambiwa na nani kwamba Maharage, Mahindi, na matunda au mimea haina UHAI??!,

Huwezi kula mchicha hadi uuchume kutoka shambani kabla hujauchuma unakuwa ni KIUMBE HAI. soma Biology mkuu.
Sasa tule mchanga au vipi Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana inaitwa imani ya mtu, hujawahii ona mtu anasema katupa hela nyingi kwa waganga wa kienyeji hadi ng'ombe katoa, lakini kanisni anataka asitoe hata mia tano eti Yesu alisema toeni bure, tunawatajirisha wachungaji mie huwa siwamalizi kabisa, hivi wale WALAWI walikuwa wanafanya kazi gani? Wakati imeandikwa usiende nyumbana mwa Bwqna Bwana mikono mitupu, Yesu mwenyewe baada ya kuwaponya aliwambia nenda katoe sadaka yako na usitende dhambi tena,

embu mtu mmoja asome hapa 2 Corinthians 9:6-11, Isaya 3:7, Kumbukumbu 12:17-19, Malaki3:10-12, Mithali 3:9-10, kama mtu anakula kila siku anashindwa nini kutenga sadaka angalau ya siku moja, bora usiende kanisan
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo usipotoa sadaka au hizo zaka kanisa litaendeshwa vipi?
Mchungaji na familia yake wataishi vipi? Kumbuka ile ndo kazi yake.
Mtumishi wa Mungu riziki yake hupatikana madhabauni na si vinginevyo.
Labda useme hawa manabii uchwara ndo wanazingua harakati za kanisa la Yesu coz wana warubuni nakuwahadaa waumini wao kwa tamaa ya pesa
 
Mkuu, amini nakuambia. Mzazi hawezi kukufanya lolote kama hukuvunja sheria za Mungu. Kwanza unazjua sheria zenyewe?
Kwani heshima kwa mzazi si ipo katika amri kumi za Mungu? Kama unajitambua sizazi kama unaweza kukubali jambo baya ambalo mzazi atakwambia wewe ukajua sio sahihi akatoa laana na ikashika hapana, vitu vingine ni kujiongeza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu mwenyewe alikuwa anafunga na kuomba, je kama maombi hayakuwa na nguvu kwanini alikuwa anafunga na kuomba? Hapo hapo aliwambia wanafunzi wake mapepo mengine sio rahisi kutoka isipokuwa kwa kufunga nakuomba, hapa kuna watu wanadanganya ili Mungu asahaulike ili atukuzwe shetani wao, washindwe tu kwajina la Yesu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…