Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Mungu nisamehe kwa nilichotaka kufanya

Omesk

Member
Joined
Jan 24, 2020
Posts
34
Reaction score
233
Binafsi kifo cha Mpauko kimenipa funzo sana. Nimepitia nyuzi zote na comment Mungu naomba tu unisamehe kwa mawazo niliyokua nayo.

Binafsi nilizaa 2014 mume akafariki ghafla kwa ajali nikabaki na mtoto. Nilihangaika sana sababu sikuwa na pakushika.

Mama yangu alikuwa Mtendaji alistaafu 2015, bahati nzuri akanipa mtaji milioni 1.5 nikafungua duka la dawa. Mungu akanisaidia nikawa naenda vizuri na maisha, 2016 nikapata mchumba aliyekuwa tempo TANESCO. Mshahara ulikuwa haukidhi na maisha ya kwao yalikuwa duni sana hivyo yeye ndio alikuwa tegemezi.

Kidogo mimi biashara haikunitupa hivyo akikwama nilikuwa namsaidia. Mungu akamsaidia Januari 2018 akapata ajira ya Uengineer mkoa mwingine. Turifurahi sababu tulimuomba sana Mungu.

Baada ya mwaka akanitolea mahari nikahamia anapoishi. Duka nikaweka mtu akaniiibia nikabaki ikabidi nilifunge. Jamaa akanifungulia duka lingine huku tulipohamia. Jamaa mshahara ukawa mzuri hakosi milioni 4 kwa mwezi pamoja na overtime, marupurupu kibao.

Akabadilika akawa hanishirikishi tena, hatupangi pamoja kama zamani tukipata kidogo tunapanga pamoja.

Changamoto ikawa uzazi ukagoma tangu 2018 mwenzangu ana hamu sana ya mtoto. Last year nikapata ujauzito Juni 26 ukatoka. Nimehangaika hospitali, dawa za kienyeji, tiba lishe, bila mafanikio.

Jamaa kaanzisha mahusiano na mfanya kazi wake mpaka kumleta ndani. Nikimuuliza anadai anatafuta mtoto.

Duka nililofungua jamaa hela zote anachukua.
Mtoto wangu shule mwaka huu kasimama. Nikimpigia mama anadai vumilia sasa utaenda wapi ushapoteza kila kitu?

Inafikia hatua unaona dunia imekutenga, huna thamani tena hasa inapofikia usiku jamaa analala nje ukimpigia anadai anatafuta mtoto.

Nilikata tamaa nikaamua nimpe sumu mtoto wangu na mimi ninywe ili haya maumivu yapotee. Juzi nimechukua mtoto tukaja guest house ili tufe wote. Kila nikitaka nimpe anywe anakuja na story nzuri tunacheka naogopa jamani.

Nisamehe Mungu wangu natubu mimi mbele zako. Eee Mungu baada ya kusoma kifo cha mpauko nisamehe mimi. Acha nipambane tu bado Mungu una makusudi na maisha yangu. Sasa hivi saa 11 sijafumba macho hata tone moja.

Jamani tupeane tu moyo haya maisha hatujui tunapitia yapi. Wewe unaweza kuwa na furaha usifikiri ni wote. Mtu akiomba ushauri humu tufarijiane tu wengine JF inatupa faraja sana.

Mbarikiwe
 
Usikate tamaa wakati wa bwana ndio wakati sahihi maana ni miaka mawili tu tangu uanze kuishi naye
 
Pole sana, Tafadhali usimpe mtoto sumu.

Unaweza ukamalea mtoto wako maana ni wengi tumelelewa na Mama zetu bila msaada toka upande wa pili na iliwezekana.

Wasiwasi wangu anaweza kukuletea magonjwa,maana hao wanawake atakuwa anajizolea huko bar na kwingineko.
 
Back
Top Bottom