Si utani ila ni kweli tupu.ndicho ninachomuomba Mungu anisaidie, snipe nguvu ya kukiongea hata Kilosa kichungu kiasi gani. Maandiko yanasema ukweli utatuweka guru.
Back to the topic;
Nimekuwa na hulka ya kuongea uwongo kama Watanzania wengi tulivyo.Juzi Nilikuwa natakiwa mahali SAA kumi na moja kamili alfajiri, nikaa bar hadi usiku wa manane nikashindwa kuamka mapema.
Ilipofika SAA 11 na nusu nkaanza kupigiwa simu, pombe ilikuwa nyingi kichwani kiasi kwamba sikuweza kusikia miito ya zile simu hadi niliposhtuliwa na wife.
Nikaamka mbiombio na kukimbilia Kwenye Gari, nikawadanga waliokuwa wakinipigia Kuwa ninakaribia eneo LA miadi. Speed ilikuwa Kali na utulivu ulikuwa mkubwa barabarani.
Mbele kuna maungio ya Barbara, ghafla Gari iliyokuwa ikitoka Kwenye barabara ndogo ikaingia kwa kazi main road, tukagonganga, UKAWA ni mwisho wa hadithi.
Laiti ningesema ukweli kuwa ndio naamka wale niliokuwa nawawahi wangefanya maarifa mengine na wangeendelea na shughuli na kuniacha nije taratibu.
Kisa cha Pili.
Wife alikuwa anafanya kazi Masaki na tulikuwa tukiishi Kijitonyama. Tulikuwa na Gari moja mbali tulikuwa tukilitumia wote wawili.
Siku hiyo niliondoka na Gari muda wa SAA kumi wife akaamza kunipigia ili nimfuate. Nilikuwa mbali sana nikawa nadanganya kuwa nakaribia kufika.
Wife akasubiri akachoka, akaanza kutembea kwa miguu. Alikuwa amebeba handbag ghafla nyuma ikatokea Gari, vijana wakashika handbag, wakamburuza wife kwa zaidi ya umbali wa mita Mia, akajeruhiwa vibaya, akapoteza Pesa na Baraka muhimu.
Nisingedanganya yasingemkuta. Mungu Naomba usafishe kinywa changu kijue kuongea ukweli ili niwe huru, nisipatwe na mabalaa na mikosi.
Amen