Mungu nisaidie nisifikie hatua hii!!

Mungu nisaidie nisifikie hatua hii!!

Huwa nawaza sana kuusu ndoa yangu apo baada nataman sana tuje kua na furaha mda wote na mke wangu, na naamini itakua ivyo tu
hiyo tamaa uliyo nayo karibu wanaume wote wanayo, ndio maana huwa tukitongoza tunakuwa na juhudi sana, tuna fantasize maisha yale ya hadithi za Cinderella, ila wakati wa kuishi kwenye ndoa, hali huwa haiwi hivyo, zile moments za party, raha tu huisha mapema mno, kama ukizitumia vema, ndio zinazofuel maisha hasa wakati mambo yanapokuwa magumu!
maisha ya ndoa yanapaswa kuwa driven Zaidi na upendo, uhitaji na hulka ya kuthamini na kuheshimu utu! ukitawaliwa na mapenzi tu, siku yakipungua utu ndio utawaweka pamoja, kama ukiishi na mtu asiye na utu au wewe ukikosa utu basi hali itakuwa mbaya na utajuta kuoa/kuolewa!
 
Unanikumbusha tabia ya wengi wetu, akiona tukio ataacha hata shughuli zake, akafuatilie na kupoteza mda wake mwingi tu kufuatilia mambo yasiyomhusu.

Imagine ulikuwa unaenda sehemu muhimu, lakini ukaacha kabisa na kwenda hadi kituoni kumfuatilia jamaa.
Nimeshangaa hata mm. Hv mleta mada ni ke au Me.
Tuanzie hapo kwanza
 
jamaaani[emoji275] [emoji275] roho inauma hayo ni zaid ya mateso
 
Kuishi na mwanamke unatakiwa kuwa mwehu zaidi ya huyo uliyemwona, mwehu zaidi ya thithonje kwa lasie du nationale
 
Wanawake wanavumilia sana yaani utakuta mme anamfokea mkewe mbele za watu, mie na mwenzangu tulikuwa tumesisima walikuja watu 2 bila shaka ni mtu namkewe mwanamme anafoka huyo halafu ni mlimani city ndani mpaka tukajiuliza hawa nimtu na mkewe au mfanyakazi maneno ya ajabu ajabu mwanamme ukimwangalia hata humzanii kwa maneno yanavyo mtoka kwanini usisubili nyumbani!
 
Unanikumbusha tabia ya wengi wetu, akiona tukio ataacha hata shughuli zake, akafuatilie na kupoteza mda wake mwingi tu kufuatilia mambo yasiyomhusu.

Imagine ulikuwa unaenda sehemu muhimu, lakini ukaacha kabisa na kwenda hadi kituoni kumfuatilia jamaa.
Mkuu wala sio kufuatilia kiviiile,ni ile hali unasisimkwa na tukio unaona sio shida kusogea hatua 10 kupata kujua zaidi.
 
kwa hiyo mkuu,ulikua unawanyemelea hadi ukayaona hayo yote,huna kazi za kufanya?
 
kwa hiyo mkuu,ulikua unawanyemelea hadi ukayaona hayo yote,huna kazi za kufanya?
Sio hivyo,ni watu niliokuwa karibu nao katika mazingira hayo kwa hiyo ilikuwa rahisi kufanya observation
 
Anaweza kuwa ni mjeshi huyo maana wao kwa kutoa amri ni namba moja
 
Jamani kuna watu wanaishi maisha ya ndoa kwa kuvumilia sana!Hakika mwanamke kapewa moyo wa uvumilivu sana. Mwanamke anaweza fanyiwa ubandidu na madharau na mumewe lakini akaendelea kukomaa tu kama vile aliokotwa porini na hana kwao

Asubuhi nimeshuhudia tukio la kusikitisha sana jamaa akimfanyia mkewe. Jamaa walikuwa bank akionekana kumuacha mkewe nje...baada ya kumaliza na kutoka alisogea alipokuwa mwanamke mmoja mpole aliyekuwa kapakatia kitoto cha miaka kama minne hivi cha kiume kilichofanana na jamaa!

Jamaa akasogea akiwa umbali kama hatua 20 akamwambia yule dada(naamini ni mkewe)....."weeeee" kwa sauti ya ukali..... yule dada alivyostuka akamwonyesha ishara(kibabe) waondoke

Nikavutiwa sana na tukio.Wakasogea kituo cha daladala na mimi nikowafuata karibu. Binti akamzunguka jamaa akaenda kusimama nyuma yake akiwa hana raha. Jamaa akaita bodaboda akapanda bila kumsemesha yule binti na kuondoka. Yule binti naye akaita yake na kumfuata

Kwa kweli imenifikirisha sana wanandoa tena wa umri huu(kwa muonekano ni chini ya miaka 35) wanawezaje kuishi maisha haya kama wanyama?
Naomba Mungu asinifikishe hapa

Ulikuwa unawafuata ulikuwa unataka kupiga mzinga ama!,usirudie tena wangejua unawadadisi wangekuteka nyara
 
Unafikiri ndoa ni kama film za kifilipino au kikorea eeh?
Ndoa ni zaidi ya
EPL
Bundasliga
 
Mleta mada, ulipata nafasi ya kusikiliza upande wa pili!? Unajuaje kama huyo mke hana mapungufu yake katika hiyo ndoa/mahusiano !? Tusiwe wepesi kutoa hukumu....ndoa zina changamoto lukuki.

Miaka ya nyuma kuna Mzee mmoja alikuwa rafiki wa baba yangu,mbele za watu alikuwa mbabe sana kwa MKE wake. Nyumbani kwao kulikuwa na kiglosari cha pombe. Ikifika usiku wakiingia ndani unaambiwa Mzee alikuwa anachezea Makonde kutoka kwa mkewe balaa. Kesho yake hatoki ndani,utasikia Mzee leo Presha inamsumbua amepumzika. Kumbe kachezea vitasa anauguza manundu....maana alikuwa mweupe kwa hiyo akitoka siku ya pili inajulikana alipigwa,akawa anajitetea kwa washkaji zake eti ana allergy na dawa za Presha ndio zinamvimbisha uso. MKE wake alikuwa Mnyakyusa.
 
Back
Top Bottom