Mungu nisaidie nisifikie hatua hii!!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,102
114,703
Jamani kuna watu wanaishi maisha ya ndoa kwa kuvumilia sana!Hakika mwanamke kapewa moyo wa uvumilivu sana. Mwanamke anaweza fanyiwa ubandidu na madharau na mumewe lakini akaendelea kukomaa tu kama vile aliokotwa porini na hana kwao

Asubuhi nimeshuhudia tukio la kusikitisha sana jamaa akimfanyia mkewe. Jamaa walikuwa bank akionekana kumuacha mkewe nje...baada ya kumaliza na kutoka alisogea alipokuwa mwanamke mmoja mpole aliyekuwa kapakatia kitoto cha miaka kama minne hivi cha kiume kilichofanana na jamaa!

Jamaa akasogea akiwa umbali kama hatua 20 akamwambia yule dada(naamini ni mkewe)....."weeeee" kwa sauti ya ukali..... yule dada alivyostuka akamwonyesha ishara(kibabe) waondoke

Nikavutiwa sana na tukio.Wakasogea kituo cha daladala na mimi nikowafuata karibu. Binti akamzunguka jamaa akaenda kusimama nyuma yake akiwa hana raha. Jamaa akaita bodaboda akapanda bila kumsemesha yule binti na kuondoka. Yule binti naye akaita yake na kumfuata

Kwa kweli imenifikirisha sana wanandoa tena wa umri huu(kwa muonekano ni chini ya miaka 35) wanawezaje kuishi maisha haya kama wanyama?
Naomba Mungu asinifikishe hapa
 
Huwa nawaza sana kuusu ndoa yangu apo baada nataman sana tuje kua na furaha mda wote na mke wangu, na naamini itakua ivyo tu
Mikwaruzano lazima hata kama ni kwa 0.001% ipo tuuu

Cha msingi muombe Mungu akupe uvumilivu na moyo wa kiume.
Ndoa ni kuvumiliana tu hakuna trick nyingine zaidi ya hiyo
 
Masikini huyo mdada pole yake hiyo sio ndoa ni ndoano
Bado mapema kutoa hitimisho la namna hiyo, unawezakuta kilichotokea nyuma ni bonge la story na kile kilichoonwa na mleta mada kikawa ni risiti na sio bili yenyewe.
Ndoa ngumu wakuu acheni utani

Applause is a receipt not a bill
 
Hata wao hawakupenda kuwa hivyo,kumbuka mwanzoni walikuwa na furaha muda wote.

Ila mkuu umetisha sana,ukaacha mambo yako ukawafungia tela kujua mwisho wao.
 
Back
Top Bottom