Mungu ni mmoja na hajaribiwi

Mungu ni mmoja na hajaribiwi

Mnamo tarehe 1 mwezi huu wa tisa kulitokea kupakatwa kwa jua, watalaam wa mambo ya kidunia walitabiri hili swala na kujionyesha wajuaji zaidi walitabiri mpk muda na sehemu pia,
lakini nimeshindwa kuelewa hawa wanaojiita wanasayansi mbona hawakutuambia kuhusu tetemeko la ardhi kwamba litatokea lini na wapi na muda pia?
nadhani sasa ni wakati wao kuamini MUNGU yupo.
Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?
 
Nyani Ngabu umenikumbusha kuna rafiki yangu juzi nilimwambia amuombe Mungu akasema bora aniombe mimi huyo Mungu hajui atamuona wapi? Hapo nikaondoka mwenyewe sikai na watu wenye kejeli na Mungu. Nakuja na suali lakini nageuza upande. Kwahio unamaanisha hakuna Mungu ndio maana hata Yesu akafikia kusulubiwa kutokana hajapata msaada kutoka kwa Mungu?

Mimi sina uhakika kama mungu yupo au la.

Ila, dalili zote zinaonyesha kuwa hayupo.

Na sihitaji hata kukuambia hizo dalili ni zipi.

Kama una akili basi naamini hata wewe utakuwa unazijua tu.
 
Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?
Mungu siku zote ni mwema na hata na ndio maana nikaanza kwa kusema juzi kati hapa nyie wataalam wa sayansi mlitutabiria kupatwa kwa jua lakini katika hili imeshindikana na Mungu kuna kipindi anaonyesha ufalme wake kama hivi ili wasioamini waamini.
 
Nimezaliwa na kulelewa kwenye familia ya Kikatoliki lakini si muumini wa imani yoyote ile ya kidini.

Mimi ni agnostic.
basi mkuu mpk hapo hatuwezi kuelewana kwenye issue ya imani ya dini, naamini unasababu zako na mie pia nina sababu zangu za kuamini
 
Mimi sina uhakika kama mungu yupo au la.

Ila, dalili zote zinaonyesha kuwa hayupo.

Na sihitaji hata kukuambia hizo dalili ni zipi.

Kama una akili basi naamini hata wewe utakuwa unazijua tu.
Mmiliki wa nyumba ndio mwenye waraka wa hio nyumba ana uamuzi wa kuiuza au hata kuikodisha kwahio hata Mungu ana uwezo wa kufanya atakacho kwa kila alicho kiumba. Hajataka yeye aonekane ila kawaleta manabii ndio alama ya uwepo wake na amri kaiweka kwenye vitabu vyake. Kila nchi ina kiongozi wake(Rais) sasa kwanini dunia isiwe na Muumba wake amabae ndie Mungu?
 
Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?
Ikiwa Mungu katukataza kufanya maasi,dhulma,uonevu,tuishi kwa kumuomba yeye lakini kutwa tupo kwa waganga, hivi bado tu unataka na yeye Mungu asitupe adhabu japo kidogo? na kutukumbusha uwepo wake. Kuna kiongozi ana miezi 10 tu na kutwa anasema yeye hajaribiwi jee huyu Mungu wa milele?
 
Usiniambie kuwa mpaka watoto wasioweza hata kuongea nao huenda kwa waganga kupiga ramli.. !
 
Tulishindwa na nani?

Uliambiwa tunajua kila kitu?

Mungu wenu muweza wa yote, mwenye upendo, na aliyepo kila sehemu mbona kashindwa kulizuia tetemeko lisitokee leo?
Jeuri imezidi. There comes a time experience is the best teacher.
 
Mungu siku zote ni mwema na hata na ndio maana nikaanza kwa kusema juzi kati hapa nyie wataalam wa sayansi mlitutabiria kupatwa kwa jua lakini katika hili imeshindikana na Mungu kuna kipindi anaonyesha ufalme wake kama hivi ili wasioamini waamini.
Hujajibu swali langu.

Umefanya kama hujaliona, ingawa umelinukuu.

Narudia kuuliza, maana hujajibu.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?

Kama huwezi sema tu.

Utasemaje Mungu siku zote ni mwema wakati kaumba ulimwengu ambao unaruhusu matetemeko ya ardhi wakati alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu matetemeko ya ardhi?

Hujajibu swali.Unazidi kuongeza maswali.
 
Ikiwa Mungu katukataza kufanya maasi,dhulma,uonevu,tuishi kwa kumuomba yeye lakini kutwa tupo kwa waganga, hivi bado tu unataka na yeye Mungu asitupe adhabu japo kidogo? na kutukumbusha uwepo wake. Kuna kiongozi ana miezi 10 tu na kutwa anasema yeye hajaribiwi jee huyu Mungu wa milele?
Hujaelewa swali.

Jaribu kulisoma tena kwa makini Zaidi ili ulielewe.

Kama huwezi kulielewa Zaidi uliza usaidiwe.

Sijaandikalolote kuhusu adhabu, nimehoji kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, kabla ya chochote kuumbwa, alipokaa anapanga kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, adhabu haihitajiki, adhabu ya nini wakati mabaya hayawezekani?

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu huo?

Hujajibu swali hili. Unaongelea adhabu, kitu ambacho ni matokeo ya ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, kitu ambacho ni nje ya swali langu.

Umeona jinsi ambavyo hujajibu swali langu?

Hebu lissome tena.

Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?
 
jamani mnisamehe kwa mapungu yagu ya kibinadamu.hivi.kunaulazima mungu akuonyeshe yote.au mnamnata ubaya aifunike hii dunia tukome wite
 
Wanasemaga absence of evidence is not evidence of absence.sio kila usilokuwa na ushahidi nalo basi halipo.nahisi huko mbeleni sayansi itakuja kuprove uwepo wa mnyaazmungu.
Nikichogundua ni kuwa wengi wanaotetea uwapo wa mungu hawana arguments zenye mashiko,wengi huanza kutumia vitabu vya dini zao kitu ambacho kinachekesha kama sio kusikitisha
 
Back
Top Bottom