Mungu ni mmoja na hajaribiwi

Mungu ni mmoja na hajaribiwi

mweka mada umesema yote hayo lkn hospitali unaenda kufanyeje sasa..? kaa nyumbani usubiri muujiza kila unapoumwa
 
Mnamo tarehe 1 mwezi huu wa tisa kulitokea kupakatwa kwa jua, watalaam wa mambo ya kidunia walitabiri hili swala na kujionyesha wajuaji zaidi walitabiri mpk muda na sehemu pia,
lakini nimeshindwa kuelewa hawa wanaojiita wanasayansi mbona hawakutuambia kuhusu tetemeko la ardhi kwamba litatokea lini na wapi na muda pia?
nadhani sasa ni wakati wao kuamini MUNGU yupo.
Nani kakuambia sayansi inamajibu yote au ina weza kutabiri kila kitu perfectly?
 
kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

mkuu kiranga,
Binadamu wote tumeumbwa na MUNGU, na kabla ya Mungu kumuumba binadamu aliumba kwanza dunia ambayo ndio yatakuwa na yamekuwa makao yake, mungu alitumia mda mrefu zaidi kuumba dunia kuliko kumuumba binadamu.

jibu kwa swali lako
soma kitabu cha MWANZO 1:1-31 nanukuu
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
MWA. 1:1-31 SUV http://bible.com/164/gen.1.1-31.SUV

Kiranga hapo juu nukuu imekuonesha jinsi amabavyo Dunia iliumbwa katika namna rafiki kwa kuishi binadamu na hiyo ni kukanusha TUHUMA zako kwa MUNGU MWEZA YOTE. sijaona sehemu tetemeko la ardhi kama sehemu ya uumbaji wake katika ulimwengu, najua utaniuliza je matetemeko, mafuriko ,tsunami yametoka wapi??? ntakujibu ukihitaji.
 
Huyo mungu kwa nini kashindwa kulizuia hilo tetemeko lisitokee?

Au kalisababisha yeye?

Kama kalisababisha yeye, mungu gani huyo katili hivyo?

Maswali ya msingi kwa mtu anayetaka kumjua mungu;na Imani yake haijaishia ktk ukomo wa macho yake(seeing is believing ) ila roho yake

Mungu huleta matukio kwa nguvu zake; na nguvu hizo hutokeza njia za kufanikisha adhima ya mungu; scientist hufafanua njia siyo nguvu ya mungu
 
...........naendelea kukujibu kiranga na wafuasi wako.

alipokaa anapanga kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Katika ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, adhabu haihitajiki, adhabu ya nini wakati mabaya hayawezekani?

Kwa nini Mungu hakuumba ulimwengu huo?

MUNGU baada ya kumaliza uumbaji wa ulimwengu aliukabidhi kwa binadamu autawale na kuutisha kwa kila kitu,
soma MWANZO 1:26-29 nanukuu

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
MWA. 1:26?-?28 SUV
http://bible.com/164/gen.1.26-28.SUV

kwa hiyo mabaya na mitafaruku yote inayotokea ulimwenguni imesababishwa na binadamu mwenyewe kushindwa kuitawala dunia na kuitiisha maana tulipewa uwezo huo lakini kwa bahati mbaya zaidi UWEZO huo tukamkabidhi shetani na sasa anatumia kututesa.
Sasa bwana kiranga na wenzako wenye mitazamo ya kumlaumu MUNGU MWEZA YOTE mlitaka afanye nini???
 
MUNGU YUPO JANA LEO NA HATA MILELE. Kama wanasayansi ni Mabingwa watuletee njia mbadala ya kubeba MIMBA badala ya miez 9 inayotesa sana dd zetu ipungue.
 
Nadhani pia baadae utauliza kuwa kama Mungu aliumba viumbe wake, kwa upendo kwanini wawe wanakufa na wanaumwa, wanafanya kazi ndipo wape kuendesha maisha yao.
Kwa ufupi tu yote yanayotokea, yanatokea ili kwa wanaamini wapate kumcha Mungu, isipokua shetani na wafuasi wake. Hata wewe nyumbani kuna wakati unawajibika kumchapa mwanao, ili kukumbusha kuachana tabia, na vitendo usivyotaka.
Hilo swali ulilosema nitauliza hujalijibu, umelikwepa tu.

Kabla ya viumbe, shetani etc. alikuwepo Mungu tu.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya na shetani haviwezi kuwepo, akaumba ulimwengu ambao mabaya na shetani vinaweza kuwepo?

Hujajibu hili swali.
 
Mnamo tarehe 1 mwezi huu wa tisa kulitokea kupakatwa kwa jua, watalaam wa mambo ya kidunia walitabiri hili swala na kujionyesha wajuaji zaidi walitabiri mpk muda na sehemu pia,
lakini nimeshindwa kuelewa hawa wanaojiita wanasayansi mbona hawakutuambia kuhusu tetemeko la ardhi kwamba litatokea lini na wapi na muda pia?
nadhani sasa ni wakati wao kuamini MUNGU yupo.

Sidhani kama hiyo ilitokea...!
 
Kwa ufahamu wangu mimi ulimwengu usiokuwa na matetemeko na maangamizo ni ulimwengu anaoishi Mungu na Malaika wake. Lakini huu ulimwengu wetu tumeletwa kwa majaribio ya nafsi zetu, sasa kuna wanaokumbuka na wasio kumbuka kama Mungu yupo. Hakika Mungu halaeti hadhabu mpaka kufuru zinapovuka mipaka. Jibu lako kuwa anao uwezo wa huu ulimwengu kuwa na amani mpaka mwisho wake lakini yeye ndie mwenye amri ya nini akifanye kwenye ulimwengu wake. Hivi wewe huwezi kubomoa nyumba yako au kuwaondoa wapangaji wako hata mukiwa na mkataba?

Hujajibu swali nililokuuliza.

Mungu haleti adhabu mpaka kufuru zinapovuka mipaka?

Mimi sijauliza kwa nini tunapata matetemeko, ningeuliza hivyo jibu lako la kufuru lingeweza kuwa sawa (ingawa hata hilo nalo lingezaa maswali Zaidi, kwa nini watoto wadogo ambao hawajafanya baya lolote wanafariki katika matetemeko, Mungu hana huruma ya kusema asiwaadhibu ambao hawajafanya kufuru pamoja na wale waliofanya kufuru?)

Swali lang ni, pale Mungu alipokuwa anapanga kuumba ulimwengu, kabla hajaumbwa mtu, kabla hajaumbwa shetani, kabla haujaumbwa ulimwengu, kabla hakijaumbwa chochote, alikuwa ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya na shetani haviwezi kuwepo, kwa nini hakuumba ulimwengu huo?

Ukijibu habari ya kufuru, dhambi, shetani etc unakuwa hujajibu swali. Nimeuliza kabla vyote hivyo havijaumbwa hivyo jibu lako likiwa na chochote kati ya hivyo hujajibu swali.

Jibu linatakiwa kutoa sababu za kutoka kwa Mungu na reasoning yake.

Hujajibu swali.
 
mkuu kiranga,
Binadamu wote tumeumbwa na MUNGU, na kabla ya Mungu kumuumba binadamu aliumba kwanza dunia ambayo ndio yatakuwa na yamekuwa makao yake, mungu alitumia mda mrefu zaidi kuumba dunia kuliko kumuumba binadamu.

jibu kwa swali lako
soma kitabu cha MWANZO 1:1-31 nanukuu
Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja.

Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.

Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne.

Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho, ambavyo maji yalijawa navyo kwa wingi kwa jinsi zao, na kila ndege arukaye, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tano.

Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
MWA. 1:1-31 SUV http://bible.com/164/gen.1.1-31.SUV

Kiranga hapo juu nukuu imekuonesha jinsi amabavyo Dunia iliumbwa katika namna rafiki kwa kuishi binadamu na hiyo ni kukanusha TUHUMA zako kwa MUNGU MWEZA YOTE. sijaona sehemu tetemeko la ardhi kama sehemu ya uumbaji wake katika ulimwengu, najua utaniuliza je matetemeko, mafuriko ,tsunami yametoka wapi??? ntakujibu ukihitaji.
Hujajibu swali langu.

Umenipa stories nyingi za ulimwengu ulivyoumbwa, wakati swali langu limeuliza kabla ya Mungu kuumba chochote alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu wowote, pamoja na ulimwengu ambao hauruhusu matetemeko ya ardhi.

Evidently, kwa sababu tunaona matetemeko ya ardhi, na mnasema ulimwengu huu umeumbwa na Mungu.

Swali linakuja.

Kabla Mungu hajaumba chochote, kabla hajaumba dunia, kabla hajamuumba mtu, kabla hajaumuumba shetani etc alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani, ubaya wowote hauwezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo? Kwa nini kaumba huu ambao mabaya na matetemeko ya ardhi yanawezekana?

Hijajibu swali hili.
 
...........naendelea kukujibu kiranga na wafuasi wako.

MUNGU baada ya kumaliza uumbaji wa ulimwengu aliukabidhi kwa binadamu autawale na kuutisha kwa kila kitu,
soma MWANZO 1:26-29 nanukuu

Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
MWA. 1:26?-?28 SUV
http://bible.com/164/gen.1.26-28.SUV

kwa hiyo mabaya na mitafaruku yote inayotokea ulimwenguni imesababishwa na binadamu mwenyewe kushindwa kuitawala dunia na kuitiisha maana tulipewa uwezo huo lakini kwa bahati mbaya zaidi UWEZO huo tukamkabidhi shetani na sasa anatumia kututesa.
Sasa bwana kiranga na wenzako wenye mitazamo ya kumlaumu MUNGU MWEZA YOTE mlitaka afanye nini???
Unajibu bada ya Mungu kumaliza uumbaji wa ulimwengu wakati swali linauliza kabla Mungu hajaanza uumbaji wa chochote.

Hata hujaelewa swali linauliza nini, huwezi kunipa jibu, hujaelewa swali.

Kabla Mungu hajaanza kuumba ulimwengu, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezekani?

Ukinijibu kwa sababi mwanadamu alifanya mabaya hujaelewa swali, ninauliza kwa nini Mungu aliumba ulimwengu ambao mwanadamu ameweza kufanya mabaya wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mwanadamu hawezi kufanya mabaya?

Unanijibu kwa sababu mwanadamu alifanya mabaya.
 
Hilo swali ulilosema nitauliza hujalijibu, umelikwepa tu.

Kabla ya viumbe, shetani etc. alikuwepo Mungu tu.

Kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya na shetani haviwezi kuwepo, akaumba ulimwengu ambao mabaya na shetani vinaweza kuwepo?

Hujajibu hili swali.
Ndivyo alivyoamua iwe ili dunia ione kama ilivyo, ameamua kuweka Duniani mazuri na mabaya ikiwa na visababishi vya maisha ya viumbe hai, kufika ukomo, Nani awezae kuondoa apangalo Mungu, najua baadae utauliza kwanini ametuumba kuwa na hitaji la kula, kuvaa.
 
Sijauliza kama ndivyo au sivyo alivyoamua.

Nimeuliza kwa nini kaamua hivyo?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aamue kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Ukiniambia ndivyo alivyoamua, hilo si jibu. Hiyo ni premise ya swali. Swali ni kwa nini kaamua hivyo na si vingine ambavyo mabaya yasingewezekana kutokea?

Hujajibu swali hili.

Ukinijibu "ndivyo alivyoamua" unaonesha hujui sababu. Kama hujui sababu humjui huyo Mungu. Kama humjui huyo Mungu unasema Mungu yupo wakati humjui. Ukisema Mungu yupo wakati humjui unaweza kisema Mungu yupo wakati hayupo.

Kushindwa kwako kumuelezea huyu Mungu kunazidi kuonesha hayupo.
 
Duh umeua
Hajaua. Hiyo katika logic inaitwa "non sequitur".

Kwanza si kila anayepinga kuwepo kwa Mungu ni mwanasayansi.

Kwa nini kushindwa kwa Wanasayansi kuwe ni uthibitisho kwamba Mungu yupo wakati viwili hivi havina uhusiano wowote?
 
Mungu inawezekana yupo ila hajishughulishi na mambo ya wanadamu.
 
Back
Top Bottom