Mungu ni mmoja na hajaribiwi

Mungu ni mmoja na hajaribiwi

Mnamo tarehe 1 mwezi huu wa tisa kulitokea kupakatwa kwa jua, watalaam wa mambo ya kidunia walitabiri hili swala na kujionyesha wajuaji zaidi walitabiri mpk muda na sehemu pia,
lakini nimeshindwa kuelewa hawa wanaojiita wanasayansi mbona hawakutuambia kuhusu tetemeko la ardhi kwamba litatokea lini na wapi na muda pia?
nadhani sasa ni wakati wao kuamini MUNGU yupo.

Teknolojia hiyo ipo, ila sidhani kama mamlaka za geology Tanzania wanayo, au hawapokei taarifa kutoka US au EU kuhusu matetemeko kwa kuwa ni adimu Tanzania.

Soma zaidi hapa:
Earthquake warning system - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Sijauliza kama ndivyo au sivyo alivyoamua.

Nimeuliza kwa nini kaamua hivyo?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aamue kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Ukiniambia ndivyo alivyoamua, hilo si jibu. Hiyo ni premise ya swali. Swali ni kwa nini kaamua hivyo na si vingine ambavyo mabaya yasingewezekana kutokea?

Hujajibu swali hili.

Ukinijibu "ndivyo alivyoamua" unaonesha hujui sababu. Kama hujui sababu humjui huyo Mungu. Kama humjui huyo Mungu unasema Mungu yupo wakati humjui. Ukisema Mungu yupo wakati humjui unaweza kisema Mungu yupo wakati hayupo.

Kushindwa kwako kumuelezea huyu Mungu kunazidi kuonesha hayupo.
Kuto jua maamuzi hakumaanishi kuwa alieamua humjui, kiswahili hakimainishi hivyo, hata Baba nyumbani anaweza akaamua jambo nyumbani, watoto wasijue kwanini baba kaamua hivyo, na wala haina mana hawamjui baba yao.

Kijumla kuto jua maamuzi ya mtu hakumaanishi alie amua hajulikani. Ukisema Mungu hayupo, Kwa kuwaeleza watu wenye imani yao Kama mimi, Naingia ndani ya imani yangu, nikiangalia Tupo kwenye forums ambayo watumiaji wengi wanatumia ID bandia. Nafasi ambayo shetani hutumia kutuma watu wake kujipatia wafuasi kwa kuwarubuni wenye nafasi nyepesi, sina hakika sana na wewe kama sio miongoni mwao.
 
Huyo mungu kwa nini kashindwa kulizuia hilo tetemeko lisitokee?

Au kalisababisha yeye?

Kama kalisababisha yeye, mungu gani huyo katili hivyo?

Asipokuchapa kiboko utajua je yupo? Ngoja na wewe upate pigo moja utajua kuwa yupo ama hayupo🙁🙁🙁
 
Mnamo tarehe 1 mwezi huu wa tisa kulitokea kupakatwa kwa jua, watalaam wa mambo ya kidunia walitabiri hili swala na kujionyesha wajuaji zaidi walitabiri mpk muda na sehemu pia,
lakini nimeshindwa kuelewa hawa wanaojiita wanasayansi mbona hawakutuambia kuhusu tetemeko la ardhi kwamba litatokea lini na wapi na muda pia?
nadhani sasa ni wakati wao kuamini MUNGU yupo.
Mada nyingine za kijinga sana? Kwahiyo unataka kusema mungu ndo kaleta hilo tetemeko? Mpaka aue watu ndo uje hapa useme yupo??
 
Kama Mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini aumbe ulimwengu ambao tetemeko la ardhi linawezekana na linaua mpaka watoto wasio na hatia wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao matetemeko ya ardhi hayawezekani?

Unaweza kunijibu swali hili?

Ni sawa na kuwa na mwanao then kila kitu unampatia, mpaka anakuwa jitu zima bado unanunulia mpaka chupi?😵

Usipompa changamoto hatafikiria namna ya kujitegemea, na kutumia uwezo wake kukabili mazingira aliyopo.

Sometime Mungu anatupa changamoto ili kuitumia akili aliyotupa kukabili mazingira tuliyopo. Ikiwa ni pamoja kutufunza nidhamu ili tuishi vizuri na akili zikae sawa🙁

Mungu yupo na yu hai kabisa na mauweza yake.
 
Labda sayansi yao ni ya angani tu na hata ka ingekuwa ya angani tu matukio ya ajali ya ndege tunazoziona yasingekuwepo.
 
Unabishana na mmtu ambaye hajui hata sekunde moja ijayo nini kitatokea.mcpoteze muda wenu bure kuna watu hubishana ili wajue zaidi
 
Mada nyingine za kijinga sana? Kwahiyo unataka kusema mungu ndo kaleta hilo tetemeko? Mpaka aue watu ndo uje hapa useme yupo??
Maswali mengine ya kijinga sana yaani ndio umetulia kabisa ukaandika swali la ugoro kama hili? Siku nyingine jifunze kujibu kwa hoja ili tupime nani ni mjinga kati yako na mleta mada wakati na wewe mwenyewe ukiwa mbumbu tu
 
Umejuaje kama nimetulia kabisa?
 
Miungu iko mingi sana! Tena yote inajaribiwa na haifanyi lolote kwasababu hata haijiwezi yenyewe
 
Nyani Ngabu umenikumbusha kuna rafiki yangu juzi nilimwambia amuombe Mungu akasema bora aniombe mimi huyo Mungu hajui atamuona wapi? Hapo nikaondoka mwenyewe sikai na watu wenye kejeli na Mungu. Nakuja na suali lakini nageuza upande. Kwahio unamaanisha hakuna Mungu ndio maana hata Yesu akafikia kusulubiwa kutokana hajapata msaada kutoka kwa Mungu?
Ndio
 
Watu wanatumia matukio kama ajali kuthibitisha uwepo na uwezo wa mungu.

Hii inaonyesha imani juu ya uwepo wa mungu imejengwa kwenye woga. Fear! Na zaidi ya hapo inaonyesha imani hii inaabudu mungu katili. Mungu mwenye kuonyesha uwezo wake kwa kuleta madhara.

Usipoamini mungu utaenda motoni. Hivyo unaamini ili ukwepe moto hata kama huwezi kuimba mapambio 24/7.

Watu wanasahau mambo mazuri na mabaya yanawatokea wanaoamini na wasioamini.

Leo basi likipata ajali wakafa wote kasoro mmoja. Wale waliokufa watu watasema ni mapenzi ya mungu. Aliyebaki ataenda kuomba misa ya shukrani. Lakini yote haya yamefanyika kwa mapenzi yake mungu.

It makes you wonder kama hawa watu wana vichwa sawa vya kufikiri.
 
Wanatambua kuhusu matetemeko ila wanatilia manani zaidi kwenye vivutio kiliko maafa...
 
Kuto jua maamuzi hakumaanishi kuwa alieamua humjui, kiswahili hakimainishi hivyo, hata Baba nyumbani anaweza akaamua jambo nyumbani, watoto wasijue kwanini baba kaamua hivyo, na wala haina mana hawamjui baba yao.

Kijumla kuto jua maamuzi ya mtu hakumaanishi alie amua hajulikani. Ukisema Mungu hayupo, Kwa kuwaeleza watu wenye imani yao Kama mimi, Naingia ndani ya imani yangu, nikiangalia Tupo kwenye forums ambayo watumiaji wengi wanatumia ID bandia. Nafasi ambayo shetani hutumia kutuma watu wake kujipatia wafuasi kwa kuwarubuni wenye nafasi nyepesi, sina hakika sana na wewe kama sio miongoni mwao.
Tatizo si kutojua sababu ya maamuzi tu.

Unaweza kuona baba kamwambia houseboy asafishe gari Jumanne, wakati kawaida gari linaoshwa Jumapili.

Usijue sababu ya kwa nini baba kaamua hivyo. Hilo halina ajabu sana. Kwa sababu inawezekana kuna sherehe baba anaenda.

Tatizo linakuja unaambiwa baba mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anapoamua kukataa watoto wake asisome shule, kuwaletea magonjwa bila ya kuwapa dawa, na kuwaachia wafe wakati anaweza kuwaponya. Tena anaachia ajali zinazozuilika zitokee na kuua hata vitoto vyake vichanga.

Ukiambiwa kuna baba huyo, na ni baba mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote utakubali hilo?

Huoni kwamba habari hii inajipinga?
 
Ni sawa na kuwa na mwanao then kila kitu unampatia, mpaka anakuwa jitu zima bado unanunulia mpaka chupi?😵

Usipompa changamoto hatafikiria namna ya kujitegemea, na kutumia uwezo wake kukabili mazingira aliyopo.

Sometime Mungu anatupa changamoto ili kuitumia akili aliyotupa kukabili mazingira tuliyopo. Ikiwa ni pamoja kutufunza nidhamu ili tuishi vizuri na akili zikae sawa🙁

Mungu yupo na yu hai kabisa na mauweza yake.
Kwa hiyo Mungu ni sawa na mtu?

Mtu alipata uwezo wa kuumba ulimwengu vyovyote vile anavyotaka?
 
Back
Top Bottom