Watenda mabaya wanahukumiwa Broo.
Acheni Siasa kwenye Imani za watu.
Unapotaja Dini ya Kikristo unazungumzia ufalme Wa Mungu hapa Duniani na wanadamu ndio waliowekwa Ili waujenge juu ya msingi Wa Kristo.
Hakuna ufalme unaojengwa kirahisi. Ukristo imejengwa kwa upanga kama ulivyo uislamu. Waliotangulia walipambana sana kuleta utawala Wenye Sheria za Kikristo.
Una bahati umezaliwa kwenye nchi ambayo tayari watu walipambana na kujenga misingi hiyo ! Mshukuru Mungu kuzaliwa zama ambazo unakaa pembeni serikali inakulipia Kisasi.
Leo hii unaweka ukaona Wakristo wakikaa pembeni wanaona Makanisa yananajisiwa na watu wanaoana na kufunga ndoa za jinsia Moja wanasema kuwa Vita yetu si juu ya damu na Nyama Huku ushoga ukiwa unaenea Kwa Kasi.
Sasa unajiuliza ni Mungu Yupi wanataka aje ajipiganie Wakati amewaweka hapa Duniani Ili wafanye KAZI yake Kwa utukufu wake?
Wakristo wamejazana kwenye mabaa na madanguro wanalewa na uzinzi halafu wanawaachia Mashoga na Mabasha wanapanga Nani aongoze na kutawala na kutunga Sheria za Dunia kinyume na Mipango ya Mungu. Wakristo Wa Sasa wamepotoka na ni waoga?
Biblia inasema waoga na wasioamini sehemu yake ni Katika lile Ziwa liwakalo moto na Kiberiti.
Wakristo watatupwa Nje Kwa sababu wameondoka kwenye Jukumu la kuujenga ufalme Wa Mungu Duniani. Hakuna ufalme Wa Mungu unaotawaliwa na waovu.
Wakristo wanapaswa kuwa Chachu ya Utawala Wa Haki isiyotoka Nje ya Neno la Mungu. Hakuna haki Kwa watenda dhambi.
Basi tuache kuwa na Majeshi mana hatuna vita ya kimwili . Haiwezekani mana tuna KAZI ya kuujenga ufalme Wa Mungu kimwili na KIROHO. Paulo alitaka watu wale wanafunzi wake wazame zaidi kwenye ulimwengu Wa roho Ili vita ianzie Rohoni na kuonekana mwilini Katika kukemea dhambi na kujenga misingi ya Kikristo kwenye Tawala na mamlaka za kimwili ambazo zitasimama Katika kulipa kisasi Badala ya Mungu.
Serikali ni Watu na zinapaswa kuadhibu Kwa haki Badala ya Mungu.
Serikali zinapaswa kuwa chini ya Kristo .
Ukiona serikali hazitendi haki Ujue Wakristo wamelala.
Dunia imefikia ilipo Kwa sababu Wakristo Wa kweli wamelala na ni waoga. Wanazipenda nafsi zao matokeo yake wanajificha Nyuma ya mistari ya kuwa YESU alisema asiye na dhambi awe Wa kwanza kumpiga . Lakini Nenda mahakamani uone walivyojazana kwenye kesi za kugombania mpaka maiti kuzika.


