Mungu hakuwa na mpango wa kuwa na binadamu zaidi ya Eva na Adam

Stavros Myles

JF-Expert Member
Jun 7, 2020
350
390
Nawapa Hi wana Jukwaa wote wa JamiiForum ila salamu zangu nyingi nawapa wana Jamii Intelligence.

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu, ila naomba nitoe angalizo kwa wale wadau wanaochangia jambo kwa makasiriko au hisia zao kali, mada hii inaweza isiwe kwa ajili yako.


Naomba niende moja kwa moja na mada ( Mungu hakuwa na mpango wakuwa na binadamu zaidi ya Eva na Adam ). Naomba kwanza kabla sijaenda mbele nitoe mahali ambapo unaweza kupatumia kama reference, soma kitabu cha Mwanzo katika Biblia Takatifu kwenye Agano la Kale.


Baada ya hapo naomba niendelee, kwa mujibu wa Biblia Adam alikuwa wa kwanza kabisa kuumbwa na baada ya yeye (Adam) kuwepo m/Mungu akaamua kutumia ubavu wa Adam kumuumba Eva (Eve). Eva aliumbwa kama msaidizi wa Adam, na siku zote wakiwa wanaishi Adam na Eva walikuwa wanaishi wakitembea na kufanya mambo mengi wakiwa watupu kabisa (Hawana nguo ). Hapa naomba niweke utuo kidogo, ukirudia kuisoma Mwanzo katika Biblia utakutana na kisa cha Eva kudanganywa na Ibilisi/Shetani/ Shweitani (though sina hakika na Uandishi wa hili neno la mwisho). Baada ya Eva kukubali kula tunda ambalo Mungu aliwakataza wasile alimshawishi Adam naye ale lile tunda. Baada ya kula lile tunda Adam na Eva wakajikuta wako tupu kabisa (Yaani Naked..nyama nyama ). Kabla sijaenda mbali nataka nijaribu kuchambua sentensi yangu niliyoiandika " Baada ya Eva kukubali kula tunda ambalo Mungu aliwakataza wasile ". Kama Mungu aliwakataza kula lile tunda la mti wa ujuzi wa mema na ubaya ina maana halisi na ya kawaida ya kwamba hakutaka wajijue ya kwamba walikuwa watupu (bila nguo) na kama wangejijua kama walikuwa tupu/naked wangetamaniana na mwisho wa siku wangefanya ngono/mjamiiano then mwishowe wangepata watoto na kuongezeka. Sasa kufikia hapa tunatakiwa tujue Mungu hakutaka uwepo wa binadamu wengine wengi isipokuwa uwepo wa Adam na Eva licha ya kuiumba dunia na Sayari nyingine nyingi. Kuna maswali mazito mengi hapa, sasa kwanini Mungu aliumba Ulimwengu mkubwa huu ambao hakutaka watu wengine wawepo (rejea hapo juu!) ?, Je Mungu alipanga kuwaumba viumbe wengine ambao alitaka wakae katika sehemu nyingine za dunia akiwa anawaweka Adam na Eva kwenye bustani?.

Sasa naomba niachane na mambo ya hapo juu tushuke kidogo hapa. Baada ya Adam na Eva kula lile tunda walifukuzwa kwenye ile bustani ya Eden na wakiwa huko walizaliana na kuanza kuongezeka, ila bado hata huu uzao haukuwa na baraka zozote za moja kwa moja kutoka kwa Mungu kwani hata majibu ya Adam yalikuwa yaliyojaa kiburi kizito mno kwani baada ya kuulizwa na Mungu kwanini alikula tunda alijibu " Si huyo mwanamke uliyenipa ndo kasababisha ".

Kwa sisi tuliopo kwa muda huu kama si Mungu kumtoa Yesu kristo kuja kutuokoa kwa kufa pale msalabani hatukuwa na thamani wala uhalali wa kuishi kabisa.


Nawasilisha, nakaribisha mawazo yenu. 🔌
 
umesema walikuwa adam na eva tu..ivi kaini alienda kumuoa nan kule nchi ya nodi,? dunian walbak watatu tu baada ya habili kufa, yaan walbak adam,eva na kain kabla watoto wengne kuzaliwa. kaini alpata wapi mke?
Mkuu, Torat, Biblia na Quran si vitabu vya ukweli, usiviamini hata. Ni hadith tu ambazo don't make any sense kwa mtu wa JF (Great Thinker).
 
Kwa ushauri tu ndugu yangu tafuta habari za Adam na Eva kupitia
Annunak Chronicles utapata picha na hizo habari Kwa angle tofauti Sana na hizo za Biblia

Annunak Chronicles inaelezea adamu ni cloning project na human manipulation iliyofanywa kisayansi na hao Alliens Tena inaelezea kisayansi combination ya DNA ambazo Leo zimewasaidia kufanya cloning Kwa wanyama mbali mbali ingawa Kuna majaribio ya binadamu ila ni Siri
Hiyo Elimu yote imekutwa kwenye Accient tablets za SUMERIAN ,

Hizo mythology hazipo kama mnavyofikiria nyie watu wa Dini ni zipo tofauti sana na zimekaa kisayansi Zaidi kuliko Imani Kiasi kwamba ukiambiwa hapa utakataa kabisa ,
Usije ukadhani Yale maandiko ya kale ya binadamu kukutana na Miungu na kuongea nao ni Hadith la hasha ni kweli hapo Mwanzo Dunia ilipata kaliwa na Viumbe ambavyo watu waliwaita Miungu !
 
Mi nahisi labda Mungu Alikua na njia nyingine ya binadamu kuongezeka zaidi ya hiyo ya kufanya ngono.
 
mm nafikil ungetoa jb kwrnye swali lake kulko kumuita mjnga kuna point y maana sn hapa
Ni mjinga na wewe acha ujinga,amejinasib kuwa ametoa maandiko ya kwenye biblia (kuwa ameisona vizuli.)biblia hiyo hiyo kwenye kurasa hiyo hiyo inajibu swali lake.sasa mtu Kama huyo unamuitaje?
 
Mungu alimuumba adamu akiwa na uwezo wa kuzaa kabla hajaumbiwa Eva.Eva alikuja ili awe na uwezo wakuzaana na adamu.Hayo mengine ya kwako nenda kasome upya andiko lako ujue concept iliyotumika.
 
Back
Top Bottom